WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

WanaCHADEMA tulieni Ushindi umekaribia!!!

Wabongo kwa kutoa hisia mtandaoni mmeshinda, mtu akisoma anaweza kukimbia nchi. Lakini ikifika kwenye matendo sasa hapo ndio mnanifurahisha.hizi ni kelele za JF, hamna uwezo wa kufanya lolote hata mkiibiwa kura. CCM itawatawala milele na mtaendelea kulialia humu jf milele, mkizeeka watakuja watoto wenu na kuendeleza kulialia. Hii ndio hulka ya cdm.
Hapa umemaanisha nini mkuu?
Kwamba unafurahishwa na wizi wa kura hapohapo unachukizwa na CDM kutochukua hatua?
Kama unataka mfano wa vitendo subiri mei 25, Mbowe atakapoisimamisha nchi.
 
Binadamu tuna hulka moja ambayo ni KUTAMANI, tunatamani kitu ambacho hatuna, na katika kufanya hivyo, tunafikia kiasi cha kudhani kama tunaweza tukapata hata zaidi ya hicho na fikra hujaza mioyo yetu kama kuna siku tutakipata kile tunachokitamani.

Matumaini yanapogeuka kuwa faraja, ndipo hapo unapoanza kukumbana na matamko kama haya. HOPING FOR THE BEST badala ya kujazwa BURNING DESIRE.

Baadhi ya wanaCHADEMA wanapokaa na kuanza kujipa matumaini kama CCM imechokwa na wananchi bila hata kuwepo na research mbadala kubainisha angalizo lao, ni kujipa matumaini yenye faraja and hope for the best.

Mwindaji mzuri ni yule asiye piga kelele na wakati mwingine kelele nyingi mara nyingi huwa hazina kishindo.
 
sisiem hawajui siku zao za kukaa magogoni mwisho ni 2015

Wanajua na wanaogopa inaweza hata isifike hiyo 2015,wamejawa hofu wamechang'anyikiwa ndo sababu wanafanya mambo ya ajabu na hata ahadi walizotuahidi hawakumbuki tena.,C tumeona No 1 wa nchi bado anaita vikao kwa ahadi yake ya 2005 "SHIDA YA MAJI ITAKUWA HISTORIA DAR ES SALAAM"???Maskini wanatia huruma ni wakuombea hawa.
 
Yericko Nyerere anasema hivi..."Huu ni wakati mwafaka kwa wanachadema kutulia na kuonyesha mshikamano wetu, propaganda za ccm zisitunyime usingizi kwakuwa nasi ni wataamu wa propaganda tena za kisasa. Tujipange na kisha tuwakabili kwa propaganda murua na za kisomi bila kuvunja katiba ya nchi wala sheria za nchi.



Chadema iandae vijana wasomi wazuri kisha iwapeleke kwenye wizara zote nchini, wanaweza kupeleka kila wizara vijana 5 tu, hao kazi yao kuu iwe kufichua maovu na matatizo yaliyokwenye wizara hizo, vilevile waweze kupendekeza nini chakufanya ili kuondoa matatizo hayo.

MFAN0: Timu ya vijana hao iyafichue matatizo yaliyo kwenye Elimu, Uchumi, Afya, Ulinzi, Maji,Chakula, Nishati, Miundombinu na kisha viongozi wa Kitaifa waende katika majukwaa ya kiisiasa na waatangazie wananchi hali ya sekta hizo nchini na hatua za haraka za kuchukua. Tukifanya hayo ninaamini ndani ya siku 60 tu CCM itaangushwa na umma wa Watanzania"

*********************************************************************************

kwenye red: kumbe ninyi na CCM mnashindana propaganda? duh nilidhan mpo busy kufikiria njia za kujenga nchi? so propaganda zipi mlisha wafanyia CCM so far,zinalingana na hii waliyo wafanyia kwa Lwakatare na Kibanda? nimestuka sana.

