Wanafunzi wa kike Saluni,UHUNI MTUPU!

hivi bado vitoto sana na ni chini ya miaka 20 ..nadhani umri unawaruhusu kufanya haya...
nakumbuka enzi zangu niko pale Tboys nlikuaga naibuka disco vumbi night ni noma kila siku...
na ukikutana na mimi utaeza kufikiri nsapoteza mwelekeo ila mwisho wa siku nkatoka na DVSION ONE Huyoo nkasepa mlimani..
lo tukikutana huezi amini..ni umri tuu huwa unapita

hata kama wewe pia ulifanya,haikuwa sahihi! Wengi wanaofanya hivyo wanaishilia pabaya.
 
Hongera sana Kasim Kasian! Hiyo ndio maana halisi ya taaluma ya Ualimu. Ualimu si kuwamezesha wanafunzi theory kisha wanafeli, bila kujua kwa nini? Kufanya hivyo ndiko kunakowatofautisha Waalimu na form Six leaver au wale wanaodandia fani au kufundisha uchochoroni. Tunapaswa kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi inayofaa. Kama kila Mwalimu akifanya kama wewe thamani ya Mwalimu itarudi. USIOGOPE!! UTAPATA FADHILA NYINGI, ACHANA NA WATU WANAKUVUNJA MOYO. Hata mimi nitakuunga mkono....
 
Mkuu kwa hongera kwa kazi nzuri uliyoifanya(your observation) hatuwezi kuongelea ukombozi wa Tanzania bila kugusa maeneo kama haya. Vijana wanaharibika na sisi tupo tu bila hata ya kusema lolote hata mtu haonyeshi kama vile linamchukiza.
 
hivi bado vitoto sana na ni chini ya miaka 20 ..nadhani umri unawaruhusu kufanya haya...
Nakumbuka enzi zangu niko pale tboys nlikuaga naibuka disco vumbi night ni noma kila siku...
Na ukikutana na mimi utaeza kufikiri nsapoteza mwelekeo ila mwisho wa siku nkatoka na dvsion one huyoo nkasepa mlimani..
Lo tukikutana huezi amini..ni umri tuu huwa unapita

kumbuka wewe ni kijana wa kiume na wale ni wa kike alafu wako form 4 wewe ulikuw a-level
 
NingaR - kwa hiyo unabariki utovu wa nidhamu na ukahaba unaofanywa na hawa wadogo zetu? Je upo tayari kuona mtoto wako au mdogo wako akifanya uhuni kama huo ili hali ukipata tabu ya kumlipia ada?
Hebu tujaribu kutafuta suluhu ya kudumu, Tanzania itajengwa na Watanzania....
 
mimi zaidi,jinsi walivyokuwa wakifuatilia hyo mistari ya nyimbo na kukata viuno! Nilitamani hata kuwauliza kama na kusoma ndo hivyohivyo.

Ndio hao hao wanaofeli hata 'dini knowledge' na kuleta kizaazaa na matamko yasiyoisha!
 
Hongera sana Kasim Kasian! Hiyo ndio maana halisi ya taaluma ya Ualimu. Ualimu si kuwamezesha wanafunzi theory kisha wanafeli, bila kujua kwa nini? Kufanya hivyo ndiko kunakowatofautisha Waalimu na form Six leaver au wale wanaodandia fani au kufundisha uchochoroni. Tunapaswa kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi inayofaa. Kama kila Mwalimu akifanya kama wewe thamani ya Mwalimu itarudi. USIOGOPE!! UTAPATA FADHILA NYINGI, ACHANA NA WATU WANAKUVUNJA MOYO. Hata mimi nitakuunga mkono....

pamoja sana!
 
Ingekua nchi zilizoendelea walishalifanyia kazi hili swala na washamtia hatian kinyozi kwa kua tupo bongolala,tiss wanakunywa tu baa!
 
Utafiti mzuri hao ni baadhi tu. Mimi ni mwalimu hayo mambo yanatokea kila siku watoto wa kike wanatumika kulea familia kwa kujiuza, kesi za watoto kuchukua waume za watu ni nyingi na mke wa mtu akija shuleni anasema mwambieni mwanafunzi wenu akapime tu. Maambukizi ya ukumwi ni mengi watoto wanatembea na watu wazima na wengi wanapata mimba. Kizazi cha jk kinaangamia wao hawataki kusoma ila hela za haraka na kujirusha madarasani hamna kitu na utoro ni kawaida. Sijui ni laana ama ndio utandawazi. Hakuna utakalo jaribu kuwashauri wakusikia wao wanasema najua zaidi yako.
 
natumia nokia e5 kwenye jf sijui like unatupia vp we ni mzalendo wa kweli wa malezi ya kizazi kijaacho lkn ndipo tulipofikia ukitaka kuamini watoto wa leo 4m 4 hawaogopi, chukua namba ya simu mrushie elfu tano kwa tigo pesa halafu mwambie apande pikipiki aje guest fulani anakuja
 
