Wanachama Yanga wachana na kuchoma magazeti ya Reginald Mengi!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
20160522_120556.jpg

Wanachama wa Yanga wamecharuka na kufanya kitendo kinachoonyesha ni hasira kutokana na kuchana na kuchoma moto magazeti.
Wanachama hao wa Yanga, leo wamechoma moto magazeti ya Nipashena The Guardian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Wanachama hao wamefanya hivyo wakipinga Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusakamwa kw amakusudi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
“Hii sasa imetosha, huyu Mengi na magazeti yake anamsakama Manji kila anapoona Yanga inafanya vizuri. Mara tu baada ya Yanga kutinga robo fainali hatua ya Kombe la Shirikisho, basi vyombo vyake vimeanza kuandika kwamba anatakiwa sijui kuondolewa Coco Beach.
“Hakuna asiyejua Manji amestaafu Quality Group, sasa anamtaja wa nini. Au anataka ashindwe kufanya kazi za Yanga kwa utulivu.

“Watuache, kweli tutatangaza watu wa Yanga waachane na kununua bidhaa zake,” alisema Abuu Chehekaheka.
Pamoja naye, wanachama wengine kama Edward Matiku, Clement Michael na Hashimu Mtanza nao walimuunga mkono pamoja na wengine waliokuwa pale kabla ya kuanza kuchoma moto magazeti hayo wakionyesha kuwa na jazba.

Hata walipoulizwa sababu kuu za kuchoma magazeti hayo yanayomilikiwa na Mengi, hakuna aliyetaka kujibu huku wakionyesha kuwa na jazba.

20160522_120410.jpg 20160522_120427.jpg 20160522_120813.jpg
 
Mengi ni shabiki wa Yanga na mfanyabiashara kama Manji. Hakukuwa na haja ya kuihusisha timu(brand ya Yanga) na ugomvi kati ya wafanaybiashara hawa wawili maana ugomvi wao upo bayana na ni wa muda mrefu. Manji hatakuwepo milele Yanga, hivyo si vizuri kuwafanyia fujo,dharau na kejeli wadau wengine wa Yanga kwa sababu ya Manji. Pia Manji atambue kuwa hao wanaopigana vita kwa niaba yake, ipo siku watapigana dhidi yake maana hawana maslahi na timu, bali mtu binafsi.

Kukosa ueledi katika masuala ya soka, ndio chanzo cha kudorora kwa timu zetu kimataifa. Tukatae kuharibu brand ya Yanga kwa maslahi ya mtu binafsi. Pamoja na mafanikio tuliyoyapata chini ya Manji, Yanga ni kubwa kuliko yeye. Manji si Yanga, wala Yanga si Manji.
 
Mafisadi ni wajanja sana.
Wameshawanunua baadhi ya wanachama ili wahalalishe ufiasadi wao. Kama Cocobeach inamuhusu awajibike asijifiche nyuma ya Yanga wala CCM.
Na mwaka huu Magufuli akiamua kutenda haki sawa kwa wote wataikimbia hii nchi. Yanga ina tija gani kwa taifa kama itatumika kama kichaka cha mafisadi?
Club ni kwa ajili ya kuburudisha tu na sio kutumika kutuibia.

Kama kuna ukweli kwenye tuhuma hizo basi atumbuliwe.
Hii nchi tumebaki nyuma sana kwa mambo ya kipumbavu.

Mtu anatuhuma halafu anapanga watu wa kumpigia kelele .
Mara wengine wanatetewa kidini,wengine kikabila,wengine kikanda ,wengine kichama na kisiasa na sasa Wamekuja kisoka. Ajabu kabisa. Hao wanachama wananufaika nini endapo serikali itakua inahujumiwa na matajiri ili kufadhili vilabu?
Yani miundo mbinu ya Taifa iharibiwe ili kulinda mfadhili wa timu?
Je,siku akifa ina maana taifa letu ndio litaishia hapo?
 
Brand ya Yanga ni kubwa sana kiasi kwamba haiwezi kutosha kukaa mfukoni mwa Manji au Quality Group. Wanachama na mashabiki tukatae Yanga kufadhiliwa na Mjomba maana yeye ni wa kupita tu. Walikuwapo kina Gulamali, Abbas Tarimba, nk. Walikaa pembeni na timu ikaendelea. Timu iendeshwe na michango ya wanachama, bidhaa za klabu, udhamini kutokana na brand na sio sugardaddy.
 
View attachment 349864 Wanachama wa Yanga wamecharuka na kufanya kitendo kinachoonyesha ni hasira kutokana na kuchana na kuchoma moto magazeti.
Wanachama hao wa Yanga, leo wamechoma moto magazeti ya Nipashena The Guardian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Wanachama hao wamefanya hivyo wakipinga Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusakamwa kw amakusudi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
“Hii sasa imetosha, huyu Mengi na magazeti yake anamsakama Manji kila anapoona Yanga inafanya vizuri. Mara tu baada ya Yanga kutinga robo fainali hatua ya Kombe la Shirikisho, basi vyombo vyake vimeanza kuandika kwamba anatakiwa sijui kuondolewa Coco Beach.
“Hakuna asiyejua Manji amestaafu Quality Group, sasa anamtaja wa nini. Au anataka ashindwe kufanya kazi za Yanga kwa utulivu.

“Watuache, kweli tutatangaza watu wa Yanga waachane na kununua bidhaa zake,” alisema Abuu Chehekaheka.
Pamoja naye, wanachama wengine kama Edward Matiku, Clement Michael na Hashimu Mtanza nao walimuunga mkono pamoja na wengine waliokuwa pale kabla ya kuanza kuchoma moto magazeti hayo wakionyesha kuwa na jazba.

Hata walipoulizwa sababu kuu za kuchoma magazeti hayo yanayomilikiwa na Mengi, hakuna aliyetaka kujibu huku wakionyesha kuwa na jazba.

View attachment 349857View attachment 349858 View attachment 349859
Upuuzi mtupu. Hawana lolote hao. Yaani unachana gazeti kwa sababu za kipuuz, only in Tanzania!
 
duh sasa ndo wamefanya nini? me nikadhani labda wamevamia kiwanda cha magazeti na kuchoma, kumbe wamenunua kwa pesa yao halafu wakachoma!!! kweli akili ni mali hapo hata hawajui kua kitendo cha kulinnunua tu gazeti kwanza wame transfer ownership ya gazeti husika. pili hawajamkomoa mengi bali ndo kwanza wamemuongezea mauzo ya magazeti yake maana watu wengi watakua na shauku ya kujua magazeti yake kesho yataandika nini. inasikitisha.
 
njaa mbaya hapo wamelishwa mrungula wanaanza kufanya ujinga.. na mimi kwaniaba ya wanayanga wapenda maendeleo nalaani kitendo hicho chakuchana magazeti ya ipp
 
Malofa kweli mwezi mzima wafanye hivyo hivyo kila walionapo wayanunue yote wayachome moto. Ama kweli hasira za mkizi furaha ya mvuvi. Sio kosa lao mizigo sokoni kariakoo imepungua fuso nyingi zinaishia mabibo, temeke na buguruni
 
Back
Top Bottom