Singida: Idadi ya wanafunzi wanaopata mimba katika shule za msingi na sekondari imepungua kwa asilimia 66.66

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,564
1576746482736.png
WANAFUNZI wanaopata mimba katika shule za msingi na sekondari Singida imepungua kwa asilimia 66.66 kutoka mimba 54 mwaka jana hadi mimba 18, Novemba 30 mwaka huu.

Ofisa Elimu Sekretarieti ya Mkoa wa Singida (REO), Nelasi Mulungu alieleza kuwa kati ya idadi hiyo, wasichana wa shule za sekondari ni 15, watatu waliobaki ni kutoka shule za msingi.

Akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Singida (RCC) mjini hapa juzi, Mulungu alisema wanafunzi waliopata mimba wamepungua kufuatia ushirikiano mzuri baina ya wazazi, jamii, walimu na wanafunzi.

“Natoa mwito kwa jamii kuendelea kushirikiana na serikali ili kutokomeza tatizo hilo. Naomba wasichana wanaosoma kujitambua na kujiona wana thamani kubwa kuchangia maarifa kwa maendeleo ya familia zao na taifa,” alisema.

Alitaka kila halmashauri ya wilaya kujenga hosteli za wasichana za kutosha ili kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa, maabara na nyumba za walimu ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu bora.

Kuhusu upungufu wa walimu, Mulungu alisema mahitaji bado makubwa na serikali itakabili changamoto kadri fedha zinavyopatikana ili kuhakikisha elimu nchini inakuwa bora zaidi.


Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom