Mkuu, Mimi nimesoma haka kauzi kote. Ila hii hoja imenigusa sana. Mwanangu namjua uwezo wake. Lakini nikaambiwa lazima apelekwe sekondari (vipaji). Nimempeleka. Leo akirudishwa nani atarudisha kasenti kangu, manake nilitumia kama kilo saba hv ambayo sikuwahi kushika yangu nizaliwe.mimi wasiwasi wangu ni sehemu Mbili,moja kuna baadhi ya watoto na wazazi wao wanalazimishwa tu kwenda sekondari sasa wakipata fursa hii ndo watafurahi kwani mwanafunzi ataamua kufanya vibaya ili asiendelee na masomo.Pili wazazi waliojibana mpaka kupata mahitaji ya mtoto je watafidiwaje kwa sababu sio kosa lao wao walitii amri ya kupeleka watoto shule,
Lazima watanzania watambue matatizo ya nchi hii sababu ni ccmYani hii nchi sijui kairoga nani... sasa wanapoteza ela tu maana mtihani wa taifa basi hauna maana tena.
Yani imefika kipindi hata mitihani yao ya taifa hawaiamini tena
Wewe una waamini mkuu?Hapa sipati mantiki yake, ni kama vile baraza haliwaamini waliosimamia mitihani ya drs la saba au wasahishaji. Mi nadhani, wangeongeza tu ufanisi ktk usimamizi wa mitihani.
Mkuu umeongea point yangu heshima kwako nakupa dah kibaya ni kwamba mtoto amekaa miezi yote ndo ameanza kusoma mambo mapya halafu umpe mtihani wa la sabaKama wabovu walifaulu vipi hiyo mitihani ya necta?
Kumbuka siku za karibuni Ndalichako alizuia Shule binafsi(private schools) kuwafanyisha mitihani ya mchujo wanafunzi wanaokwenda kusoma private schools, sasa hiki kinachotaka kufanywa na necta(serikali) kina tofauti gani na kile kilichokua kikifanywa na Shule binafsi?
Na vipi kuhusu wataofeli huo mtihani watapelekwa wapi sasa?
Hii serikali ya kutafuta kiki sana hii
Siwaamini sana, ila njia bora nadhani ingekuwa kuiimarisha taasisi hisika si kuwafanyisha mtihani upya. Hata kwa muda waliokaa mtaaani laweza kuwa ni shida kwa wale waliokuwa zima moto.Wewe una waamini mkuu?
Nina Imani Kama wako siriaz na paper itafanyika kwa Usimamizi makini ni wanafunzi laki moja tu watapata nafasi ya kuendelea wengine wote watafeli vibaya sanaaaBaraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa
wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika
kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na
wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato
hicho.
Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu
Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt.
Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka
NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya
Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa
Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao
hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo
hayo ya sekondari.
NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki
uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao
cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu
ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli
hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka
sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa
elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za
serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha
orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.
Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili
ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi
wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa
taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote
yatakayojitokeza,” alisema.
Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi
uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya
mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi
hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi
wote waliofanya mtihani huo.