Wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kufanya mtihani mwingine

Hii ni proficiency test inafanywa kila mwaka kwa form 1 kubaini wasiojua kusoma,kuhesabu na kuandika sema sasa hivi itasimamiwa na NECTA kwani bado kuna ujanja ujanja hawataki kuonesha ubovu wa wanafunzi wanalinda vyeo na ajira zao
 
Ufanisi utapatikanaje wakati msimamizi kazi ya wiki nzima analipwa laki moja tu? Kwanini mwenyeji akiongeza laki nyngne nisimpe mzigo? Haya, shule INA walimu wanne toka darasa la kwanza had Ia saba. Uchawi gani utatumika kukamilisha masomo hapo? Mwalimu mkuu wa shule isiyofaulisha atawajibishwa na kudhalilishwa, nani atakubali kudhalilishwa? Pana mengi ya kutatua,lakini yamefumbiwa macho. Matokeo yake ni kupeleka vihiyo sekondari.
Ndo haya yote yafanyiwe kazi, si kuwafanyisha watoto wetu mitihani mara mbilimbili kwa upimwaji wa jambo lilelile.
 
MUUMBA aione hii nchi na awape viongozi utashi wa kuiona "Future" ya nchi yao itakavyokuja kuwa huko mbele japo kwa dakika 1 tu.
Hapa naona kuna "WALIMU a.k.a WASIMAMIZI WA MITIHANI" wakitafutiwa lawama na hata kuweza kuambiwa walifanya "CHEATING" kwenye kazi hyoo...
I can n I'll mengi round hii
 
Gharama zote zilizotumika katika kufanya ule Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba leo wanasema warudie? Bado sijamuelewa Ndalichako. Ina maana:
-Aidha wasahihishaji wa ule mtihani hawaaminiki?
-Watungaji wa ule mtihani hawana sifa?
-Vigezo vya ufaulu havina ukweli?
-Mtihani ulivuja?
-...,...
Kiongozi wangu hapo ndo tukubali kwamba tunaongozwa na nanga!!
 
Safi sana kwa uamuzi huo wa kuchuja makando kando na kubakisha wanaostahiri ila ushauri wangu kwa necta murudishe mitihani ya kufanya wanafunzi wenyewe tuondoe maswali yote ya kuchagua hadi hisabati.
 
Sasa haina haja ya drs la 7 kufanya mtihani wa NECTA wawe wana wa subiria huko form 1 ili kuokoa hizo kodi zetu.
 
Nchi ya maajabu na vituko, mliwambia kuwa watakuja kufanya paper nyingine au mmeamua tu from no where! ! kazi ipo
 
Hawa wanafanya siasa kwenye elimu kweli Ndalichako acha mizaha na elimu yetu,juzi wale form two waliorudia mwaka jana na wamefeli tena wameagizwa waendelee kidato cha tatu na div.zero zao.sasa mbona hakuna uhusiano wa matukio la saba hesabu za kuchagulia hata wasiojua kusoma na kuandika wamefaulu kwa wastani wa B,form one uwachuje na kamtihani ka hovyo,form two wanavuka tu
Hii nchi usanii utaisha na watu wakawa siriasi na kile wanachofanya kweli? Mbona kila siku tamthilia zinaendelea tuu. sioni muunganiko wa nukta hapa. kwani HV cc tumerogwa au. ahh haya bhana
 
Watafanya mtihani wa masomo ya shule ya msingi, au walipojifunza kuanzia shule zilipofunguliwa kidato cha kwanza!!!!?

Wakati mwingine tunaingia gharama kubwa kwa kitu ambacho umakini ungekuwepo katika mitihani ya darasa la saba, haya yoye yasingetokea.

Kuna uwezekano wa kuwahukumu watoto kwa makosa ambayo siyo yao, hasa wale wajuzi wa kubahatisha.
Watu waliponda sana walipoanzisha mitihani ya kuweka vivuli kwa kubahatisha. sasa wao wenyewe Hawaiiamini mitihani yao.
 
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa
wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika
kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na
wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato
hicho.
Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu
Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt.
Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka
NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya
Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa
Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao
hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo
hayo ya sekondari.
NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki
uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao
cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu
ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli
hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka
sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa
elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za
serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha
orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.
Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili
ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi
wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa
taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote
yatakayojitokeza,” alisema.
Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi
uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya
mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi
hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi
wote waliofanya mtihani huo.

Hii serikali duh! Kwa hiyo, mtihani waliofaulu hauna maana?

Lililo nyuma ya pazia ni hili.

Watoto wamefaulu kupita kiasi. Serikali haikujiandaa kuwapokea. Shule za sekondari, walimu, vifaa, bajeti haitoshi. Hivyo, ili kuwapunguza ni kutafuta au kuweka kizingi kipya.
Lengo la mtihani huu ni kuwapunguza, serikali itakuwa haina fedha ya kuwapokea na kuwasomesha wote.

Mbinu za vigezo na masharti mapya, ni mbinu ambayo serikali imeitumia kwa miaka mingi kupunguza wenye haki ya kuhudumiwa na serikali. Kumbuka bodi ya mikopo, kumbuka sababu za kutopandisha watumishi mishahara, vyeo na madaraja.

Serikali hii inakotupeleka siko
.
 
Back
Top Bottom