Wanafunzi 10 tu ndiyo wanasoma Kitongoji cha kisiba.

BEDECCA

Member
Oct 27, 2016
10
4
Kiji cha Mwela, kitongoji cha Kisiba kina wanafunzi kumi (10) tu wanaosoma katika shule za sekondari, uongozi wa BEDECCA umefanya utafiti na kujua sababu inayopelekea kitongoji hicho kuwa na wanafunzi wachache ni suala la UTORO, wengi wao huwa wanaachia njiani.

Suala hilo limekithiri sana katika eneo hilo asilimia kubwa ya wanafunzi wa kike wameachwa huru na kurejea nyumbani muda wanaotaka hasa masaa ya usiku, kuna watoto wa kike wadogo sana ambao ni darasa la nne hadi darasa la saba kuruhusiwa kuingia ndani kuanzia saa nne za usiku na kuendelea huku wakikuta wazazi wao wamelala.

Hii inapelekea kuwa na ndoa za utotoni, mimba za utotoni na kuacha shule. Baadhi ya watoto wakiume kutokuhudhuria shuleni kwa sababu ya kuenda kutazama ngoma za asili huku wengine wakijiusisha na kucheza ngoma ambazo ni siku za shule.

Pia ajira za utotoni (vibarua) ambazo hufanya siku za shule na wengine kushinda mitaani bila sababu. Kwa mwaka huu walioweza kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba ni watoto watatu (3) tu nawao walikuwa wanaishi mbali na sehemu hiyo.

Makundi mabaya kwa wanafunzi si vizuri kuwaruhusu kujiunga katika makundi hayo. Watoto elimu kwanza mengine baadaye.
NDUGU WAPENDWA TUNAANDAA TAIFA GANI LA BAADAYE!

Uongozi wa Bedecca umepanga mwezi ujao yaani mwezi wa kumi na mbili kuenda katika kitongoji hicho kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa Elimu na kufundisha jinsi ya kuwa na malezi bora kwa mtoto
 
Back
Top Bottom