Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA

Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana kikiadhimisha miaka 34 tangu kianzishwe, zaidi ya wanachama wake 1,550 wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Maswa, Luhende Mipawa, alisema kuwa wanachama hao wamerudisha kadi hizo kwa wakati tofauti siku tatu tangu CCM ilipozindua maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
"Tangu CCM walipozindua sherehe zao za kutimiza miaka 34, tumepokea wanachama wapatao 1,550 kutoka matawi mbalimbali ya CCM katika Wilaya ya Maswa ambao wamejiunga na chama chetu," alisema.
Alisema kuwa dalili hizo zinaonyesha wazi wananchi wa wilaya hiyo walivyo na imani kwa CHADEMA wanachokiamini ndicho chama kikuu cha upinzani hapa nchini.
"Hizi ni dalili njema kuwa wananchi wanakikubali chama chetu ndiyo maana unaona kwa muda wa siku tatu tumevuna wanachama 1,550, tuna kazi kubwa ya kutimiza kiu kubwa ya wananchi wetu," alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mmoja wa wanachama wa CCM aliyehamia CHADEMA, Geni Jilala, alisema kuwa kwa sasa chama hicho kimekosa mwelekeo na kupoteza misingi iliyowekwa na Mwalimu Nyerere na matokeo yake kimekuwa ni cha kuwatumikia wenye fedha huku wanyonge wakiachwa, hivyo CHADEMA ndiyo chama mbadala.
"CCM ya leo inawakumbatia wenye fedha, kwani ndiyo wana sauti ndani ya chama, sisi wanyonge tumeachwa, hivyo tumeona heri tukimbilie CHADEMA ambacho ndicho chama cha wanyonge," alisema Jilala.
Aliongeza kwamba kutokana na mgawanyiko na makundi yanayokitafuna chama hicho wilayani humo, kuna hatari ya kusambaratika na kubaki na jengo la ofisi. Hivi karibuni Katibu wa Uenezi wa CCM Taifa, Kapteni John Chiligati, alishindwa kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Maswa katika viwanja wa MADECO, baada ya wananchi kutojitokeza kwa madai kuwa chama hicho hakina jipya la kuwaeleza wakazi wa mji huo.

Source: Tanzania daima

Good news
 
Namna nzuri ya kutatua tatizo ni kukiri kuwepo kwa tatizo lenyewe, ili kutafuta ufumbuzi. Habari ya sisiemu kufulia iliandikwa kwa kirefu sana na gazeti la Rai Mwema wiki chache zilizopita, kwamba ilitokana na kushuka kwa ruzuku yake iliyotokana na chadema kupata viti vingi vya ubunge katika uchaguzi wa mwaka jana! Mengi tutayaona lakini. Time will tell.
:laugh::boxing:
 
Kwa sisi ambao tayari tunajua jinsi CCM ilivyoiharibu Tanzania, wakati tukiendelea kuhangaikia maisha yetu ya kila siku, kila mmoja ajiwekee lengo la kueleimsha angalao watanzania 100 kila mwaka ambao kutokana na hila ya CCM ya miaka mingi ya kufifisha akili za watanzania, bado wanaitumikia CCM. Tukifanya hivyo sasa, nina hakika CCM kwenye uchaguzi wowote ujao itaingia ikiwa imedhoofu na isiyo na mategemeo.

Kwa kukosa kwetu ujasiri, na kuachia mambo ya siasa yafanywe na watu wasio na
ufahamu, adhabu tuipatayo sasa ni wananchi wenye akili kuongozwa na majuha.
 
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema kuwa nguvu ya vyama vya upinzani imeongezeka na kusababisha ruzuku ya CCM ipungue, hivyo aliwataka Wana CCM kubuni vyanzo vingine zaidi vya mapato ili kuiimarisha kiuchumi.
Aidha, alikiri kuwa Wana CCM wamekuwa wakitishwa na kunyong’onyezwa na mafanikio ya CHADEMA iliyoyapata katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Sanjari na kukiri hilo, Rais Kikwete alitumia sehemu ya hotuba yake hiyo kurejea tena matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa kutoa maelezo ya kuwatia moyo Wana CCM, akiwataka wasiwe wanyonge kwani bado chama chao kilijitahidi kupata ushindi mkubwa.
Akionekana kuiacha CUF na kuishambulia zaidi CHADEMA huku akitumia maneno yenye husuda ya kisiasa ndani yake, Rais Kikwete alisema: “Nadhani tunatishwa na kelele na propaganda za chama fulani na bwana Fulani, ambazo zinajenga hisia kama vile wako wengi sana na wamepata ushindi mkubwa sana hata kuliko CCM. “Hilo si kweli, ingawaje safari hii wamepata viti vingi kuliko uchaguzi uliopita. “Kwa nini tujisikie wanyonge baada ya kupata ushindi mnono kiasi hicho?” alisema Rais Kikwete.

Source: Tanzania daima

Naye Makamba akitaja takwimu za kura za uraisi, alisema : Kikwete alipata kura kadhaa, Slaa kadhaa na "ndugu yetu " Lipumba alipata kadhaa......
Hapo ndo nikajua kuwa Professor Lipumba keshafanywa pumba na Makamba, yaani ni domu tupu....masikini kachakachuliwa na ndo mwisho wa CUF
 
Wacha JK aendekeze mipasho sisi tartiiib tunachukuwa nchi. Ajiandae kujiunga na kina Yusuf Mzee kwani huko ndiyo kwenye fani yake.Tunaka kiongozi mahiri mwanaume wa shoka ambaye akisema anachukia ufisadi mafisadi wote wanatetemeka, wacha mkwere arembe rembe kuwakenualia washikaji zake kina RA, wakae wakijua kuwa kiama chao kinakuja.
 
Wandugu sasa ni wakati wa kuongeza nguvu tena badala ya kutembea tuanze kukimbia. Naomba Mungu Makamba aendelee kuwa katibu mkuu CCM mpaka 2015 ili ujinga wake uzidi kuvuruga chama kile. Shibuda na makada wetu jamani Shinyanga hakikisheni hao wanachama wanapewa elimu ya uraia ipasavyo ili nao wakashawishi wengine mara kumi yao. Jamani tukumbuke Mao Tse Tung alivyopambana mpaka kuikomboa China ni kila mwanachama wake kushawishi wengine kumi. Mtaji upo wazi ni wananchama wa CCM walioumizwa na kupoteza tumaini tena ni mamilioni. Mungu ibariki Chadema ukombozi umekaribia.
 
..."BILA CCM IMARA NCHI ITAYUMBA"........mzee wangu aliwahi kusema
 
CCM.... ikiwa imesheheni watu wa makada tofauti ieanza kujirekebisha kwa kuanza mikakati stahili ambayo ni kuhakikisha inakuwa imara zaidi
 
Upinzani ukiimarika maamuzi ya hovyo hovyo yatapungua. Hii ni dalili njema.
 
Back
Top Bottom