GE2025 Wanachama CHADEMA wazuiwa kuingia mahakamani kesi ya Lissu

GE2025 Wanachama CHADEMA wazuiwa kuingia mahakamani kesi ya Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ambapo kesi ya Mwenyekiti wao inaendelea kusikilizwa, kwa madai kwamba ukumbi wa mahakama ni mdogo.

Wanachama hao wamelalamika kwamba kitendo hicho kimewanyima fursa ya kushuhudia mwenendo wa kesi muhimu kwa chama chao, wakieleza kuwa nafasi nyingi ndani ya ukumbi zimejazwa na askari polisi badala ya wananchi.
1757406309281.png
Screenshot 2025-09-09 112433.png

 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Septemba 9, 2025

Part 1

Kesi imeanza Mhe. Lissu ameingia. Katuga amesimama na kutambulisha jopo lake na mshitakiwa amesema yuko tayari.

Jaji amesema naomba nitoe mrejesho wa tulianzia wapi jana na tuliishia wapi? Ametoa huo mrejesho kuwa sasa tuendelee na lile pingamizi la endapo mahakama hii ina mamlaka ya kuendelea.

LISSU: Mh. Jaji nashukuru, jana nilipewa nafasi nikasome. Sasa hiyo kazi nimeifanya usiku kucha kwahiyo naomba kwa kuanzia nieleze tofauti zilizopo kati ya hizi nyaraka mbili na ili nisiwachanganye ninaposema rekodi ya Ukonga maana yake ni ile niliyoletewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu na hakimu FRANCO KISWAGA ndio alimpa Kamishina mSaidizi wa Polisi Rabi Stima.

Rekodi ya Ukonga nina maana ni hiyo nyaraka niliyoletewa na Hakimu Kiswaga.

Kwahiyo nikisema rekodi ya Mahakama hii nitakuwa namaanisha ile niliyopewa jana.

Sasa naomba nianze.

1. Utofauti wa rekodi ya Ukonga ina kurasa 16 tu. Rekodi ya Mahakama hii ina kurasa 101. Sasa hizo kurasa zingine zilikuwa wapi? Nyaraka za mahakama zinawezaje kuwa na utofauti wa namna hii? Katuga hawakumpa hii niliyonayo mimi.
2. Rekodi ya Ukonga haina ile scanned berg (kibox pembeni kulia) inamaanisha ni original. Sasa ya ukonga haina lakini niliyopewa jana inazo hizo scanned berg. Sasa ililetwa na mahakama lakini sio original.

3. Rekodi ya ukonga inaanza tarehe 18/08 na inaishia Tar. 18/08. Kwa kifupi ilianza siku hiyo hiyo na kuishia siku hiyohiyo. Kesi ilianza na kumalizika siku hiyohiyo. Rekodi ya Mahakama hii imeanzia April 10, 2025 na kuishia Agosti 18, 2025. Mliyonipa hapa ilikuwa imekamilika kwa kila kitu.

4. Ukurasa wa 1 wa rekodi ya Ukonga na Ukurasa wa 86 wa rekodi ya Mahakama hii. Ukiangalia ile ya Ukonga page 1 ni kwamba commitall proceedings ilianza immediately. Yani mwanzo pale committal proceedings open, evident on itself lakini kwenye rekodi ya mahakama hii ukurasa wa 86 kulikuwa na ubishani mkubwa sana ambao umerekodiwa. Utaona baada ya corum kuna heading inaitwa Proveedings Mr. Katuga alielezea mambo kadhaaa.... ilianza hivyo. Kinachofuata kuanzia page 86 hadi 89 ni submissions kati ya prosecution na mimi mwenyewe. Rekodi ya ukonga mabishano hayo hayapo kabisa. Lakini hii niliyopewa hapa kila kitu kipo.

Utaona kwa mfano ukurasa wa 87 rekodi ya mahakama hii Hakimu alisema nimezingatia mawasilisho ya pande zote. Na akatambua uamuzi wa mahakama kuu. Mambo hayo kwenye document nikiyoletewa hayakuwepo na hakuambatanisha.

