Taarifa kwa umma wa watanzania juu ya serikali kuwatelekeza wanafunzi wa vyuo vikuu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334

1.0. UTANGULIZI
Mfumo mzima wa elimu hapa Tanzania bado ni changamoto kubwa sana ya kufikia malengo ya kitaaaluma na maendeleo ya kujitegemea kielimu. Mfumo wa elimu ya Tanzania umejikita zaidi kuwafanya wanafunzi wakimaliza chuo waajiriwe na si kuwapa mbinu za kuwafanya hata kama watakosa ajira wanaweza kuwa wabunifu wa kubuni vitu vitakavyo wafanya wajikwamue kimaisha. Pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali lakini vyuoni kunamatatizo makubwa sana ambayo wanavyuo unapoongea nao unapata huruma sana nahii ni kutokana na Serikali kuwa mbali na matatizo ya wanavyuo, kwani shida kubwa zinazopatikana vyuoni si vyuo bali ni wanavyuo wenyewe. Chama cha NCCR-mageuzi kupitia Kitengo cha vijana wa NCCR-mageuzi takribani siku 20 sasa kimefanya mahojiano na majadiliano na wanafunzi mbalimbali juu ya matatizo yanayowakabili vyuoni na namna ya kuyatatua.

CHANGAMOTO VYUONI KWA WANAFUNZI.
Kuna changamoto nyingi sana ila tunalenga zile ambazo ndio zinazua mitafaruku vyuoni;

2.1.MIKOPO
Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi hutoa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juuTanzania, moja ya fedha ambazo hutolewa na bodi hii ni fedha za kujikimu, malazi, utafiti,ada kwa asilimia n.k, kutokana na uwepo wa Bodi hii ya mikopo inaonekana kuna ukritimba ndani ya Bodi na kuna siri kubwa nyuma ya pazia ambayo tutaifichua siku si ndefu. Wanachuo wengi ni watoto wa wananchi wa kawaida sana na hutegemea fedha kutoka bodi ya mikopo ili waweze kuishi na pia wengine kupitia hiyohiyo fedha ya kujikimu huitumia kumalizia kulipia ada vyuoni kulingana na asilimia au kiwango anachopewa na bodi ya mikopo. Fedha hizi zimekuwa zikichelewa sana kuwafikia wanavyuo husika kwa mda muafaka na hata sababu zinazotolewa na viongozi wahusika hazina tija kwa maendeleo ya taaluma nchini maana huwezi ukaweka programu ambayo haitekelezeki kikamilifu na kujikuta wanavyuo wanaingia kwenye migomo kudai haki zao.

2.2. WANAOSABABISHA KUTESEKA KWA WANAVYUO NI;
2.2.1. BODI YA MIKOPO, bodi haina ukweli halisi katika kusaidia matatizo ya wanachuo na wamekuwa wakiwapiga chenga wanavyuo, wanavyuo wamekuwa wakiambiwa kama unaoona mkopo haujapata nenda bodi na wakienda bodi wanarudishwa vyuoni bila kujua mstakabali wao zaidi ya kuchezewa danadana. Wanapofanya migomo juu ya swala hili wanafukuzwa vyuo.

2.2.2. UONGOZI WA VYUO(UTAWALA), kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana baina ya utawala wa chuo na wanavyuo juu ya fedha kutoka bodi kwani utawala wao hawajui kuhusu bodi wanachotaka ni fedha yao ulipe kama unadaiwa. Utawala wa vyuo unalikimbia hili swala la mikopo ili kuepuka migogoro na wanavyuo. Kimsingi vyuo bado vinanafasi ya kuwasaidia wanafunzi wao ili kuwarahisishia kufanya vizuri katika masomo yao.

2.2.3. SERIKALI ZA WANAVYUO, hizi nazo zimeshindwa kazi viongozi waliowekwa wanafisadi pesa za michango ya wanachuo kwani moja ya kazi yao ni kushughulikia matatizo ya wanachuo wenzao hasa hili la bodi ya mikopo na STUDENT UNION ndio nauli zao na posho zao katika kushughulikia matatizo ya wanachuo lakini hakuna jipya bali serikali za wanachuo zimegeuka ndio chanzo cha kusababisha wanavyuo kufukuzwa.

2.2.4. LOANS OFFICERS, hawa ni waajiriwa vyuoni wanashughulika na maswala ya mikopo ya wanachuo lakini wamekuwa na majibu makali kwa wanavyuo wanapodai haki zao na hakuna zaidi na wengine wanashutumiwa kuomba rushwa ili kuwahisha mikopo.

2.2.5. MAWAZIRI WA MIKOPO VYUONI, hawana majibu sahihi kwa kuchelewa kwa mikopo kila wanapotoa majibu yao ndio kwanza wanaweka siasa katika maisha ya wanavyuo huku wao wakipata posho za safari.

