Wanafunzi UDSM wagomea uteuzi wa viongozi Daruso | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi UDSM wagomea uteuzi wa viongozi Daruso

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::3/17/2009

  Wanafunzi UDSM wagomea uteuzi wa viongozi Daruso

  Ellen Manyangu na Felix Mwagara
  Mwananchi

  WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wamegoma kuchagua uongozi mpya wa serikali yao, na sasa wanapinga kitendo cha mshauri wao kuteua serikali ya muda.

  Uongozi wa UDSM ulitangaza kuufuta uongozi wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso) wakati wanafunzi waliporejea chuoni hapo mapema mwaka huu baada ya mgomo wa kupinga sera ya mikopo ya elimu ya juu uliosababisha taasisi hiyo kufungwa.

  Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa wanafunzi hao walitakiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao wa mawasiliano ya kompyuta, lakini hawakujitokeza kufanya hivyo na ndipo mshauri wa wanafunzi alipoamua kuteua viongozi wa muda.

  Mshauri huyo, Dk Martha Qorro alitangaza serikali hiyo Machi 3, akitaja majina ya viongozi hao wa muda, lakini wanafunzi sasa wanapinga uteuzi huo wakisema kuwa hawakupewa haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka.

  “Hivi inawezekanaje uongozi wa chuo uufute uongozi wa Daruso halafu uwateue viongozi wao, tena kutoka katika uongozi walioufuta," alihoji mwanafunzi Alphonce Patrick.

  "Kama walitaka wawakilishi wetu sisi wanafunzi, kwa nini wasitupe uhuru wa kuchagua viongozi tunaowataka badala ya kutuchagulia wao.

  “Kama chuo kimeamua kuivunja Daruso, basi kitoe nafasi kwa wanafunzi kuchagua viongozi wengine kwa hiari yao na si kuchaguliwa na ofisi ya mshauri wa wanafunzi. La sivyo huo utakuwa uongozi wa ofisi ya Dean na si Daruso.”


  Lakini Mwananchi ilipowasiliana na Waziri wa Fedha, Msigwa Bahati alithibitisha kuwa wanafunzi hawakutumia haki yao walipotakiwa kupiga kura, ingawa waziri huyo wa muda alijibu kwa kifupi.

  “Ndiyo mimi ni kiongozi na nimechaguliwa na ofisi ya mshauri wa wanafunzi. Kama Dean ametoa nafasi kwa wanafunzi kuchagua viongozi online na hawakuchagua, unategemea nini kifanyike? Au wewe mwandishi unatakaje," alihoji Bahati.

  Ismael Emmanuel, ambaye ameteuliwa kuwa rais wa muda, aliiambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa ndiye kinara wa timu hiyo ya muda ya Daruso, lakini akakataa kueleza aliteuliwaje, akidai kuwa yuko darasani.

  Jibu kama hilo lilitolewa na makamu wake, Patrick Damas na waziri mkuu wa serikali hiyo ya muda ya wanafunzi, Reginald Goodchance, ambaye alidai kuwa si msemaji wa Daruso hiyo.

  Mshauri wa wanafunzi, Dk Qorro alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko mkoani Kilimanjaro.
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hawa wanafunzi wanafikiria migomo migomo tuuuuuuuu. Someni nyie watoto sisi tunawalipia masomo yenu alaaah!!
   
 3. n

  ndotomtaa Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fair player yes but you dont practise fair play to UDSM students. Mzee hujapita hapo juu nini? Ufisadi ndio uko hivyo, it seems umeshakucorrupt na wewe. Tunahitaji mapinduzi ya nchi nzima, sasa lazima yaanzie kwenye grass root level. UDSM students wanahitaji support. Alaa, hujui demokrasia nini?
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ndotomtaa;

  Mwaka wa kwanza nilikuwa Hall Six wa pili Hall 5 wa tatu Hall 6. Revolution square nineenda sana, Kupigwa virungu nilipigwa mara 2. Mara ya 3 nikakataa kwenda kwenye mgomo. Hiyo ilikuwa ni mwaka wa mwisho!

  Katika masuala matano wanayodai unakuta mawili ndo ya maana.

  Na dhana kuwa kila anayepinga migomo hajapitia channel hiyo ya usomi IFUTE Kabisa.

