Wanafunzi wa kike kutoboa Pua hasa shule za msingi ni sawa?

Wanafunzi wa kike kutoboa Pua hasa shule za msingi ni sawa?

Kutoboa pua,kuvaa vikuku
Zote signs hizo

Ova
Hakuna signs zo zote.

Hapo zamani kwa wanawake wa pwani na wale wa jamii ya kihindi kutoboa masikio na pua halikuwa jambo la ajabu wala aibu. Pia kuweka jino la dhahabu hasa kwa wenyeji wa Tanga.

Masikio yanawekwa herini (zamani ilikuwa dhahabu)
Pua inawekwa kipini (cha dhahabu)

Hapa kati hivi vitu viliondoka kwenye fasheni.

Leo hii umekuwa mjadala mkubwa wala sioni faida yake.
 
Ni kweli..wanatobolewa wakiwa wadogo ili wapone haraka..halafu ili kuzuia hilo tundu kuziba kilikuwa kunawekwa kijiti ili utakapokuwa mkubwa na uwezo wa kununua hereni au kipini pasiwe pameziba.
Hakika Mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Hivi kutoboa pua au masikio ni maadili mabovu?
 
Watu wa bara acheni ujinga, kama watu wa bara wakitoboa kipini ndo umalaya, pwani ni jambo la kawaida mtu anatopoa kisha anaweka kijiti,

Sasa mnakuja huku then mna pre conceived notion zenu
Kweli kabisa, hawajui utamaduni wa watu halafu wanajifanya kutafsiri.

Hebu wacheki filam za kihindi wataona moja kati ya mapambo huwa yanaunganishwa mpaka kwenye pua.
 
Hakuna kitu sikipendi kama kuona mtu katoboa pua na masikio tundu zaidi ya moja, halafu hereni na vipini vya jero jero .
Wewe sasa ndo tupo pamoja...
Kutoboa siyo nongwa ila kutoboa zaidi ya tundu moja huo ndo ushenzi
 
Hivi kutoboa pua ni maadili mabovu?
Siku hizi ndo imejengeka hii dhana Mkuu hasa baada ya huu utoboaji wa kasi ya ajabu hasa huku mijini na chanzo cha yote ni aina ya wanawake ambao wanatoboa kuonekana ni ile aina ya wanawake fulani ambao kwa muonekano wa haraka haraka wanaonekana wana maadili yasiyofaa.
 
Hakuna tatizo. Mbona masikio wanatobolewa hata shule hawajaanza? tofauti ya kutoboa masikio na pua ni nini?
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Hapo ni malezi....mimi mama sijatoboa hata sikio yeye anaanzaje kutoboa pua!
 
Kipindi niko la saba...kuna mtoto alikuaga darasa la kwanza na alikuaga ametoboa pua. Tena yeye alikuaga anavalishwa na kipini kabisa. Kwenye darasa hilohilo akawepo mtoto wa kiume amesokotwa dreads. Sa sifahamu kuwa yumkin kulikua na makubaliano na uongozi wa shule labda... Kuna watoto ni tamaduni zao labda zinawaruhusu...
 
Mie jamii niliyotoka ni kawaida hata mtoto mdogo anayejifunza kutembea anaweza toboa sikio au pua, kwetu sio tatizo
 
Huku pwani mtoto anatobolewa pua mdogo sana kwa sababu nyama ya pua inakuwa laini na ni kitu cha kawaida. Ukiona ni mtoto bas ni wazazi wake .
 
Back
Top Bottom