Wanafunzi wa Sekondari kuchujwa kwa mtihani kabla ya kupanda kidato

Hahahaaa! Mbona hajasema kwa shule za kata!! Maana anajua itafikia darasa moja lina wanafunzi karibia wa shule nzima maana watakaosonga hawazidi 10.
 
Waziri wa mpya wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameagiza Wanafunzi wa shule za Serikali kufanya mitihani ya mchujo kabla ya kupandishwa vidato.

===========

jafo+pic.jpg


Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo ameagiza wanafunzi wa shule za Serikali kufanya mtihani wa mchujo kabla ya kupandishwa vidato.

Pia, amesema hatapanga ada elekezi kwa shule binafsi bali watapunguza wenyewe.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatano mjini Dodoma alipozungumza na wafanyakazi wa Tamisemi.

Ametoa kauli hiyo akisema shule kongwe za Serikali zimekuwa ‘zikikimbizwa’ na za binafsi.

"Naagiza kuanzia leo, lazima wanafunzi wa shule za Serikali wafanye mitihani mara mbili, mwezi wa sita na mwisho wa mwaka ili kuwachuja wa shule zenye vipaji maalumu na kuwarudisha shule za kawaida za Serikali, vinginevyo ndiyo maana tunafanya vibaya wakati wote," amesema.

Amesema katika mchujo huo, wanafunzi watatolewa kutoka shule kongwe na kupelekwa za vipaji maalumu na vivyo hivyo kutoka vipaji maalumu kwenda shule kongwe.

Kuhusu ada kwa shule binafsi amesema si jukumu la Serikali bali wanataka kuboresha shule zake ili watu na taasisi binafsi zikose wanafunzi.

"Mheshimiwa Kakunda (Joseph –Naibu Waziri Tamisemi) nakuagiza kuanzia leo maana wewe ndiyo nimekukabidhi jukumu la elimu, nataka mtihani wa 2019 shule za vipaji zote 22 ziongoze mtihani wa Taifa na shule binafsi ziwe nyuma, lakini tuongoze kwa halali si ubabaishaji hapo ndipo shule binafsi za makanjanja zitajifuta zenyewe," aliagiza Jafo.

Wakati huohuo, Jafo amewaagiza watendaji katika idara ya elimu kushughulika na wakuu wa shule kongwe zote ili kuona kama bado wana sifa za kuendelea kuwa wakuu wa shule au kuwaondoa wanaoonekana kushindwa kazi.

Kuhusu watendaji wa Tamisemi amesema hataki mambo matatu wizarani hapo ambayo ni ulegevu, mazoea na kutojali muda ambayo amesema ni adui wa mafanikio.

Naibu waziri, Kakunda amesema hana shaka na kazi aliyopewa akiahidi kuifanya kwa kutumia weledi na uzoefu wake ili kuibadilisha Tamisemi.

Kakunda ambaye kabla ya kuwa mbunge alikuwa mkurugenzi Wizara ya Maji amesema mipango mingi anaijua lakini akaomba ushirikiano kwa watumishi.


Chanzo: Mwananchi
b299dfb99b6b1fdd885317221d60085f.jpg
 
Na kwa kuwa mmekataa kutupandishia mishahara sasa subirini muone Kama kuna atakayepanda kidato
 
Serekari yetu ijipange ije na hoja moja wanakinzana sana juu ya uchujaji wa wanafunzi mkuu wa nchi alisema tabia ya shule binafsi kuchuja watoto marufuku kwakuwa ilikuwa kawaida kwao sasa huyu amekuja na hili kuwa anatengua kauli ya boss wake au ndio hawajui kujipanga watusaidie tujue kipi tunafanya
 
Maslahi ya walimu kwanza wasijifanye kusahau

Ngoja kwanza hivi Jafo ni waziri wa elimu?
 
agizo zuri, ila hiyo load ya wanafunzi kurudia vidato itawashinda
 
kwenye mchujo hata mimi nawapa hongera haiwezekani mtu anafeli afu anaendelea na shule
 
Well kama lengo ni kuongeza ubora au kiwango cha elimu, michujo hiyo ni sawa na kuamua kumpima uzito ng'ombe mara kwa mara ukitarajia kufanya hivyo kutaongeza uzito wake, badala ya kumpa malisho bora na matunzo mazuri. Ndivyo elimu yetu ilivyo sasa: obsessed with exams rather than the quality of the education.
 
Mimi nijuavyo kila private ina mitihani yao ya mtoto asipofika wastani wautakao anarudia darasa labda shule za kata maana hata baadhi ya shule za jeshi pia zinautaratibu huo sasa xjui wanazunguzia mitihani ya kutunga wao labda
 
Anaingilia kazi za waziri wa elimu! Waziri wa elimu ndio mwenye dhamana ya kuweka Sera na miongozo ya elimu nchini. Kazi ya waziri wa Tamisemi ni kutekeleza na kusimamia Sera na miongozo kama zilivyotolewa na wizara husika kama vile elimu, afya, kilimo nk. Vinginevyo tutakuwa tumepata Mrema mwingine!
 
Ukifuatilia hoja yangu hapa utajifunza kitu Najiuliza tangu Prof.Ndalichako ateuliwe kuwa waziri wa elimu ni kitu gani amekifanya chenye kuboresha elimu kimsingi hatuna dira ya elimu. Haya yote ni kukosa dira kuhusu elimu. Anaongelea shule maalum, hebu jiulizeni hizo shule maalum zinalenga kufanya nini? wanaomaliza shule maalum wanaenda vyuo maalum au wanaishia wapi? hakuna maana yakuwa na shule maalum if wahitimu wa shule maalum hawana muendelezo....
Pili, Ubora wa elimu haupimwi kwenye kufaulu tu. Nini hasa dhamira ya elimu? kama mwanafunzi anapata first class lakini hawezi kuishi maisha yake kisomi jua ni utapeli tu. Elimu itoe ujuzi na knowledge ya kukabiliana na hali ya maisha na mazingira ya mwanadamu regardless kapata one au two au zero. ukitunga mtihani rahisi wote watafaulu na utasifiwa kufaulisha lakini je umeboresha elimu?

something wrong is still in our minds, lazima tuzinduke
 
Back
Top Bottom