  Asante
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Shule ni pamoja na kupambana na mifumo yenye kila dalili ya kufuga ufisadi na utawala wa kimakundi. Shule si kukaa kitako na kusikiliza tafiti za kale huku ukuinyamazia uchuro unazingira leo.
  Hii ni Count down.
   
 6. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wanafunzi wa UDSM wanatakiwa kujiuliza wamefuata nini pale chuoni, kabla hawajaanza kudai mambo ambayo hata hawakujua wangeyakuta.

  Siku ya kwanza mwanafunzi yeyote aliyoingia chuoni pale na hata vyuo vingine vyovyote, alikuwa na nia moja tu; nayo ni kusoma na kelewa anachofundishwa ili aweze kufaulu mitihani yake na afuzu elimu ile aliyoomba kusomea kwa kiwango cha juu. Kama kuna madai katika kukwamishwa kwao kufikia azma hiyo, watakuwa na haki na ni busara kuidai ili malengo yao yafanikiwe.

  Kama madai yao ni kwa nia nyingine yoyote, sidhani kuwa ni madai ya msingi. Yatakuwa ni madai ya nyongeza tu. Wanao wajibu wa kuyadai kama kufanya hivyo hakutapotosha azma yao ya msingi ya kuwa mahali pale.
   
 7. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #7
  Mar 18, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee fair,halls ulizokaa zinaonyesha wewe fisadi kabisa. Hall six two times? Tuliopitia pale tunajua ili upate kukaa hall six unatakiwa kufanya nini.
   
 8. K

  Kleptomaniacs Member

  #8
  Mar 18, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Manifest and latent functions! Chuoni wanachuo hawaendi kukaa madarasani tu! baadhi yenu mnataka kutuambia kwamba kwahiyo kwa kuwa wapo chuoni kusoma kazi yao iwe hiyo tu! kama wewe ulifanya hivyo ulikuwa mvivu wa kufikiri, chuoni ni mahala pa kukuza vipaji mbalimbali, wanaharakati,wanasiasa, viongozi nk wanatokana na harakati hizo mbalimbali na sio na watu ambao wao hufikiria kwamba kazi yao ni kwenda kukariri nadharia na kusomea mitihani tu! hongereni sana wadau wa UDSM kwa kupigania demokrasia na haki zenu na sio kuwa makondoo na mazumbukuku yapokeayo tu kila kila kinacholetwa tupo nyuma yenu.
   
 9. K

  Kleptomaniacs Member

  #9
  Mar 18, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Manifest and latent functions! Chuoni wanachuo hawaendi kukaa madarasani tu! baadhi yenu mnataka kutuambia kwamba kwahiyo kwa kuwa wapo chuoni kusoma kazi yao iwe hiyo tu! kama wewe ulifanya hivyo ulikuwa mvivu wa kufikiri, chuoni ni mahala pa kukuza vipaji mbalimbali, wanaharakati,wanasiasa, viongozi nk wanatokana na harakati hizo mbalimbali na sio na watu ambao wao hufikiria kwamba kazi yao ni kwenda kukariri nadharia na kusomea mitihani tu! hongereni sana wadau wa UDSM kwa kupigania demokrasia na haki zenu na sio kuwa makondoo na mazumbukuku yapokeayo tu kila kila kinacholetwa tupo nyuma yenu.
   
 10. K

  Kleptomaniacs Member

  #10
  Mar 18, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  my Tz upo sahihi kabisa hawa ndio walikuwa wanufaika na bila shaka mpaka sasa ni wanufaika wa ka system kwahiyo haitushangazi anapochukulia migomo negatively inawanyima raha jamaa zake kwenye system! wangependa kuendelea kula keki ya taifa undisturbed!enough is enough watz wa sasa sio wale wa 47!mpaka kieleweke tutakomaa nanyi
   
 11. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Wanapoambiwa wapige kura zao online, swali la kujiuliza, endapo vyumba vya kufundishia (Lecture Theatres) hazitoshi mpaka wengine huwa wanachungulia madirishani, hiyo miundombinu mingine kama access ya internet kwa kila mwanafunzi imewekwa lini? Labda kwa kuwa sijafika muda mrefu huko Mlimani, pengine mambo yamebadilika sana!

