Wanafunzi wa vyuo vikuu mkue jamani acheni utoto!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa vyuo vikuu mkue jamani acheni utoto!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pdidy, May 10, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  akuna serikali isiyo na matatizo na pengine kwa afrika mashariki tanzania inaongoza kila sekta
  kwa upande wa elimu bomu kubwa limeangukiwa wizara hii pale walipopewa bomu lililoishinda wizara ya miundo mbinu na saasa limeamia elimu

  Ok nije kwenye mada hapo juu..ndugu wapendwa ni kweli waweza kusema chuo kimevamiwa na watoto walio na umri mdogo sana ndio maana hata humu jf wanamizaha kupita uko nyuma

  embu jiulize wanataka nauli ipunguzwe iwe 250

  kule dom wanataka kila mwanafunzi awe na laptop

  wapi utapata hili ndugu zanguni kuweni makini na migomo ya kijinga muulizen zito awape njia za migomo kudai haki zenu mpaka
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kaka mie nakuunga mkono. mie siku ile nisikie eti wanafunzi wa UDOM wamegoma kisa laptop nilijiuliza sana na sikupata jibu aina ya wanavyuo tulio nao sasa ktk vyuo vyetu. Kitu kingine wamekuwa marimbukeni wa siasa na kuchotwa kiurahisi na wanasiasa bila kujijua kuwa wanatumika kama vile mtu anavyoitumia Jojo.Hali hii ya kutumiwa huwapelekea wao kujisahau malengo yao ya kuwepo chuoni na kusahau umuhimu wao na elimu yao ktk familia zao.
   
 3. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nakuunga mkono kaka, lakini cha kuzingatia hapa ni kwamba wanafunzi watendewew haki pale wanapostahili, mfano wanafunzi wa Udom college ya Informatics katika kipindi cha nyuma waliahidiwa kwamba lazima watapewa hicho walichokuwa wanakumbushia/wanadai, na aliyewaahidi ni kiongozi mkubwa sana serikalini. sasa kila mara awlikuwa wakikumbushia wanapigwa danadana. hakuna majibu ya moja kwa moja ya kuridhisha, na kwa kweli migomo mingi ya hapa Udom inasababishwa na baadhi ya watu wa Utawala. Baadhi yao wana majibu ya kejeli, jeuri, kebehi, hii ndo source ya migomo hapa chuoni. taarifa hazitoki katika muda muafaka, ktu ambacho kinaleta ukengeushi mkubwa sana hapa chuon. Wanafunzi wa Informatics kama wangepewa taarifa za mara kwa mara juu ya ahadi wallioahidiwa sidhani kama leo wangekuwa wapo hapo walipo leo. Cha msingi kila mtu awajibike vyema katika nafasi yake na wanafunzi sometimes wawe na subra na wawatumie zaid viongoz wao na hawa viongozi kwa kweli wajirekebishe katka suala ya uwajibikaji kwa sababu Serikal ya Wanafunzi imelala mno. Amkeni sasa kumekucha mtimize ahadi zenu....
   
 4. LWAKAPISI

  LWAKAPISI Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pdiddy,mbona hueleweki na huna uhakika na usemacho ndio maana suala la UDOM unasema eti ulisikia!!!hakuna mwanachuo anayeingia barabarani bila sababu,UDOM waligomea special faculty requirements ambazo wanadhurumiwa/hawapewi kabisa na wakipewa hizo hela wananunua laptops ambazo kwa masomo yao lazima uwe nayo.Ila uongozi kama kujivua gamba wanasema eti waligomea laptops
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  usilaumu sana nahisi alioandika hii thread kasoma coarse ambazo special faculty req haina umuhimu so muambie afufuke sababu tayari ashakufa..
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wewe mtoa mada kama umesoma ungwini bora ukae kimya......je, utasoma programming bila computer?? Kwa nchi kama India chuo kina dhamini wanafunzi mikopo ya laptops kupitia mabenki na wanafunzi wanalipa kidogo kidogo mpaka wana maliza masomo.

  Tatizo la wazee wa Tanzania wana endekeza siasa na wanafikiri hata nchi zingine zimeendelea kwa kupiga porojo. Lakini ukweli ni kwamba hilo halipo. Nawashauri viongozi wa Tanzania kwamba wasipo jali sayansi wenyewe wasifikiri kuna nchi kutoka ng'ambo itakuja kutufundishia vijana wetu bure mpaka waweze ku-design vifaa vya kisayansi.
   
 7. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ccm iliwaahidi
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Huu ni utoto kwakweli. Hivi nani kakwambia laptop na faculty requirement? Laptop ni basic needs kwa kila mwanafunzi haijalishi anasoma nini. Unless muombe kuwekewa maabara maalum kwa ajili ya computer. Yaani utakuwa upuuzi wa hali ya juu kama chuo kitaanza kutoa laptop kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Ni mzigo usiobebeka. Nanyi wanafunzi hebu fungueni akilini zetu, jitahidi kufikiria zaidi ya utegemezi.
   
 9. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kuna sehemu wanafunzi wanakosea. lakini makosa makuu ni selikali na utawala kutofanya wajibu wao kwa wakati!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hata sisi tulisoma vilevile na tukasoma hizo programming lakini hatukununua wala kumdai mtu laptop. Tuliendaga Kariakoo kule tukanunua PC used tukaipiga mtungo na TUKAFAULU VILEVILE..wanafunzi wa siku wana mizaha sana aisee..lol
   
 11. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Huo utakuwa ukomunist. Someni vijana acheni hizo utopia za ccm
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Watu mnasahau haraka sana!

  Wakati wa Kampeni Mzee wa Msoga kule Bagamoyo aliahidi laputop kwa kila mwalimu na wanafunzi

  Tanzania daima
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mimi kama mdau wa maendeleo, elimu na mlipa kodi siwezi ku-endorse mwanafunzi anayedai apewe laptop. This is outrageous. Ni kweli tunahitaji wasomi wengi zaidi kama taifa, lakini with this kind of wasomi NO PLEASE. Bora waendelee kufeli tu huko shule za kata. This kind of wasomi hawatalisaidia taifa bali ni mzigo wa kuni.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hili linaweza kuonekana la kitoto lakini kwa karne ya leo ni la muhimu sana.

  Ni wajibu wa serikali kuchukua changamoto hii positively na kujaribu kuitafutia ufumbuzi. Kwa mfano, naamini kama serikali inaweza ikaingia mikataba hata na watengenezaji wa hizi laptops na zikawafikia wanafunzi hapa kwa bei nafuu kabisa! Hivi hata kwa bei za sasa za sokoni ya laptops za kawaida kabisa yale mabilioni wanayotaka kuwalipa dowans yangeweza kununua laptops ngapi? Tuliambiwa wanataka kulipa 94 billions ($ 65.8million), so kwa bei ya shillingi milioni 1.2 kwa laptop (mimi naamini kwa kuingia mkataba na manufacturer, unaweza kupata laptop nzuri tu kwa shilingi kati ya laki 6 mpaka 8!), unaweza kuwapa laptops wanafunzi zaidi ya elfu 78! Wanafunzi wa vyuo vikuu (undergraduate) wapo wangapi kwa sasa? Na kama haiwezi kuwapa bure (kama faculty requirement), si inaweza kuwakopesha tu kwa bei ya chini (subsidised)!

  Wenzetu Rwanda wanazungumzia kuwa na laptop kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi, sisi hapa tunaona ni utoto kwa mwanafunzi wa chuo kikuu kudai laptop (shame on us!). Juzi niliona tangazo (nadhani ni la Haki Elimu) likimwonesha mwalimu anajaribu kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi sehemu mbalimbali za komputa na jinsi ya kuwasha na kuzima bila kuwapo kwa komputa...yaani ni vichekesho tu...hata mwalimu mwenyewe anaonekana hiyo komputa anayojaribu kufundisha haijui sawasawa!


   
 15. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Abdulhalim naona umeanza kuongea kwa hisia...nimependa ulivyo jitambulisha kuwa wewe ni mdau wa maendeleo. Lakini usije kusahau kuwa hayo maendeleo hayafikiwi bila kuwa na elimu bora...unajua kwa haraka haraka mtu akisia kuwa eti wanadai laptop wale wasio jua vizur umuhimu wa kompyuta huona kuwa ni anasa. Lakini napenda nikuhakikishie kuwa kwa ulimwengu wa sasa kompyuta ni kifaa muhmu sana cha kazi....nashangaa kuona unatereza na kutaka kutoka nje ya hicho ulichodai kuwa wewe ni mdau wa maendeleo kwa kuta
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wazee wao wananyanyasika vijijini waowanadai laptop!!Ndizo zinazofundisha?
   
 17. p

  papachu Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua nimesoma ulichoandika ni mawazo na mtazamo wako siwezi kukupinga lakini kumbuka kunanchi kama rwanda wanakauli mbiu ya one student one laptop na imewezekana,pili swala la mgomo la wanafunzi wa informatics nimelifuatialia kwa karibu sana mbali na laptop kama uongozi wa chuo unavyodai pia hapo informatics hawana walimu wa kufundisha bahazi ya kozi inapelekea kozi ya semista nzima kufundishwa wiki moja,naomba TCU ifuatatilie kwa kwa karibu iwezekani kila mwaka wanafunzi wasio pungua 70 wanafeli na kuacha masomo je tujiulize mbona vyuo,vingine akuna kitu kama hicho
   
 18. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  unaweza kutusaidia malengo ya kuwepo vyuoni?
   
 19. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  SMU idea yako ni nzuri lakini si endelevu. Hawa wanafunzi wanaingia chuo kila mwaka. Kwahiyo serikali kila mwaka iwe inanunua laptops? Mie nadhani wao kama hawana vitu vya kufundishiwa kama Maabara ingekuwa rahisi kuelewa tatizo ni nini. Hivi kweli katika elimu yetu priority inaweza kuwa laptop kwa wanafunzi wa Informatics? Umuhimu wa ICT unafahamika tena kwa kila mtu, kununua computer ni moja ila cha msingi professional yoyote inahitaji jitihada binafsi kujiendeleza. Vinginevyo, wanaosoma kilimo watadai matrekta muda si mrefu na wale wa mifigo sijui watadai nini au wanapewa nini. Tujifunze kujitafutia uwezo na si kuwa tegemezi.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Why laptops? Kwanini msidai maabara ya computer au library yenye computer za kueleweka na za kutosha? Computer si anasa ni basics na kila mwanafunzi anastahili computer lakini hoja ya serikali igawe computer kwa kila mwanafunzi haina mashiko. Hata huo mpango wa serikali naamini utakuwa endelevu kama tu shule zitapewa maabara za computer na si kugawa computer.
   
Loading...