Wanachuo - boom hilo...!!!??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachuo - boom hilo...!!!???

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by HAKUNA, Mar 21, 2012.

 1. H

  HAKUNA Senior Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanachuo; katika wakati huu ambao mmeshapokea/mnasubiri kupokea fedha za kujikimu (BOOM), jaribu kuwa na mpango mzuri wa matumizi, kuepuka kuingia katika hali ngumu ya kifedha baada ya muda mfupi na hata kutumbukia kwenye madeni. Nilishuhudia mwanafunzi wa chuo (binti) akikamatwa supermarket kwa kuiba, katika wiki hili, katika vyuo vingine kumekuwa na taarifa za wizi (hata kwa kutumia silaha - mapanga,visu) kati ya wanachuo wenyew; haya yote yanatokea baada ya BOOM kukata na maisha kuanza kuwa magumu. Mabinti wamekuwa wakienda kumbi za strarehe na kujaribu kuweka mitego.

  Tukumbuke ule usemi "PESA INAONGEA", usemi huu ni dhahiri ndugu zangu; utakuta unapo-pokea fedha tu mipango yote mizuri utashangaa inatoweka na mawazo mapya yanakuja, PESA inasema na wewe, "twende tukanunue ngou", "twende club", "twende tukanywe na washikaji" na mengineyo mengi. Jitahidi kuheshimu na kusimamia mpango wako wa Matumizi. Usiangalie wengine wanaishi vipi?, mpango wako wa matumizi, ndio maisha yako.

  Usiishi kwa imani ambayo baadae haitatenda kazi, kwamba zitapatikana nyingine. Kutoka wapi.......????, hapo ndipo wengine wanapojikuta wameangukia kwenye vitendo vibaya kama wizi, umalaya, na mengineyo. Epuka kabisa kufanya mpango wa matumizi kwa pesa ya kutarajia....FROM SOMEWHERE...????. Hakikisha una FOCUS kwa hicho ulichonacho.

  Vile vile unaweza kufikiri jinsi ya kuongeza pesa uliyonayo, hata hapo chuoni unaweza kufanya jambo la kuongeza kipato chako (THINK..). Itakusaidia kuwa na uhakika wa kipato chako, badala ya kuwa zinatoka tu.

  Jitahidi kutokutembea na pesa taslimu (mfukoni/begi) amabzo hujapanga kwa siku hiyo zitakuwa na matumizi gani ni rahisi kushawishika kufanya matumizi ambayo hujapanga, kama siku kuna utamaduni wa vitu kutembezwa mitaani, hivyo unapokuwa na pesa ambazo hazina matumizi ni rahisi kushawishika kununua.

  Naamini wengine wataweza kuongeza yale ambayo yatatusaidia katika kuwa na akiba ya fedha za kujikimu chuoni katika muda husika, kutokana na uzoefu......KARIBU......!!!

   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ukipata hilo boom naomba unikopeshe japo milioni 1.
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  We unaongea nin?watu tulipewa bumu tangu tuko kitaa,saa hzi ni mwendo wa Code 001.
   
 4. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mkuu kanisa lako liko Ubungo Kibangu au Mbezi tuje kujisubscribe kabisa manake mahubiri yako ni mazito. Ila wasiwasi wangu ni kuwa asilimia 90 ya wanachuo watakaosoma huu uzi wataona ushauri wako ni kama nguvu za giza vile. Na sio kosa lao kwani fedha mara zote ndio huwa inatafuta pa kutokea hata kama hauna mpango wa kuitoa itakulazimisha tu ili ichoropoke
   
 5. Mad Max

  Mad Max JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,434
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  pesa yenyewe nikiwatajia hapa aibu. ndio maana wakaiita ya meals and acomodation. but wengi wanatumia kununua vitu kama cm, nguo, Saloon, etc.

  ujana huu!
   
 6. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mkupuo mmoja haufiki hata laki 5 husninyo! Labda elf 10...
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Mnachekelea kupata laki 4 kwa miezi 3 kweli bongo wanafunzi vichwa maji
   
 8. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Ushauri mzuri, hongera kwa angalizo...
   
 9. H

  HAKUNA Senior Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakipokea BOOM, club zinajaa....!!!
   
 10. mtzedi

  mtzedi JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  vipi kuhusu mimi ni loan
   
Loading...