  Nina ushahidi wa baadhi ya wanafunzi wengi sana waliofaulu vizuri zaidi A Level mwaka jana, wazazi wao waliwapiga marufuku ku-apply UDSM na wakawashauri waende wakasome Mzumbe kwa kuwa Mzumbe hakuna migomo na migogoro ya kila siku. Na ndiko wanakosoma mpaka sasa!

  Kama mambo yataendelea hivi, miaka kadhaa ijayo UDSM kibaki kuwa chuo cha wababaishaji waliokariri kufanya migomo badala ya kusoma!
   
 12. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Samahani wanaJF leo nitapingana na madai ya UDSM. Uzuri ninauzoefu mkubwa juu ya wanafunzi wa vyuo vya bongo na serikari zao kwakuwa nimeshiriki kikamilifu. Tukiacha matatizo madogomadogo, wanafunzi wa vyuo vikuu bongo ni very complex individuals.

  Hapa wanalalamika kutopewa uhuru wa kuchagua viongozi wao. Lakini report hii pia inasema walipewa nafasi ya kuchagua viongozi wao kwa njia ya mtandao. Kimsingi njia hii ndio inayotumika vyuo vya ulaya nafikiri hii ndio njia inayopaswa kutumika vyuo vyote bongo kwani ni cost effective in terms of both time and money.

  Swala la kuhoji uhalali wa Chuo kufuta Daruso, nadhani wanatakiwa kutambua kuwa Daruso ilikuwa enacted kutoka kwenye Prospectus ya Chuo. Hivyo kwa namna yoyote ipo chini ya chuo na chuo kinamamlaka ya kuintervene baadhi ya mambo. Kimsingi ni kama taasisi yoyote ya serikari, ndio maana Daruso ipo intitled kupata ruzuku Chuoni.

  Ujumbe wangu kwa wanafunzi wa UDSM, kuna mambo ambayo ni haki ya mwanafunzi mfano conducive learning environment i.e. adequate lecture theaters & lecturers, class facilities, computers and internet access and full furnished libraries among others. Hivi ni vitu ambavyo wanaweza negociate na ikibidi kuandamana ili vipatikane. But kuna issues kama exams regulations, bylaws, accommodation, transport, etc. Haya si majukumu ya msingi ya chuo japo chuo kinaweza facilitate hivyo hawapaswi kugomea.Hali kadhalika uongozi wa wanafunzi ni mpango wa chuo kuweza kuwasiliana kirahisi na wanafunzi na kushirikisha wadau wake (wanafunzi) katika baadhi ya maamuzi. Hivyo chuo kinaweza amualolote juu ya DARUSO. Mbona vyuo vya ulaya wanafunzi hawagomigomi kama bongo kunanini hapo???
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wana JF naomba nitumie fursa hii kuwasalimu wote, naamini kuwa afya zenu ni nzuri na mnaendelea kuchapa kazi kama kawaida kila mmoja katika nafasi yake.Nimeanza na salamu kwa kuwa ni muda mrefu kidogo sijaonekana kwenye hili jukwaa letu.

