Pendael6410
Senior Member
- Oct 18, 2012
- 154
- 214
Kilio cha wanafunzi wanaosomea Udaktari Bingwa chuo cha KCMC.
------------
Kwa madaktari tunaosoma Masters mbalimbali hapa KCMC na kulipiwa ada na serikali tumegawanyika katika makundi mawili.
1. Global Fund (hawa wanalipiwa kila kitu ikiwemo ada,research,malazi na chakula)
2. Basket fund( hawa wanalipiwa ada na research tu)
Mkataba wa kusomeshwa husainiwa baina ya serikali na daktari mnufaika. Chuo hupewa tu barua ya dhamana ambapo serikali huji commit kwamba italipa gharama tajwa kwa madaktari tajwa.
Tatizo limekuja kwamba serikali kwa kipindi cha zaidi ya miaka 3 haileti ada chuoni hivyo kufanya uendeshaji wa masomo kuwa mgumu sana.
Sasa mwezi February,mkuu wa chuo KCMC(Provost) alituandikia barua madaktari wote tunaosomea ubingwa mbalimbali(wanaodhaminiwa na serikali) kutuarifu kwamba serikali haijaleta chochote na ikifika semister ya pili(ambayo imeanza mwishoni mwa March) basi hata kuwa na la kufanya zaidi ya kutufukuza chuoni.
Jana tarehe 03 May 2017 tulipokea barua( wote wanufaika wa serikali) kuanzia 1st hadi 4th year kwamba tunahitajika Urgently leo katika kikao cha dharura.Na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba hadi leo serikali haijaleta chochote na chuo kimeamua kuturudisha wizarani tukajue namna ya kupata hizo ada.
Nimeambatanisha na barua zote 3....ya mwezi February na May...
Leo tumekutana na Mkuu wa Chuo na team yake...wametupa barua rasmi za kutufukuza.
Kwasasa tumeunda team itakayojaribu kufikisha tena hili suala wizarani ingawa barua wamepelekewa mara kadhaa na hawatoi jibu lolote.
-------------
NB: Serikali iliangalie sula hili kwa umakini, wapo wanafunzi wa mwaka wa nne sasa serikali hajawalipia hadi mwanafunzi anadaiwa 40 milioni.
Kujenga nchi ya viwanda kusipuuze elimu ya vijana wetu mwisho wa siku wakapita njia za mkato na kununua vyeti feki kariakoo.
Na Yericko Nyerere