WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

asante mkuu huku mtaani kwangu manzese sokoni walikata tamaa...asante kwa kutupatia glucos....
Waambie wasife moyo, tupo hatua ya mwisho kuukaribia ushindi.


Hii ni vita takatifu kwakuwa ni vita kati ya wema na ubaya,
 
Kitengo cha mpambano JF kiko kazini leo.Ludo yuko ndumwa sasa sijui ni nani anakiongoza.
 
Salute mkuu.
Hakuna ukombozi utakaopatikana bila gharama, ccm wafahamu kuwa chadema ilipofikia si ya mbowe, si ya slaa,si ya arfi,si ya zitto nk. ? Ni chama cha watz kwahiyo hata wakiwafunga viongozi wote, wabunge wote! Chama kitaendelea kuwepo....maana ni chama cha watz...kwa mbinu wanazotumia wangefanikiwa miaka 13 iliyopita sio sasa.
Pipoooooooozzzzz!!!!!!!
 
Kitengo cha mpambano JF kiko kazini leo.Ludo yuko ndumwa sasa sijui ni nani anakiongoza.
Kwa kuwa kitengo iko hakina nia njema kinaendeshwa kwa siri.Lakini mungu mkubwa hawa maharamia wa nchi kavu watajulikana tu.
 
Mkuu Yericko Nyerere.

Umeweka sawasawa kisu kwenye mfupa! Nami naomba niwe kama muwindaji wa ndege! Nilenge shabaha kwanza ndio niachie manati bila kupiga kwenye kipago.

Naweke msingi wa nukta zangu kwa kusema yafuatayo.

1. CCM imeiacha misingi yake iliyo asisiwa nayo na kushika mkondo ambao haukuwa wa misingi mikuu, kwa kuicha misingi yake iliyo asisiwa nayo wananchi wengi wamekosa imani na matarajio ya ustawi endelevu kupitia ccm. (Misingi ya kujali utu, raslimali za nchi, udugu, amani na utulivu wa nchi, kupiga vita rushwa, nk havipo tena ndani ya ccm). CCM imeshindwa kutembea juu ya msingi yake na matokeo yake kwa kuogopa nguvu ya watu wenye fedha wamejikuta wanachagua wagombea ambao hawakidhi matarajio ya wananchi wala kufuata misingi iliyo asisiwa kwayo.
Mwl Nyerere alisha waonya mwaka 1995, kwa kuwaambia wachague mtu ambaye atakidhi matarajio ya watanzania maana watanzania wanahitaji mabadiliko. Alipaza sauti yake mzee watu pale Dodoma (R. I. P). "...Watanzania wasipo yaona, wasipo yapata mabadiliko ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm".

Yametimia! Watanzania hawana imani tena kuwa wanaweza kuyapata mabadiliko ndani ya ccm (kupitia wagimbea wa ccm), sasa hivi mabadiliko wanayatafuta nje ya ccm, nje ya ccm kupitia chama kikuu cha upinzani kinacho ilaza macho ccm. CHADEMA. Na ndio maana chama hiki leo kina watu wa familia ya Mwl Nyerere ambao nao kama watanzania wengine hawayaoti mabadiliko ndani ya ccm.

2. Watanzania wamechoshwa na uendashaji mbovu wa nchi yao ambao umegubikwa na rushwa kila mahali, rushwa imewaathiri watanzania kwa kuto kuzifaidi raslimali zao, madini yao yamebinafishwa kwa mikataba ya kilaghai, wanyama wao wanatoroshwa kwa rushwa na ghilba zisizo kuwa na haya, vyombo vya kusimamia haki na kulinda usalama wa watanzania haviaminiki tena! (Sio wananchi wa kawaida wala viongozi waandamizi wa serikali). Kila mahali ni rushwa, kwenye hili Mwl Nyerere aliwaambia wana ccm pale Dodoma "Chagueni mtu ambaye hata ukiulizwa swali, huyu atatusaidia kupiga vita rushwa?, jibu litoke ndani ya roho kwamba NDIO!" Wangapi wana ccm leo wanaweza kutoka mbele ya hadhara na kupiga kifua kwa kusema kiongozi/viongozi wetu wanapiga vita rushwa?! Hili limewachoshwa wananchi ndio maana wanaiona chadema kuwa ndio mkombozi wao na waliipa heshima kuanzia pale kwenye list of shame mwembe yanga.

3. Ccm kimeacha kuwa chama cha wakulima na wafanya kazi matokeo yake kimegeuka kuwa chama cha matajiri na mafisadi. Leo hii bila kuwa na mafurushi ya fedha ni vigumu kupenya kwenye chaguzi za ccm! Wenye chama ambao ndio wanawakilishwa na ile alama ya jembe na nyundo wanaona wameporwa chama chao! Kwa mantiki ya kawaida ukiporwa unacho miliki kama huwezi kukipigania kukirejesha unakuwa mpole na kutafuta kingine utakacho weza kuita cha kwako, hii ndio sababu ya wakulima na wafanyakazi wengi kuachana na ccm na kujiunga na chadema maana wamekuwa wanaambiwa wazi na peupe kuwa "ccm ina wenyewe". Wamewaacha wenyewe wenye ccm yao wamejiunga kwa chadema chama chao.

4. Ccm imekubuhi kwa kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini na makabila, labda bila kujua athari zake, mara kadhaa ccm wamekuwa wakinadi kuwa vyama flani vya upinzani nivya dini fulani au mahali fulani. Walianza na NCCR, wakaja na CUF kuwa ni chama cha kidini na chama cha wapemba magaidi, leo wanasema chadema ni chama cha watu wa kaskazini wakristo. Watanzania wamegundua kuwa wao ni wamoja hawataki tena kugawanywa kwa udini na ukabila, wengi walio chukizwa na mambo hayo wameichukia na kuidharau ccm kwa propaganda zake chafu, wamekataa hila hizi, wameamua kujiunga na jeshi la ukombozi ili kurudisha heshima na utu wa mtanzania ulio jali haki na usawa. Matarajio yao yapo ndani ya chadema.