2.3. MATATIZO YOTE YANAZALIWA NA BODI YA MIKOPO;
2.3.1. Wanfunzi kuandamana mara nyingi chanzo kikubwa ni fedha kuchelewa.
2.3.2. Wanafunzi kulawitiwa, kuibiwa na kuuza vifaa vyao.
2.3.3. Mgogoro wa wanavyuo na maeneo yanayowazunguka
2.3.4. Wanafunzi kuhisiwa kufanya biashara ya kujiuza.
2.3.5.Wanavyuo kuacha vyuo
2.3.6. Wanachuo kutofanya mitihani yao ya mwisho.
2.37. Wanavyuo kudaiwa walivyokopa kwa kusubiri boom.

2.4.SULUHISHO.
Serikali haihitaji kuunda Tume wala kamati katika kukagua uozo uliopo vyuoni, Bodi ya mikopo na wizara ya Elimu kabla hawajafanya selection huwa wameshafanya majumuisho ya idadi ya wanafunzi watakaopewa mikopo na bajeti yake kupitia wizara ya elimu hupitishwa bungeni, sasa ni wapi na wapi tangu bajeti ipitishwe bungeni lakini wanavyuo wanalia na bodi ya mikopo. Serikali inatakiwa kutambua bodi ya mikopo ni bomu kubwa na siku likilipuka watakimbiana. Tunaiomba serikali ione uchungu kwa Vijana wenzetu walioko masomoni lasivyo watasababisha migomo kuwa mingi kama wataendelea kufumbia macho. Mwisho wa kuwahadaa wanachuo umefika mwisho. Tunaipa muda Wizara ya elimu na bodi yake ya mikopo kushughulikia fedha za wanachuo kwani ziko kwenye bajeti yao na wanapaswa kutekeleza mapema kabla hatujasema ukweli ulio jificha nyuma ya pazia la bodi ya mikopo.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-MAGEUZI.
11/2/2013



 
haaaaa Kisandu huyuhuyu kapata cheo tayari!!!! hiz ndizo siasa,taarifa noted.
 
Jamaa anatafuta Huruma ya Wanavyuo, Mkuu wanavyuo si wajinga kama unavyo fikilia wewe, na huwezi kuwa na msaada wa aina yoyote ile katika matatizo ya mikopo, wewe katika Nchi hii si chochote wala lolote, kama ndo unazani ndo njia za kupata popula imekula kwako mkuu,
 
hivi ni kwanini we jamaa huwa hujipangi as if umekurupushwa ghafla kutoa matamko?
 
Mzee naona upo moto!!! Jana ulikuja na ID nyingine ukisema wenje kawasahau SAUT leo Serikali. Tuliaga basi kabla ya kuanzisha mchakato kaka sasa hapo sijui umesimia upande gani wa kupeleka shutuma. Pili hayo matatizo ni yaleyale ambayo hayahitaji hata maelezo na chanzo tunakijua.
Tulia kijana fikiria kwa makini kabla ya kutenda sio kukurupuka unajishushia heshima. Hayo ni mawazo yangu tu.
 
Huyu jamaa wakina Mkosa mali ndo wanao mpa huu ushauri kuku, na anataka kulalia mlango wazo Bahati za wenzake
 
nadharia... nadharia... nadharia
keyboarder... keyboarder... keyboarder

please something we dont know,
 
Deo my brother, wanafunzi wanaumia kweli, in real life.

Wewe una-sympathis nao kweli behind the monitor blaming on a keyboard.

Kaka fanya kitu physical tuone, wacha hizi pang'ang'a humu JF ukidhani watakusamehe wanaJF.

Enda physicaly, enda Ofisi za Bodi, Enda kwa Waziri, Andamana, Shinikiza na unachokitaka utakipata chaaaap.....
 
Kisandu 0yeeeeeee! ujue nilivyoona taarifa yako ni9kaanza kukumbuka kama nilishakuona mahali lakini wapi nikawa sikumbuki.sasa nakumbuka sasa!
 
Sasa hivi tuko bize tufuatilia juu ya nani mwenye haki ya kuchinja wanyama. Na mauaji ya wenzetu huko buseresere. Hayo mambo yako ya cheap popularity, ungesubiri kwanza.
 
Umeanza tena Mwishowe utasema Uchafu ulioko NCCR Mbatia atakutimua Muda sio Mrefu.Mwongo ni Mwongo tu sisi hapa tulishakutupia laana.
 
..... na huwezi kuwa na msaada wa aina yoyote ile katika matatizo ya mikopo, wewe katika Nchi hii si chochote wala lolote, ........,

Mimi nadhani kama wewe una hakika huna msaada kwa watanzania wenzako, inakubidi uwaache wenye uhakika kuwa wanao msaada kwa watanzania wenzao wawasaidie kwa namna wanayoweza. Lakini kama una hakika una msaada kwa watanzania wenzako basi wasaide kuliko kukatisha wengine taama.

Vinginevyo nitaamini kuwa wewe si mtanzania ila ni SATAN wa ukweli.
 
Labda nimekurupuka lakini mara nyingi fedha zinacheleshwa na serikali kwenda bodi ya mikopo,kama kisandu hukugusia hili basi hujui unalosema!!!
 
ukweli board ya mkopo ni kichaka cha majambazi hawana hata utu hata chembe mimi nafikria hata hela hawana
 
Back
Top Bottom