Wanafunzi UDSM wagomea uteuzi wa viongozi Daruso

Mkuu,
suala hapa sio kulumbana, tunatakiwa tuiangalie hali ya watanzania wenzetu wanaotaabika kwenye vyuo vikuu sasahivi.Hebu jaribu kutembelea mlimani, DUCE, ARDHI UNIV.,DIT, SUA na vingine vingi ujionee jinsi wadogo zetu wanavyotaabika.Kama hauko bongo fanya kadri uwezavyo uujue ukweli.
Tatizo lako ni sawa na watanzania wengine wanaoamini kuwa uwezo wa mwanafunzi, na uelewa wake wa kufikiria mambo na kuyapambanua ni mdogo, kitu ambacho sio sahihi hata kidogo.Kuna watu wako vyuoni vichwa vyao vinachemka ile mbaya. Ukumbuke kuwa Mwanafunzi ni binadamu kamili anayefikiria na kuamua sawasawa na mtu mwingine, kama kuna udhaifu au jazba au gadhabu hilo ni jambo la kawaida hata maprofesa/Mawaziri/wakuu wa mashirika/wakuu wa mikoa/wakuu wa wilaya (kama Mnali) wanakuwa katika hali hizo hizo sawa na wanafunzi.Na kabla ya kuwashambulia ulitakiwa ujibu maswali yaliyoulizwa na wadau hapo juu, namimi pia nimekuuliza;(1) Miundombinu ya kupiga kura online inakidhi haja na mahitaji ya kufanya hivyo?(2) Hao wagombea nani au kamati ipi ilifanya kazi ya kuwachuja na hatimaye kuwapendekeza kugombea uongozi wa wanafunzi?(3)Wanafunzi wenyewe wanaotafutiwa viongozi wameshirikishwaje ili wapate viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya maslahi yao?Kwahiyo kabla ya kuwanyooshea kidole ulitakiwa ujiulize japo maswali ya msingi kama hayo.
Mwisho ninakushauri uondokana kasumba ya kwamba wanafunzi uwezo wao wa kuchuja hoja ni mdogo, tena sahau kabisa.Kama wakati unawaongoza wenzako (sijui chuo gani na mwaka upi) ulikuwa na uwezo mdogo wa kuchuja hoja, nakuhurumia sana, na usichukulie kwamba wote ndivyo walivyo.

It wont make a difference tukiendelea kulumbana kwa muelekeo huo. Haya mkuu nimekusikia
 
It wont make a difference tukiendelea kulumbana kwa muelekeo huo. Haya mkuu nimekusikia

Hakuna shaka mkuu,
tuendelee tu kuelimishana na kufahamishana, lengo letu liwe ni kujijenga kadri iwezekanavyo, na zaidi sana tuyatambue mazingira yetu vizuri.
 
Back
Top Bottom