Wanachadema wanaomkashifu Dr. Slaa wajifunze kwa CUF

Wanachadema wanaomkashifu Dr. Slaa wajifunze kwa CUF

Tangu Dr. W.P Slaa alipoamua kupumzika kufanya siasa za harakati mnamo mwaka 2015 kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokuridhishwa kwake na mchakato wa kumpata mgombea urais wa CHADEMA kumekuwa na kundi kubwa la Washabiki wa siasa linalomponda, kumkashifu na kujaribu kufuta mema yote yaliyofanywa na Dr Slaa katika harakati za kuimarisha upinzani wa kweli hapa nchini tangu wakati huo.

Kwa bahati mbaya sana muasis wa vitendo hivyo vya kashfa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiwatumia vijana wa mtandao wake John Mrema na Reginald Munisi. Hawa walikuwa wanafanya kazi ya kujenga dhana na kupandikiza maneno ya uongo na chuki kwa wajumbe wa vikao vyote vikubwa vya Chama yaani Baraza Kuu na Kamati Kuu. Wengine ambao walisikika kwa nyakati tofauti tofauti wakimchafua Dr Slaa kwa Watanzania ni Mh. Tundu Lissu na Mchg Peter Msigwa ambao walimtuhumu katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Hoja kubwa ikiwa ni kwamba Dr Slaa amenunuliwa na CCM na kwa upande mwingine wakidai Dr Slaa anapelekeshwa na Mkewe. Tuhuma zote ni tuhuma za kuudhi sana na kukera kwa mwanaume yoyote hususan mtu mzima wa makamo ya Dr Slaa.

Binafsi ninapoyatazama yanayoendelea ndani ya CUF ambao kauli mbiu yao miaka yote imekuwa ni Ngangariiiiii (Kwamba unyonge mwiko), Jino kwa Jino na Haki Sawa kwa Wote ikimaanisha kuwa suluhu ni mmoja kushinda tu, ndipo ninapoiona busara kubwa, hekima, unyenyekevu na kila aina ya utu wema toka kwa Dr Slaa. Dr Slaa ameamua kukaa kimya tangu wakati ule mpaka leo ili tu asikivuruge Chama chake cha CHADEMA. Je Dr Slaa angeamua au akiamua kutetea haki ya jasho lake ndani ya CHADEMA je Chama kitabaki? Hakitabaki. Isitoshe Dr Slaa tofauti na Prof Lipumba hakuwahi kuandika barua yenye maudhui ya kuacha kazi wala kujiuzulu bali aliomba kupumzika kwa muda. Na alikubaliwa na vikao vya Chama.

Dr Slaa anapaswa kupongezwa na kuigwa na wapenda demokrasia wote. Yeye kama binadamu amevumilia mengi tangu wakati ule mpaka leo. Heshima yake kwa jamii ya Watanzania imevunjwa na watu wachache na wamemuacha hana kitu. Lipumba ameshindwa kuvumilia dharau hizo ila Dr Slaa ameweza. WanaCHADEMA wote wanapaswa kumuheshimu na kuwa na Staha katika kumjadili.

Aliyemleta Lowassa Chadema mtujumiwa wa.kwanza ni Dr.Slaa na aliongea mwenyewe kwenye press conference tena walianza kushauriana na Lipumba.Lipumba akitaka Lowassa and CUF mimic his hind ikan a ni uungwaji mkono wa CUF bara.

Ukijaribu kupotosha kumbuka si peke.yako ulikuwepo Bongo.

Dr.Slaa ana feel guilty kwa sababu alichokitegemea kuwa haki kuwa ameondoka sababu ya kupumbazwa na Mwanamke.(Kama Delilah alimdanganya Samson ndivyo ilivyokuwa kwa Dr.Slaa.)Utamu wa choroko ulimfanya asahau responsibility zake
 
Ukitaka kuikosoa chadema inabidi uwe na roho ngumu sana ya kuvumilia matusi.Bavicha huwa hawajui kupinga hoja kwa hoja wao ni matusi tu

Umeshindwa kukosoa uonevu wa Mwenyekiti wako wa Chama Cha Mabwepande hunamoral authority hata ya kuigusa Chadema.
 
Tumeshindwa kukosoa uonevu wa Mwenyekiti wako wa Chama Cha Mabwepande hunamoral authority hata ya kuigusa Chadema.
Tatizo lenu huwa hakuna mwenye ubavu wa kuhoji chochote,nyie ni ndio tu
 
Aliyemleta Lowassa Chadema mtujumiwa wa.kwanza ni Dr.Slaa na aliongea mwenyewe kwenye press conference tena walianza kushauriana na Lipumba.Lipumba akitaka Lowassa and CUF mimic his hind ikan a ni uungwaji mkono wa CUF bara.

Ukijaribu kupotosha kumbuka si peke.yako ulikuwepo Bongo.

Dr.Slaa ana feel guilty kwa sababu alichokitegemea kuwa haki kuwa ameondoka sababu ya kupumbazwa na Mwanamke.(Kama Delilah alimdanganya Samson ndivyo ilivyokuwa kwa Dr.Slaa.)Utamu wa choroko ulimfanya asahau responsibility zake

Dr Slaa hakupinga Lowasa kuja CDM, bali alitaka chama kwanza kitafakari faida atakazo zileta NA pia sio kama mhombea.
 
Dr slaa mjanja alikomaa na ccm akapewa cash lipumba na uprofesa wake aliingizwa cha kike kama madiwani wa hai.
Hongera Kwa Josephine mushumbuzi.
Na lipumba angekuwa na mke sidhani kama angekubali ile tiketi ya go and return ya kigali,labda angemshauri wao waende Geneva.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Your post is very great, there is no one like Dkt Slaa he will remain an icon in the field of political race.
 
Mbona anarudi kuitafuta nafasi ya ukatibi mkuu was CHADEMA kupitia msajili was vyama vya siasa?

Wewe endelea na mradi wako, ila umebugi kuiingiza CHADEMA kwenye upuuzi wako.
 
Back
Top Bottom