6. Kwenye ukurasa wa 15 wa rekodi ya Ukonga kuna orodha ya mashahidi halafu kuna maneno kuwa na mimi mshitakiwa I WILL CALL THE FOLLOWING WITNESSSES
Lakini kwenye ukurasa wa 100 wa rekodi ya Mahakama hii inasema I will call my witnesses and I will have my Advocates.

Kwenye rekodi ya ukonga na kwenye orodha ya mahakama hii hawajaandikwa mashahidi wangu.

Sio kwamba hawakuwepo, niliwataja lakini nyaraka hizi hazina majina hayo.

1. Samia Suluhu Hassan
2. Isdory Mpango
3. Kassim Majaliwa

Hao wote niliwataja lakini hawakuandika kabisa.

Nitarudi kwenye hilo la majina baadae.

Lakini ieleweke kuwa majina hayo nilitaja mchana kweupe kila mtu alisikia na ilikuwa kwenye Open Court. Aliamua kwa matakwa yake mwenyewe kutokuyaandika.

Hizi nyaraka zote zimetoka Kisutu na zinadai kuwa ni committal proceedings.

Which one is forgery and which one is original.

Mahakama hii inapaswa kujibu why this differences?

Jana niligusia kidogo kwamba kulikuwa na maahirisho mengi sana.

Nilisema yalikuwa zaidi ya 10 hayo maahirisho. Niliposoma usiku nimegundua iliahirishwa mara 13.

Kesi inapoahirishwa kwenye commitall proceedings s. 265(1) the court must record the reason of adjournment and for reasonable cause that adjournment can be granted.

Na hiyo sababu ya msingi lazima iandikwe katika mwenendo.

Sasa nataka nioneshe namna mahakama ya Mh. Franco Kiswaga ilivyoheshimu huo utaratibu wa kisheria.

Part 2 inaendelea post inayofuata.

Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ambapo kesi ya Mwenyekiti wao inaendelea kusikilizwa, kwa madai kwamba ukumbi wa mahakama ni mdogo.

Wanachama hao wamelalamika kwamba kitendo hicho kimewanyima fursa ya kushuhudia mwenendo wa kesi muhimu kwa chama chao, wakieleza kuwa nafasi nyingi ndani ya ukumbi zimejazwa na askari polisi badala ya wananchi.
Inasikitisha Sana.
 
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ambapo kesi ya Mwenyekiti wao inaendelea kusikilizwa, kwa madai kwamba ukumbi wa mahakama ni mdogo.

Wanachama hao wamelalamika kwamba kitendo hicho kimewanyima fursa ya kushuhudia mwenendo wa kesi muhimu kwa chama chao, wakieleza kuwa nafasi nyingi ndani ya ukumbi zimejazwa na askari polisi badala ya wananchi.

“Tunalalamika kwa sababu tuna haki ya kikatiba kushiriki na kusikiliza kesi ya kiongozi wetu, lakini tunazuiwa kwa kisingizio cha ukumbi kuwa mdogo, huku askari wakiwa wamejaa ndani,” alisema mmoja wa wanachama waliokuwa nje ya viunga vya mahakama.

Wameitaka Mahakama na Jeshi la Polisi kuhakikisha haki ya wananchi ya kufuatilia mashauri ya wazi inalindwa, hasa kwa kesi zinazomgusa kiongozi wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa katika jamii.
1757408382591.png
 
Duh.....makubwa kila kona hiki chama kinashambuliwa hakika kinapitia wakati mgumu kuliko wakishinda hapa hakuna wakukizuia hii inanikumbusha enzi za siasa za ubaguzi wa rangi kule Afrika ya Kusini (apartheid). Hii hatua ni muhimu kwao ili kujitofautisha na vyama vingine shikizi vyenye kubeba maslahi ya wachache pekee
 
Back
Top Bottom