  Mkuu pamoja na kutufahamisha kwamba una uzoefu na serikali za wanafunzi vyuo vikuu vya bongo, kama huo mtazamo wako ndiyo uelewa wako ulivyo, basi hukustahili kuwa kiongozi wa wanafunzi, huenda ulikuwa mamluki. Ushahidi upo wa kutosha kuwa baadhi ya watu wanagombea uongozi vyuoni kutafuta maslahi binafsi na si kuwakilisha maslahi ya wanafunzi.Kuwepo chuo cha elimu ya juu hakuishii kwenye kuingia darasani kukariri 'theories' mbalimbali na kusubiri mitihani. Chuoni ni mahali pa watu kukuza vipaji vyao, vya kisiasa, kiuongozi, kitaaluma, kimichezo, kiutamaduni, n.k, n.k
  Na ili uweze kuonyesha kipaji chako ni lazima upewe nafasi ya kufanya hivyo.Kinyume chake ni kutaka kuvigeuza vyuo vikuu viwe sawa na shule za msingi au sekondari, maana kule ndipo watu wanaamrishwa kama vile wako jela.Nakumbuka nilipokuwa sekondari pale Moshi tech. uongozi wa shule ulikuwa unakaa kutathmini na kupendekeza majina ya wanafunzi wanaofaa kuwa viongozi, then yanapelekwa kwa wanafunzi kwa ajili ya kupigiwa kura, utaona kuwa walimu wale waliona umuhimu wa wanafunzi kuchagua viongozi wanaowataka. Kwa kiwango cha chuo kikuu wanafunzi wenyewe wanao uwezo wa kuunda kamati za kuwatathmini wanafunzi wenzao wanaoomba kuchaguliwa kuwaongoza, na hili limekuwa likifanyika miaka nenda rudi.Hili suala la mikopo lisiwafanye watu mkasahau mambo ambayo ni haki ya wanafunzi na wana uwezo wa kuyatekeleza bila matatizo.Uongozi unaowekwa na menejimenti ya chuo unatekeleza matakwa ya menejimenti na hauwezi kutetea maslahi ya wanafunzi.Na ndio maana uongozi wa chuo hauwezi kuwachagulia wafanyakazi wa chuo viongozi wa vyama vyao kama vile RAAWU, UDASA, n.k, hilo ni jukumu na haki ya wafanyakazi au wanataaluma wenyewe.Na hata kwenye senate kunakuwa na uwakilishi wa pande zote yaani wanafunzi, wanfanyakazi/wanataaluma na serikali kwa maana ya wizara.Hivi tujiulize kama tunahubiri ushirikishwaji wa wanachi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo hadi huko nyanchabakenye kwa wavuvi na wakulima,kwamba wanatakiwa washirikishwe, yaani hatuoni umuhimu wa wasomi kuipata hiyo haki ya kushirikishwa?Kwakuwa kuna mambo mengi tu ya kipuuzi na kimabavu yanayofanywa na menejimenti za vyuo na hawapendi kuulizwa ulizwa au kubughudhiwa wanaona ili kuondoa usumbufu wa kufuatiliwa matendo yao maovu ni kuivunjilia mbali na daruso kisha wateue watu wao.Na kitu kibaya zaidi haki za wanafunzi zinaminy sana vyuoni kama hakuna strong leadership, wengine hudiriki kuwarubuni na hata kuwahonga viongozi wa wanafunzi.
  Hata hivyo tujiulize maswali machache kama kweli walipewa nafasi ya kupiga kura online, je miundombinu inatosheleza?na hao waliotakiwa kupigiwa kura ili wawe viongozi ni nani aliyewateua au kuwapitisha kugombea?ni utaratibu gani ulitumika kuwapata wagombea?

  Nimalizie kwa kuwasihi wadau wenzangu, tujaribu kufanya utafiti wa kina kuhusu maisha ya vyuo vikuu tanzania kwa sasahivi hususani mlimani, inawezekana wengine mna uzoefu wa miaka ya 80-90 ambako mambo yalikuwa mswano, sasahivi udsm inaendeshwa kisiasa,tena siasa chafu, siasa za mabavu, pale udsm kuna maprofesa wa deokrasia/utawala/uongozi lakini hawajui kutumia taaluma zao kwa maslahi ya umma badala yake wameweka mbele ubinafsi.
  Nimeyasema hayo kwa kuwa nina uzoefu wa kutosha katika siasa za vyuo vya elimu ya juu nchini mwetu na nimeshiriki kiasi kikubwa katika harakati za kutetea maslahi ya wanafunzi wa elimu ya juu. Sisemi hivyo kwa kutafuta sifa au kujikweza lakini ukweli ni kuwa nilipata kuwa Raisi wa serikali ya wanafunzi katika moja wapo ya vyuo vya elimu ya juu hapa nchini nikiwa mmoja wa waanzilishi wa TAHLISO tukahangaika hadi ikapata usajili pamoja na mizengwe mingi sana tuliyokutana nayo, ingawa nasikitika kwamba sasahivi taasisi hii inaonekana imepoteza muelekeo.Na kwa nafasi yangu nimeweza kujifunza mambo mengi sana ambayo watu wengine ambao hawajishughulishi kutaka kujua mambo kwa undani huishia kuwalaumu wanafunzi tuu.Kama kuna mtu anaikumbuka ile tume ya mama sinare(mwanasheria) iliyoundwa na dr.Ng'wandu kati ya 2003-2004 ilitoa ripoti ya uchunguzi wake kuhusu matatizo ya vyuo vya elimu ya juu vya umma nchini,alikuwemo muhingo rweyemamu akiwakilisha kundi la wanafunzi, wakati huo akisoma tumaini iringa na akiandikia gazeti la mwananchi.Ripoti yao ilitolewa hadi kwenye magazeti aliyeisoma anajua kilichopendekezwa lakini wizara ya elimu ya juu inafanya mambo mengine kabisa na yale mapendekezo yako kwenye makabati ya mama naomi katunzi na maghembe pale wizarani.

