Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 766
- 1,884
Tangu Dr. W.P Slaa alipoamua kupumzika kufanya siasa za harakati mnamo mwaka 2015 kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokuridhishwa kwake na mchakato wa kumpata mgombea urais wa CHADEMA kumekuwa na kundi kubwa la Washabiki wa siasa linalomponda, kumkashifu na kujaribu kufuta mema yote yaliyofanywa na Dr Slaa katika harakati za kuimarisha upinzani wa kweli hapa nchini tangu wakati huo.
Kwa bahati mbaya sana muasis wa vitendo hivyo vya kashfa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiwatumia vijana wa mtandao wake John Mrema na Reginald Munisi. Hawa walikuwa wanafanya kazi ya kujenga dhana na kupandikiza maneno ya uongo na chuki kwa wajumbe wa vikao vyote vikubwa vya Chama yaani Baraza Kuu na Kamati Kuu. Wengine ambao walisikika kwa nyakati tofauti tofauti wakimchafua Dr Slaa kwa Watanzania ni Mh. Tundu Lissu na Mchg Peter Msigwa ambao walimtuhumu katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Hoja kubwa ikiwa ni kwamba Dr Slaa amenunuliwa na CCM na kwa upande mwingine wakidai Dr Slaa anapelekeshwa na Mkewe. Tuhuma zote ni tuhuma za kuudhi sana na kukera kwa mwanaume yoyote hususan mtu mzima wa makamo ya Dr Slaa.
Binafsi ninapoyatazama yanayoendelea ndani ya CUF ambao kauli mbiu yao miaka yote imekuwa ni Ngangariiiiii (Kwamba unyonge mwiko), Jino kwa Jino na Haki Sawa kwa Wote ikimaanisha kuwa suluhu ni mmoja kushinda tu, ndipo ninapoiona busara kubwa, hekima, unyenyekevu na kila aina ya utu wema toka kwa Dr Slaa. Dr Slaa ameamua kukaa kimya tangu wakati ule mpaka leo ili tu asikivuruge Chama chake cha CHADEMA. Je Dr Slaa angeamua au akiamua kutetea haki ya jasho lake ndani ya CHADEMA je Chama kitabaki? Hakitabaki. Isitoshe Dr Slaa tofauti na Prof Lipumba hakuwahi kuandika barua yenye maudhui ya kuacha kazi wala kujiuzulu bali aliomba kupumzika kwa muda. Na alikubaliwa na vikao vya Chama.
Dr Slaa anapaswa kupongezwa na kuigwa na wapenda demokrasia wote. Yeye kama binadamu amevumilia mengi tangu wakati ule mpaka leo. Heshima yake kwa jamii ya Watanzania imevunjwa na watu wachache na wamemuacha hana kitu. Lipumba ameshindwa kuvumilia dharau hizo ila Dr Slaa ameweza. WanaCHADEMA wote wanapaswa kumuheshimu na kuwa na Staha katika kumjadili.