Wanafunzi wa Sheria UDOM wanufaika na wiki ya usuluhishi

Wanafunzi wa Sheria UDOM wanufaika na wiki ya usuluhishi

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
Viongozi mbalimbali kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria, leo tarehe 16 Aprili 2026 wamefanya majadiliano ya pamoja na wanafunzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Majadiliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa CT1 uliopo Ndaki ya Biashara na Uchumi (CoBE), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Usuluhishi nchini.

7544f49b-86d5-4e4d-8acf-759c56549278.jpeg


Lengo kuu la majadiliano hayo lilikuwa ni kujadili umuhimu wa usuluhishi pamoja na namna ya kutatua migogoro kwa njia mbadala (Alternative Dispute Resolution – ADR), ambayo imeendelea kuwa nyenzo muhimu katika mfumo wa utoaji haki.

Akizungumza kwa niaba ya Amidi wa Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Gamba aliishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kuihusisha UDOM katika maadhimisho hayo na kuichagua kuwa moja ya vituo vya utekelezaji wa programu na shughuli mbalimbali za Wiki ya Usuluhishi kitaifa.

8a00fc03-e65b-4e57-a1cc-176bc547002b.jpeg


“Baadhi ya wanafunzi wetu wanasoma masomo yanayohusiana na usuluhishi, na tunatambua nafasi yake muhimu katika kutatua migogoro mbalimbali ndani ya jamii,” alisema Dkt. Gamba.

Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, ambaye pia ni Mratibu wa Wiki ya Usuluhishi, Mheshimiwa Dkt. Fatma Khalfan, alikipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mchango wake katika kuzalisha wataalamu mahiri wa sheria. Aidha, alisisitiza umuhimu wa chuo hicho katika kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii kupitia Kliniki ya Msaada wa Kisheria iliyopo chuoni hapo.

76795e0f-978b-4c42-88da-c34cc5ebc2aa.jpeg


Katika majadiliano hayo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu dhana ya usuluhishi, taratibu za usuluhishi, sifa za msuluhishi bora, maeneo yanayotolewa huduma za usuluhishi, pamoja na majukumu na nafasi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika kulinda haki za makundi maalum katika jamii.

a78b21db-ac20-406c-a52d-b8a9e93f059a.jpeg
 
Back
Top Bottom