Wanafunzi Wafukuzwa shule kwa kuvaa "Yeboyebo"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,863
image.jpeg



Wanafunzi wapatao 21 wanaosoma Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu yeboyebo.

TUKUMBUKE; Hawakupenda kuzaliwa kwenye familia masikini, hawakuchagua baba wala mama masikini! Wengi wetu tumetoka huko huko. Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga na Ofisa Elimu wa Mkoa hebu watendeeni haki watoto hawa!

Source:mad:Julius Mtatiro Fb Account
 
Haa hawa walimu vipi? au ni hasira za kuzuiwa kwa michango mashuleni? Hawajui watu wamesoma pekuna sasa ni wakuu wa nchi? Waache dharau kazi yao ni kufundisha watotot na kuhakikisha wamefaulu, usafi ni sawa wafuatilie bali aina ya kiatu? kwa nchi hii kwa kipato cha wengi wetu? aaaa huu sasa ubishoo, au walimuona mtoto wa Mwigulu akitolewa shule sasa wanataka kukopi yale mavazi?
 
Huko mbona yeboyebo ndiyo viatu vyao,ukizikusanya zote unajaza semi za kutosha
 
wengine tulivaa tairi na kaptula iliyoacha sehemu mojaya kalio hewani na tukafaulu vizuri tu.
 
mbna wamezngua ao walim,,mi npo chuo ssaiv ila hali imekua mbaya natmba maclas na yeboyebo na pens kama kawa cha msng pindi zisogee
 
kuna shule wanafunzi walirudishwa nyumbani hivhivi kwa kuvaa yeboyebo lakin kesho yake wote walikuja na viatu. Baada ya kuchunguza ilionekana kuwa kuna baadhi ya wazazi huwanunulia watoto viatu vizuri tu lakini watoto huamua kuvaa yeboyebo ili kutunza viatu vyao visiishe mapema.

kwahyo sio wote kwamba hawana uwezo bali kuna wengne hufanya kwa makusudi..

my take:
walimu wajaribu kushirikisha wazazi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuwafukuza shule.
 
Kama shuleni wanapaswa kuwa na sare kwa nn wasivae.
Viatu ni miongoni mwa sare za shule so lazima wawe nazo
 
Kwa kweli hawajawatendea haki hao watoto hata kidogo.

Unamfukuza mtoto shule sababu ya Viatu?

Je wanazijua hali za Wazazi wa watoto?

Unafikiri watoto hao wamependa kwenda hivyo shuleni!

Kama si hali ndio iliosababisha!

Wahusika wakuu huko, wawasaidie hao watoto warudi shuleni
 
Walimu safari hiii ya magufuli wamejitoa ufahamu.nao ni jipu.no way out.ujinga huuu.
 
Walimu hawakutenda haki kabisa, baadhi ya Wazazi kipato chao kidogo haswa. Watu huko wanaishi maisha ya shida sana, kuna kipindi nilishawahi fika huko mwambao,kuna Tarafa ina itwa Wampembe, kipindi hicho usafiri ni shida,kulikuwa na Fuso ina safiri mara moja tu kwa wiki kwenda Namanyere-Nkasi, hakuna umeme wala mawasiliano ya simu,ni radio call tu, sijui kwa sasa.
 
tabia za wanafunzi ukanda wa pwani viatu wanavaa sherehe za idiiiii ukanda wa bara viatu wanavaa pasaka,ekaristi,kipaimara na krismas
 
Back
Top Bottom