  Nawasilisha.
   
  Last edited: Mar 18, 2009
 14. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwita sitaki tulumbane sana hapa swala la msingi ni kuwa hoja iliyopo imetolewa na mtau UDSM na haijaonyesha tatizo la miundombinu kama ni sababu ya kugomea uchaguzi. Kimsingi hoja yako haina tofauti na wanafunzi waliokwenye mgomo kwani upeo wao wakuchuja hoja huwa nimdogo wakati wa mgomo nahujikuta wakitamka mambo hata yasioyamsingi. Kasome vizuri hoja ya mdau then review comment yako.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Lakini yote haya yanahusiana nini na kupachikiwa uongozi? Hao viongozi vinara watakuwa na credibility gani kwa wanafunzi ambao wanapaswa kuwawakilisha? Na huo uongozi wa Chuo kweli utaweza kujidai kuwa inajadiliana na wawakilishi wa wanafunzi wanapojadiliana na watu walioteua wenyewe? This is beyond a bad joke!
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mbona hatuambiwi hao wagombea ambao walikuwa wapigiwe kura walipatikanaje? Wangapi katika hao wanafunzi wana access na mtandao? Na how secure is that mtandao system? Hata nchi zilizoendelea haya mambo bado yanawasumbua, itakuwa sisi? Na uamuzi wa namna gani uchaguzi ufanyike ilibidi ushirikishe wanafunzi. Kinachoendelea hapa ni yale yale ya kuburuzana kwa vile wameshika mpini!

  Amandla........
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  DARUSO ilifutwa.

  Imerudi lini?
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wakati wetu tungesema haya yote ni magirini! Vijana wamewastukia.
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu,
  suala hapa sio kulumbana, tunatakiwa tuiangalie hali ya watanzania wenzetu wanaotaabika kwenye vyuo vikuu sasahivi.Hebu jaribu kutembelea mlimani, DUCE, ARDHI UNIV.,DIT, SUA na vingine vingi ujionee jinsi wadogo zetu wanavyotaabika.Kama hauko bongo fanya kadri uwezavyo uujue ukweli.
  Tatizo lako ni sawa na watanzania wengine wanaoamini kuwa uwezo wa mwanafunzi, na uelewa wake wa kufikiria mambo na kuyapambanua ni mdogo, kitu ambacho sio sahihi hata kidogo.Kuna watu wako vyuoni vichwa vyao vinachemka ile mbaya. Ukumbuke kuwa Mwanafunzi ni binadamu kamili anayefikiria na kuamua sawasawa na mtu mwingine, kama kuna udhaifu au jazba au gadhabu hilo ni jambo la kawaida hata maprofesa/Mawaziri/wakuu wa mashirika/wakuu wa mikoa/wakuu wa wilaya (kama Mnali) wanakuwa katika hali hizo hizo sawa na wanafunzi.Na kabla ya kuwashambulia ulitakiwa ujibu maswali yaliyoulizwa na wadau hapo juu, namimi pia nimekuuliza;(1) Miundombinu ya kupiga kura online inakidhi haja na mahitaji ya kufanya hivyo?(2) Hao wagombea nani au kamati ipi ilifanya kazi ya kuwachuja na hatimaye kuwapendekeza kugombea uongozi wa wanafunzi?(3)Wanafunzi wenyewe wanaotafutiwa viongozi wameshirikishwaje ili wapate viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya maslahi yao?Kwahiyo kabla ya kuwanyooshea kidole ulitakiwa ujiulize japo maswali ya msingi kama hayo.
  Mwisho ninakushauri uondokana kasumba ya kwamba wanafunzi uwezo wao wa kuchuja hoja ni mdogo, tena sahau kabisa.Kama wakati unawaongoza wenzako (sijui chuo gani na mwaka upi) ulikuwa na uwezo mdogo wa kuchuja hoja, nakuhurumia sana, na usichukulie kwamba wote ndivyo walivyo.
   
  Last edited: Mar 19, 2009
 20. m

  mchakato Member

  #20
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  kaka ulikua dit nini?
   
Loading...