kwenye blue:CDM bana,yaan yawezekana wewe ndo chief strategist wa chama, umekuja hapa JF kupanga mipango...duh? ndo maana wanawazidi kila siku....! why shudn't you conceal your intentions? so by pre emptying like this unafikiri utawashinda ndani ya siku hizo 60? kama chama ndo kina watu wa dizaini hii.. a long way to go,and even impossible,other wise ziwe rhetorics tu.
asante.
Soma vizuri maandiko yangu hapo juu nilivyoanza na kumaliza,

Siasa nimchezo mzuri sana hasa ukijua kuucheza, lakini kwa watwana ni ghadhabu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa kitengo iko hakina nia njema kinaendeshwa kwa siri.Lakini mungu mkubwa hawa maharamia wa nchi kavu watajulikana tu.
Veve bana bongo ako anyooka thawa veve???Haramia hatari kwako na taifa lako ni yupi kati ya wapora raslimali za taifa na warusha thread hapa jf????Pls,pls!!!DON'T PULL OUR NATION DOWN.
 
CDM tumetulia tu,tunasubiri 2015 tuyapukutishe magamba
 
Yeriko, napendekeza m4C ianze kampeni mkoani Kagera KWAMBA LWAKATARE ASIPOACHIWA HURU NDANI YA SIKU 7 MKOA WA KAGERA UTAJITENGA NA KUJITANGAZA JAMHURI HURU.

Na hivyo hivyo kwa mkoa wa mtwara - kama serikali inafanya ushenzi huu basi wananchi wajitangazie jamhuri huru.
 
Veve bana bongo ako anyooka thawa veve???Haramia hatari kwako na taifa lako ni yupi kati ya wapora raslimali za taifa na warusha thread hapa jf????Pls,pls!!!DON'T PULL OUR NATION DOWN.
Msamehe hajui atendalo, anahitaji msaada waukombozi kifikra.
 
Yeriko, napendekeza m4C ianze kampeni mkoani Kagera KWAMBA LWAKATARE ASIPOACHIWA HURU NDANI YA SIKU 7 MKOA WA KAGERA UTAJITENGA NA KUJITANGAZA JAMHURI HURU.

Na hivyo hivyo kwa mkoa wa mtwara - kama serikali inafanya ushenzi huu basi wananchi wajitangazie jamhuri huru.
Tunataka ukombozi wa jamhuri yote ya Tanzania, hakuna kipande cha ardhi kitakachojitenga kudai uhuru,

Kujaribu kutumia njia hii kutaligawa taifa na kuruhusu maadui wetu yani nchi jirani zianze kuyavamia maeneo yetu hasa yale yanayotagaza kujitenga,

Hivyo tutatumia njia zile ambazo haziligawi taifa letu, kwaumoja wetu na wingingi wetu ndio silahapekee ya ushindi.
 
Kwa kuwa kitengo iko hakina nia njema kinaendeshwa kwa siri.Lakini mungu mkubwa hawa maharamia wa nchi kavu watajulikana tu.
Najua fika kuwa mashushu wa magamba wangewajua wengine wetu humu wangetu- Ulimboka au ktu- Kibanda lakini kama Mungu alivyokuwa pamoja na Ulimboka pamoja na Kibanda ndivyo alivyo pamoja nasi. Walidhani wamammaliza Ulimboka na Kibanda lakini Mwenyezi Mungu mkubwa. Hatutanyamaza. Tutaendelea kuhamasisha umma hadi ukombozi halisi ufike!
 
Mbona chemba,nepi na wanaofanana hawajaitolea ufafanuzi kesi ya lwakatare? binafsi inanishangaza bora riziwan aliibukia fb na kulonga japokuwa alidai ni hackers. ila magamba nayaamini hata akichukuliwa mkeo na gamba jenzio haushtaki kutetea ugamba. kikwetu tunasemba,gamba kwanza unyumba baadae. teh teh teh...
 
wakati Magamba na wenzio wanapanga njama nyingi dhidi ya CDM, ndipo CDM itakapoibuka kama dhahabu safi , baada ya mapigo yote haya na kuwajua wabaya , takataka na makapi.
 
Back
Top Bottom