Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 6, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana kikiadhimisha miaka 34 tangu kianzishwe, zaidi ya wanachama wake 1,550 wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Maswa, Luhende Mipawa, alisema kuwa wanachama hao wamerudisha kadi hizo kwa wakati tofauti siku tatu tangu CCM ilipozindua maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
  “Tangu CCM walipozindua sherehe zao za kutimiza miaka 34, tumepokea wanachama wapatao 1,550 kutoka matawi mbalimbali ya CCM katika Wilaya ya Maswa ambao wamejiunga na chama chetu,” alisema.
  Alisema kuwa dalili hizo zinaonyesha wazi wananchi wa wilaya hiyo walivyo na imani kwa CHADEMA wanachokiamini ndicho chama kikuu cha upinzani hapa nchini.
  “Hizi ni dalili njema kuwa wananchi wanakikubali chama chetu ndiyo maana unaona kwa muda wa siku tatu tumevuna wanachama 1,550, tuna kazi kubwa ya kutimiza kiu kubwa ya wananchi wetu,” alisema.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mmoja wa wanachama wa CCM aliyehamia CHADEMA, Geni Jilala, alisema kuwa kwa sasa chama hicho kimekosa mwelekeo na kupoteza misingi iliyowekwa na Mwalimu Nyerere na matokeo yake kimekuwa ni cha kuwatumikia wenye fedha huku wanyonge wakiachwa, hivyo CHADEMA ndiyo chama mbadala.
  “CCM ya leo inawakumbatia wenye fedha, kwani ndiyo wana sauti ndani ya chama, sisi wanyonge tumeachwa, hivyo tumeona heri tukimbilie CHADEMA ambacho ndicho chama cha wanyonge,” alisema Jilala.
  Aliongeza kwamba kutokana na mgawanyiko na makundi yanayokitafuna chama hicho wilayani humo, kuna hatari ya kusambaratika na kubaki na jengo la ofisi. Hivi karibuni Katibu wa Uenezi wa CCM Taifa, Kapteni John Chiligati, alishindwa kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Maswa katika viwanja wa MADECO, baada ya wananchi kutojitokeza kwa madai kuwa chama hicho hakina jipya la kuwaeleza wakazi wa mji huo.

  Source: Tanzania daima
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema kuwa nguvu ya vyama vya upinzani imeongezeka na kusababisha ruzuku ya CCM ipungue, hivyo aliwataka Wana CCM kubuni vyanzo vingine zaidi vya mapato ili kuiimarisha kiuchumi.
  Aidha, alikiri kuwa Wana CCM wamekuwa wakitishwa na kunyong'onyezwa na mafanikio ya CHADEMA iliyoyapata katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
  Sanjari na kukiri hilo, Rais Kikwete alitumia sehemu ya hotuba yake hiyo kurejea tena matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa kutoa maelezo ya kuwatia moyo Wana CCM, akiwataka wasiwe wanyonge kwani bado chama chao kilijitahidi kupata ushindi mkubwa.
  Akionekana kuiacha CUF na kuishambulia zaidi CHADEMA huku akitumia maneno yenye husuda ya kisiasa ndani yake, Rais Kikwete alisema: "Nadhani tunatishwa na kelele na propaganda za chama fulani na bwana Fulani, ambazo zinajenga hisia kama vile wako wengi sana na wamepata ushindi mkubwa sana hata kuliko CCM. "Hilo si kweli, ingawaje safari hii wamepata viti vingi kuliko uchaguzi uliopita. "Kwa nini tujisikie wanyonge baada ya kupata ushindi mnono kiasi hicho?" alisema Rais Kikwete.

  Source: Tanzania daima
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katika kilele cha sherehe za CCM Mwenyekiti wa CCM Kikwete alisema yafuatayo:
  Alisisitiza chama kujiimarisha kiuchumi akisema hali ya kifedha ya chama hicho si imara na kinategemea zaidi ruzuku inayotokana na ushindi kwa upande wa wabunge na madiwani.

  Kwa ajili hiyo, vyanzo vya asili vya chama kupata fedha za kujiendesha vimesahaulika, kwani miaka yote ada na michango ya wanachama vilikuwa ndizo nguzo na vyanzo vikuu vya mapato ya chama.