Watoto wenyewe mnazalia wazazi wenu ninyi mnakimbilia mijini mnajifanya mnatafuta maisha.
Hivi babu na bibi "wazazi wako" wanaweza kuwa na mbio zakukimbizana na wajukuu? hasa hawa mnao walea huku mijini mkiona mambo magumu mnawahamishia vijijini kwa wazazi wenu.
Lazima tufike mahali tulee wanetu wazazi walitulea sisi tunapo kwepa majukumu yetu kwakupeleka watoto Vijijini walelewe na wazazi wetu "bibi na babu zao" matokeo yake ndo hayo wazee umri umekwenda muda wakufuatilia masomo yao hawana nikipindi chao chakula mafao.
Nashukuru mdau kwakuliona hilo ila ulipaswa kuwashauri ingawa siyo lazima wafuate utacho washauri ila ungekuwa umetimiza wajibu wako kama mzazi/mshauri angalao baadae waweze kujutia kutokushika ulilo washauri hapa Jf sidhani kama wanamuda wakuperuzi.
 
unayoyaongea ni ya ukweli ofisa.Mimi kinachoniudhi ni kwamba,baadhi ya wazazi hawazingatii malezi ya wazazi wao,na kusikiliza maoni ya waalimu.Hapa mzazi akiitwa shule na kuambiwa mwanao anajishughulisha na 1,2,3...Atakuja juu,na kauli chafu,akiwatuhumu waalimu labda wanawivu au vitu vingine kama hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Watoto wenyewe mnazalia wazazi wenu ninyi mnakimbilia mijini mnajifanya mnatafuta maisha.
Hivi babu na bibi "wazazi wako" wanaweza kuwa na mbio zakukimbizana na wajukuu? hasa hawa mnao walea huku mijini mkiona mambo magumu mnawahamishia vijijini kwa wazazi wenu.
Lazima tufike mahali tulee wanetu wazazi walitulea sisi tunapo kwepa majukumu yetu kwakupeleka watoto Vijijini walelewe na wazazi wetu "bibi na babu zao" matokeo yake ndo hayo wazee umri umekwenda muda wakufuatilia masomo yao hawana nikipindi chao chakula mafao.
Nashukuru mdau kwakuliona hilo ila ulipaswa kuwashauri ingawa siyo lazima wafuate utacho washauri ila ungekuwa umetimiza wajibu wako kama mzazi/mshauri angalao baadae waweze kujutia kutokushika ulilo washauri hapa Jf sidhani kama wanamuda wakuperuzi.

unajua nini jcb? Isingekuwa rahisi tu mimi kuzungumza palepale. Chochote kingeweza kutokea na ukizingatia kinyozi mwenyewe anatafuna mirungi na big G,pengine hata bangi anavuta huyu.Lakini niliahidi kwamba,nitatoa taarifa kwa waalimu wao,na ujumbe utawafikia hata wale ambao hawakuwepo pale saluni siku ile.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: jcb
Wakifeli mitihani utawasikia "yakhe baraza la mitihani linatuonea sisi waumini wa dini ya kii*#@&".
 
Leo niliingia SALUNI
moja amitaa ya Holili(BODA)-Moshi mida ya saa 11 jioni,kwaajili ya
kupunguza nywele.Nikawakuta wanafunzi wawili wa kike(kati ya kidato cha 2
hadi 4). Kinyozi naye amekaa kwa pembeni,anatafuna Mirungi na Big G
huku wakipiga stori.Matendo niliyoyaona ambayo siwezi kuyaandika,ni
kwamba binti mmoja kati ya wale alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na
kinyozi yule.Kinyozi akaanza kunihudumia huku akijisifu kuwa yeye
anafahamika sana,punde si punde wakaingia wanafunzi wengine wawili wa
kike.Hawa walikuwa ni wa form 4(mmoja alikuwa na kitabu cha chemistry
form 4) ktk shule moja hapa holili.Kinyozi akanifinya kidogo,akaniambia
"sinimekuambia nafahamika? Hawa wote nawanyoa mimi" akawasha
muziki,wanafunzi wakaanza kucheza hapo,mara nyingine anaacha
kuninyoa,anacheza nao kidogo.Ni mengi nimeyashuhudia jamani. Sasa
ikabidi,wale wasichana wamkazanie jamaa aninyoe haraka "wewe vipi? mnyoe
kaka wa watu haraka unamchelewesha!"
Sasa mimi nikajiuliza,hizi division 4 and 0 zitapungua kwa hali kama
hi? Na maambukizi ya magonjwa ya zinaa je?
MAONI YANGU: Wazazi wenye watoto wanaosoma shule za kutwa,muwe makini
na watoto wenu kwasababu,wengi wanaharibikia mitaani,disco na sehemu
kama hizi alafu mwisho wa siku wanafeli masomo yao,alafu lawama zote
anatupiwa mwalimu shuleni na serikali.
Hapo wakifeli lawama lukuki kwa walimu,tena wengine wanalaumu NECTA nakumbuka matokeo ya form 4,2010 kwa vile ulikua mwaka wa uchaguzi wakasema walimu waliosahihisha walikua CHADEMA nilicheka sana,yaani watu wanasingizia siasa kila sehemu.
 
Back
Top Bottom