HITIMISHO.
Ccm imewaongoza watanzania kwa miaka 50 (nusu karne) kwa kuwa imeshidwa kutatua matatizo na changamoto ilizokumbana nazo na nyingine kwa kuzisababisha yenyewe, basi kinahitajika chama kingine chenye watu wenye upeo na fikra mpya zenye muono mwingine tofauti nawa ccm ili kuikwamua nchi yetu kutoka kwenye hili tope.

Mwanamahesabu mmoja wa bara la Ulaya aliwahikusema "... Problems cannot be solved by the same level of thinking which created them"

Muhimu ni ccm kutambua tu kuwa hawana hati miliki ya kuwaongoza watanzania kama wameichoka na hawaitaki iendelee kukaa madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Yeriko kila baada ya ijumaa kuu huja pasaka kwa hiyo ikiona ijumaa kuu ujue pasaka inakaribia. Ni kuwa Cdm wasikurupuke na wafanye mambo kwa umakini.safari tulisha ianza nia tunayo sababu tunayo uwezo tunao KANANI NILZIMA TUTAFIKA
 
Yap yap yap!

Yericko Nyerere
Mohamedi Mtoi

Hakika Mi kwa mtazamo wangu wa kutambua na kuona,hakika naweza kusema ya kwamba mwisho wa mafisadi umefika rasmi!
Nawaambia ya kwamba Watanzania wa leo siyo wale wa miaka 28 iliyopita. Ninaweza kusema kabisa ya kwamba mbinu zote ya mafisadi iko mikononi mwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Hawa majambazi wa ccm wajikanyagekanyage tu ila hakika mwisho wao itagota pabaya.
Hata hawa polisisisiem waliongukia kiapo hakika ni amri tu wanatii kwani hata wao wenyewe hawaitamani kuiona ccm machoni mwao ni wanakamilisha kiapo tu!

Tuombeane uzima na tuone hawa mafisadi watakavyohanya kukimbia Nchi bila hata ya kuambiwa!

Haki lazima itasimama tu!
 
Last edited by a moderator:
Hili ni dogo sana, inakera pale wapuuzi wanaiba kura halafu baadaye wanatutesa
 
Basi na sisi CDM tuache kuchukua vihela vidogo vidogo tunavyopewa kwenye Kamati za Bunge, km. Kamati ya Siasa na Katiba. Ushahidi ipo. Aibu, mbunge mzima unajivunjia hadhi kwa vihela vidogo. Mlini-bore!
 
Wabongo kwa kutoa hisia mtandaoni mmeshinda, mtu akisoma anaweza kukimbia nchi. Lakini ikifika kwenye matendo sasa hapo ndio mnanifurahisha.hizi ni kelele za JF, hamna uwezo wa kufanya lolote hata mkiibiwa kura. CCM itawatawala milele na mtaendelea kulialia humu jf milele, mkizeeka watakuja watoto wenu na kuendeleza kulialia. Hii ndio hulka ya cdm.
 
Pamoja sana mkuu!
Kwa mfano hii ishu ya Rwakatale cha ajabu nikwamba, CCM inawapa presha mno kuliko faraja....yaani hawana amani kasia!
 
Kweli ushindi kwa Chadema ni dhairi, kwa sasa magamba watumia mbinu zao za mwisho za kung'ang'ania madarakani.
 
Yericko Nyerere anasema hivi..."Huu ni wakati mwafaka kwa wanachadema kutulia na kuonyesha mshikamano wetu, propaganda za ccm zisitunyime usingizi kwakuwa nasi ni wataamu wa propaganda tena za kisasa. Tujipange na kisha tuwakabili kwa propaganda murua na za kisomi bila kuvunja katiba ya nchi wala sheria za nchi.



Chadema iandae vijana wasomi wazuri kisha iwapeleke kwenye wizara zote nchini, wanaweza kupeleka kila wizara vijana 5 tu, hao kazi yao kuu iwe kufichua maovu na matatizo yaliyokwenye wizara hizo, vilevile waweze kupendekeza nini chakufanya ili kuondoa matatizo hayo.

MFAN0: Timu ya vijana hao iyafichue matatizo yaliyo kwenye Elimu, Uchumi, Afya, Ulinzi, Maji,Chakula, Nishati, Miundombinu na kisha viongozi wa Kitaifa waende katika majukwaa ya kiisiasa na waatangazie wananchi hali ya sekta hizo nchini na hatua za haraka za kuchukua. Tukifanya hayo ninaamini ndani ya siku 60 tu CCM itaangushwa na umma wa Watanzania"

*********************************************************************************

kwenye red: kumbe ninyi na CCM mnashindana propaganda? duh nilidhan mpo busy kufikiria njia za kujenga nchi? so propaganda zipi mlisha wafanyia CCM so far,zinalingana na hii waliyo wafanyia kwa Lwakatare na Kibanda? nimestuka sana.

kwenye blue:CDM bana,yaan yawezekana wewe ndo chief strategist wa chama, umekuja hapa JF kupanga mipango...duh? ndo maana wanawazidi kila siku....! why shudn't you conceal your intentions? so by pre emptying like this unafikiri utawashinda ndani ya siku hizo 60? kama chama ndo kina watu wa dizaini hii.. a long way to go,and even impossible,other wise ziwe rhetorics tu.
asante.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom