Wanafunzi wa Sekondari kuchujwa kwa mtihani kabla ya kupanda kidato

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Waziri wa mpya wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameagiza Wanafunzi wa shule za Serikali kufanya mitihani ya mchujo kabla ya kupandishwa vidato.

===========

jafo+pic.jpg

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo ameagiza wanafunzi wa shule za Serikali kufanya mtihani wa mchujo kabla ya kupandishwa vidato.

Pia, amesema hatapanga ada elekezi kwa shule binafsi bali watapunguza wenyewe.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatano mjini Dodoma alipozungumza na wafanyakazi wa Tamisemi.

Ametoa kauli hiyo akisema shule kongwe za Serikali zimekuwa ‘zikikimbizwa’ na za binafsi.

"Naagiza kuanzia leo, lazima wanafunzi wa shule za Serikali wafanye mitihani mara mbili, mwezi wa sita na mwisho wa mwaka ili kuwachuja wa shule zenye vipaji maalumu na kuwarudisha shule za kawaida za Serikali, vinginevyo ndiyo maana tunafanya vibaya wakati wote," amesema.

Amesema katika mchujo huo, wanafunzi watatolewa kutoka shule kongwe na kupelekwa za vipaji maalumu na vivyo hivyo kutoka vipaji maalumu kwenda shule kongwe.

Kuhusu ada kwa shule binafsi amesema si jukumu la Serikali bali wanataka kuboresha shule zake ili watu na taasisi binafsi zikose wanafunzi.

"Mheshimiwa Kakunda (Joseph –Naibu Waziri Tamisemi) nakuagiza kuanzia leo maana wewe ndiyo nimekukabidhi jukumu la elimu, nataka mtihani wa 2019 shule za vipaji zote 22 ziongoze mtihani wa Taifa na shule binafsi ziwe nyuma, lakini tuongoze kwa halali si ubabaishaji hapo ndipo shule binafsi za makanjanja zitajifuta zenyewe," aliagiza Jafo.

Wakati huohuo, Jafo amewaagiza watendaji katika idara ya elimu kushughulika na wakuu wa shule kongwe zote ili kuona kama bado wana sifa za kuendelea kuwa wakuu wa shule au kuwaondoa wanaoonekana kushindwa kazi.

Kuhusu watendaji wa Tamisemi amesema hataki mambo matatu wizarani hapo ambayo ni ulegevu, mazoea na kutojali muda ambayo amesema ni adui wa mafanikio.

Naibu waziri, Kakunda amesema hana shaka na kazi aliyopewa akiahidi kuifanya kwa kutumia weledi na uzoefu wake ili kuibadilisha Tamisemi.

Kakunda ambaye kabla ya kuwa mbunge alikuwa mkurugenzi Wizara ya Maji amesema mipango mingi anaijua lakini akaomba ushirikiano kwa watumishi.

Chanzo: Mwananchi
 
October 11, 2017 patrick

Jafo-Bungeni.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo ameagiza wanafunzi wa shule za Serikali kufanya mtihani wa mchujo kabla ya kupandishwa vidato.

Pia, amesema hatapanga ada elekezi kwa shule binafsi bali watapunguza wenyewe.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatano mjini Dodoma alipozungumza na wafanyakazi wa Tamisemi.

Ametoa kauli hiyo akisema shule kongwe za Serikali zimekuwa ‘zikikimbizwa’ na za binafsi.

“Naagiza kuanzia leo, lazima wanafunzi wa shule za Serikali wafanye mitihani mara mbili, mwezi wa sita na mwisho wa mwaka ili kuwachuja wa shule zenye vipaji maalumu na kuwarudisha shule za kawaida za Serikali, vinginevyo ndiyo maana tunafanya vibaya wakati wote,” amesema.

Amesema katika mchujo huo, wanafunzi watatolewa kutoka shule kongwe na kupelekwa za vipaji maalumu na vivyo hivyo kutoka vipaji maalumu kwenda shule kongwe.

Kuhusu ada kwa shule binafsi amesema si jukumu la Serikali bali wanataka kuboresha shule zake ili watu na taasisi binafsi zikose wanafunzi.

“Mheshimiwa Kakunda (Joseph –Naibu Waziri Tamisemi) nakuagiza kuanzia leo maana wewe ndiyo nimekukabidhi jukumu la elimu, nataka mtihani wa 2019 shule za vipaji zote 22 ziongoze mtihani wa Taifa na shule binafsi ziwe nyuma, lakini tuongoze kwa halali si ubabaishaji hapo ndipo shule binafsi za makanjanja zitajifuta zenyewe,” aliagiza Jafo.

Wakati huohuo, Jafo amewaagiza watendaji katika idara ya elimu kushughulika na wakuu wa shule kongwe zote ili kuona kama bado wana sifa za kuendelea kuwa wakuu wa shule au kuwaondoa wanaoonekana kushindwa kazi.

Kuhusu watendaji wa Tamisemi amesema hataki mambo matatu wizarani hapo ambayo ni ulegevu, mazoea na kutojali muda ambayo amesema ni adui wa mafanikio.

Naibu waziri, Kakunda amesema hana shaka na kazi aliyopewa akiahidi kuifanya kwa kutumia weledi na uzoefu wake ili kuibadilisha Tamisemi.

Kakunda ambaye kabla ya kuwa mbunge alikuwa mkurugenzi Wizara ya Maji amesema mipango mingi anaijua lakini akaomba ushirikiano kwa watumishi.
 
Mkakati wowote ambao unaweza kupata angalau nafasi ya kufanikiwa, lazima uanze na walimu. maslahi yao, makazi yao, mafao yao. hilo la kwanza. vyoo bora, madawati na vyumba vya madarasa vifuatie, maktaba na maabara pia. lakini kwanza mwalimu. maana hata chini ya mti, mwalimu aliyehamasika atapiga kazi na atafanikisha kwa kiwango kikubwa tu. lakini hata uweke kila mwanafunzi awe na laptop, kama mwalimu hana morali ni kazi bure tu. Ni "kujilisha upepo". hayo maagizo hayana maana yoyote. Ni UMAGUFULI na UMAKONDA katika ubora wake.
 
Haya maagizo ni ya hovyo tuu kama wamepigila msumali kutoongeza mishahara kwanza....
 
Kwahiyo mwanafunzi wa shule ya kata mchujo haumuhusu na shule za kata ni jarala lakupokea makapi?
 
Kisarawe wana operation ondoa zero
Nashangaa wanaoganaizesheni wote hawajui operation tokomeza zero ni scientific approach wao wanajua kuweka watoto kambini kama JKT

Mawazo ya viongozi wetu yamekua kama fly lifecycle
 
Walimu wapunguziwe mshahara kwanza ili wapate akili ndio wataweza kufundisha vizuri maana sasahivi hawajielewi.

Wanapokea mshahara mkubwa halafu hawafanyi kazi kwa bidii.
 
Aanze na kuchagua watoto wenye ufaulu mzuri wa darasa LA saba kuliko kuchagua wote.
Pia amshawishi waziri wa ELIMU kufuta mitihani ya majibuvya kuchagua A,b,c,d ktk mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi.
Hapo nitawaona wako serious.
 
Kama sio ameboresha maslai ya mwalimu kwanza, huo ni ubatili.

Hivi mwalimu anakwenda mwaka wa sita hamna daraja, elimu hata masters ya elimu mwalimu aliejiendeleza kwa hela yake anaambiwa anajifurahisha, huko elimu hata weredi hauzingatiwi yaani unakuta walimu wana degree, masters na wengine ni PhD candidate still wanaongozwa na head ana diploma kwa kisingiizo cha uzoefu.

Huku primary ndio utachoka Mratibu cheti kabisa wakati shule zina walimu wana degree masters na kadharika wanapigishwa jalamba na grade IIIA kitu ambacho kinafanyika hata katika ngazi za shule hili sio sawa

Pia inshu ya posho. Kwa nini walimu hawapewi posho wakati wafanyakazi wengine wanapewa?
Zinaanzishwaga kwa mikwala mara wanaoishi kwenye mazingira magumu mara blaaaa blaaa blaaaa zinayeyuka.

Mwisho, hakikisheni kila mwalimu wa nchi hii yupo kwenye daraja husika kwa mujibu elimu yake, uzoefu wake kazini na juhudi yake k atikakukej. Kuna watu wapi na daraja moja miaka 10 na sio kuwa katikia ukomo wa kupanda daraja au nini ni figisu za kawaida za kindezi ndezi tu.

Tupeni heshima tunayostaili na sisi tutaoa tija inayostaili na sio kuonana nakuja na kukejeliana kunakopelekea haya matokeo mnayoyaona.

Ndalichako angeweza kulifanyia hata mojawapo ya hayo niliyoyasema labda elimu inaweza kupata positive compared to what these buddies currently practicing
 
Safi sana. Ila usisahau kufaulu kwa mwanafunzi ni factors Nyingi ikiwemo vifaa na waalimu. Upande huko umejipangaje Mh. Waziri?
 
Walimu mambo yao safi kabisa,yaboreshwe mambo mengine kwanza.
Safi sana. Ila usisahau kufaulu kwa mwanafunzi ni factors Nyingi ikiwemo vifaa na waalimu. Upande huko umejipangaje Mh. Waziri?
 
Back
Top Bottom