  "Hatuwezi kuacha jukumu la kugharimia uendeshaji wa chama chetu mikononi mwa wafadhili matajiri. Tunahatarisha uhuru wa chama chetu," alionya na kuongeza:

  "Bahati mbaya safari hii ruzuku hiyo imepungua kwa sababu ya nguvu ya vyama vya upinzani kuongezeka.

  Uchaguzi ujao nguvu ya upinzani ikiongezeka zaidi tutakuwa na hali mbaya."

  Source: Habari leo
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bado hawajaamka kumbe. poleni.
   
 5. f

  furahi JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli hizi ni habari njema kwa wa2 wa Mungu. Tunafarijika sana na natumaini maombi yetu yatajibiwa soon. Lakini baba Januari si ndiye aliyewaambia wana ccm wanaotaka kuondoka milango iko wazi?
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wameanza kukiri taratibu. Watalia!!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nilikuwepo huko mwisho mwaka jana, kwa kweli wamechoka na ccm yaani wanashangaa jk alishindaje?..hata hao watu 1550 si ajabu na bado chadema iendeleze mapambano..kwani mikoa ya shy na simiu nikati ya mikoa ambayo imeumizwa sana na ccm
   
 8. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi bado naamini wakulima, wafanakazi na vijana ni wana mapinduzi. Kwa sababu CCM wameyasahau makundi hayo na kujikita kwa matajiri watajuta kuzaliwa na kufikisha miaka 34.
   
 9. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama sio siasa, basi ni dalili njema kwamba wananchi wetu wanaanza kujitambua.Lakini mara nyingi nasita kuongelea vyama kwa kuwa najua origin ya vyama.It's just another devide and rule system in place.The truth is we have been cheated!Baba wa CCM na CHADEMA ni mmoja.
   
 10. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Jana kuna babu m1 mkoani Ruvuma alinifurahisha, alicema "...ccm chama chetu kiko imara, lakini kama kimepoteza mwelekeo, hasa kuchukiwa na vijana. Vijana wameondoka na wametuacha ss wazee na chama chetu..." Hata jana raisi sijui alijisikiaje kuhutubia majukwaa matupu mbele yake walikuwa watoto wa halaiki, huku watu wazima kwa uchache wakiwa kushoto kwake na kulia kwake, kitu kilicho mlazimisha kugeuka geuka kuwatazama wageni wake! Mh
   
 11. i

  ibange JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ccm ni marehemu mtarajiwa. nina hakika ccm ikianguka itaanguka jumla haitaamka tena
   
 12. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  safi sana.nimeipenda hiyo! cdm tusilale bado mapambano!
   
 13. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kwa mwenyekiti wa ccm kukiri kuwa nguvu ya upinzani imeongezeka,kwangu mimi napata faraja kwani hii ni dalili njema.Cha msingi kwa CDM ni kuanza tena kuwasha moto mikoani na vijijini kuamsha waliolala.
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Big up CDM, keep it up
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ya kujiona ndio washika hatamu yakianza legalega ndio kutimia kwa semi za wahenga wetu kwamba dalili za mvua ni mawingu ati mwenzangu.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinguzi kukiri hadharani katika kilele cha maadhimisho ya Kuzaliwa kwa CCM kwamba chama kina hali mbaya ya fedha na kwamba sasa hivi upinzani una nguvu ni ishara wazi kuwa CCM inaweweseka
   
 17. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ....bravooooooooo!
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naona sasa njia inaanza panuka zaidi
  Aluta continuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  :msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela:
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ndio maana sijui
   
 20. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usikate tamaa Zambia, Kenya na Malawi waliweza na wapinzani ndio wanaongoza nchi, kwanini sisi tushindwe? Ofcourse kuna vyama vingine viko kwa maslahi binafsi na CCM inavitumia vizuri kupunguza nguvu ya upinzani lakini pia kuna vyama makini kama CHADEMA. CCM imepoteza imani kwa umma wa watanzania, kimebakia kukumbatia mafisadi tu.
   
Loading...