Wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kufanya mtihani mwingine

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa
wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika
kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na
wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato
hicho.
Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu
Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt.
Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka
NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya
Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa
Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao
hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo
hayo ya sekondari.
NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki
uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao
cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu
ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli
hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka
sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa
elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za
serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha
orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.
Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili
ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi
wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa
taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote
yatakayojitokeza,” alisema.
Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi
uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya
mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi
hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi
wote waliofanya mtihani huo.
 
Hawa wanafanya siasa kwenye elimu kweli Ndalichako acha mizaha na elimu yetu,juzi wale form two waliorudia mwaka jana na wamefeli tena wameagizwa waendelee kidato cha tatu na div.zero zao.sasa mbona hakuna uhusiano wa matukio la saba hesabu za kuchagulia hata wasiojua kusoma na kuandika wamefaulu kwa wastani wa B,form one uwachuje na kamtihani ka hovyo,form two wanavuka tu
 
Watafanya mtihani wa masomo ya shule ya msingi, au walipojifunza kuanzia shule zilipofunguliwa kidato cha kwanza!!!!?

Wakati mwingine tunaingia gharama kubwa kwa kitu ambacho umakini ungekuwepo katika mitihani ya darasa la saba, haya yoye yasingetokea.

Kuna uwezekano wa kuwahukumu watoto kwa makosa ambayo siyo yao, hasa wale wajuzi wa kubahatisha.
 
Hii nzuri nimeipenda. Watuondolee watoto wabovu.
Kama wabovu walifaulu vipi hiyo mitihani ya necta?
Kumbuka siku za karibuni Ndalichako alizuia Shule binafsi(private schools) kuwafanyisha mitihani ya mchujo wanafunzi wanaokwenda kusoma private schools, sasa hiki kinachotaka kufanywa na necta(serikali) kina tofauti gani na kile kilichokua kikifanywa na Shule binafsi?

Na vipi kuhusu wataofeli huo mtihani watapelekwa wapi sasa?
Hii serikali ya kutafuta kiki sana hii
 
kwa hili sasa NAONA kachemka vibaya mno ....ninavyojua Mimi kwa wanafunzi wakitanzania baada ya kufanya mtihani huwa wanatupa daftar wanachoma ...wanasahau kabisaaa ...sasa Leo unawambia wajiandae na mtihani ..mmmmhhhh NAONA kama serikali kwa hili wanataka wapunguze WATU sekondari garama za kuchangia zinazidi kuongezeka hahahahahaha Elimu bureeee hatimaye mdogomdogo wameanza kunawa mikono ...nabado fom 4 na 6
 
Tumeamua kuwa Kama uchaguzi wa marekani, EC na majority votes. Mitihani miwili inayotolewa na chombo kilekule kwa watu walewale kwa lengo lilelile. Tuzihurumie basi hizo pesa za umma!!!

Kwanini basi wanapinga shule binafsi kuwa na mitihani ya mchujo?
 
Sasa mtoto kafanya mtihani wa kuchagua mpaka hesabu sasa uwo mtihani sijajua itatumika lugha gani maswali ni ya form one au primary kama ni ya primary hii ni kazi bure nakama niya form one uko ni kukomoana isije ikawa inatafutwa namna ya kupunguza wanafunzi koz pesa ya kuwasomesha bure hakuna waseme tu
 
Hii nchi ina mifumo ya ajabu saana viongozi wanakurupuka tu kwahyo mtihani wa darasa la saba hauna maana sasa na kwann wanafunzi waandike mitihani miwili ili kujiunga kidato cha kwanza hii haileti maana hata kidgo
 
Kuna haja gani ya kufanya mitihani mara mbili au ndio tuseme ule wa awali hauna maana yoyote maana huu ndio utaamua hatma yao kwa mujibu wao
 
SAFI SANA.TUNAJUA UDANGANYIFU UNAOFANYWA KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA.SAFI SANA WIZARA KWA UAMUZI HUU.
 
Mambo ya ajabu sana mtihan wa taifa walitunga wao na kusahihidha wao ina maana wao wenyewe wanamashaka na kile wanachokifanya.Kama mwanafunzi alipita kimagumashi mitihan wa kidato cha pili si upo utaamua
 
Back
Top Bottom