Mutakyamirwa
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 4,942
- 1,360
Ni wakati wakutiana moyo, ni wakati wa kusonga mbele kwa kasi.
Hali ya siasa nchini ipo katika kipimo cha Def Cond 003, hii inamaana kuwa tungelitazama katika mizani ya hali ya Taifa, rais angelishatangaza hali ya hatari isiyozidi wala kupungua siku 28 kwamjibu wa katiba ya nchi hii.
Siasa ni mchezo mzuri sana, hakika kwa waamini wa siasa hufarijika wakiwa katika ulingo wa siasa hasa siasa safi, ninatamani sana kuiona Tanzania ikiishi katika siasa safi na ikitumia raslimali watu katika siasa hizo bila tone la damu lakini tamaa yangu inajaribiwa na siasa msonge na za kiimla za wanasiasa wetu nchini.
Kuendesha siasa Afrika ni ngumu, tena ni ngumu kuliko kujitwisha gunia la misumari, ndio ni ngumu kwakuwa vyombo vya dola ambavyo vipo kwamjibu wa katiba na sheria na ambavyo uwepo wake hutokana na kodi za wananchi wa vyama vyote hugeuko vitengo mhimu vya chama kilicho madarakani,
Moja ya mapungufu yaliyomo kwenye sheria zilizozaa vyombo vyetu vya dola ni pale sheria inaposisitiza kuwa ni lazima vyombo hivyo VIAPE kuwa VITAILINDA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI kwa utii na uaminifu.
Hili nimelieleza ili wale wenzangu wanaolalamika kuwa Polisi,TISS, JWTZ nk wanaisaidia CCM, Ukweli ni kuwa wanatimiza kazi yao kwamjibu wa sheria iliyoviunda vyombo hivyo (Invisible Act)
Chama kikuu cha upinzani nchini Chadema kimepita mapito mengi na magumu sana kuanzia mwaka 2005 mpaka hii leo, na majaribu yote yalilenga dhidi ya kifo kamili kwa Chadema, lakini Mungu alivyo si mnafiki chama kiliyashinda majaribu yote hata yale ya alama za damu.
Mwaka 2010 chama kilipata jaribu kuu ambalo kama si umahiri wa Mwenyekiti na timu yake ni dhahiri kuwa leo kingekuwa ni historia tu ya vyama vilivyowahi kuwepo Tanzania, hii ilitokana na KUPORWA ushindi wa uchaguzi wa URAIS na kufuatia wabunge wake kufunguliwa kesi zaidi ya 24 za kupinga matokeo ya uchaguzi wao.
Hayo yote yalitokea chini ya uratibu wa chama tawala kikitumia vyombo vyake vya dola ambavyo mimi wewe na wale tunavilipia kodi zetu.
Matukio yamauaji na utekaji yanayofanywa na CCM kwakutumia vyombo vya dola ambavyo kikatiba na kisheria ni vyauma na kisha kujaribu kuyageuza kuwa ni CHADEMA, ni dalili tosha na ya mwisho kwakuukaribia ushindi na ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi CCM ambae kwa hakika ni mbaya kuliko mkoloni mweupe wa leo.
Huu ni wakati mwafaka kwa wanachadema kutulia na kuonyesha mshikamano wetu, propaganda za ccm zisitunyime usingizi kwakuwa nasi ni wataamu wa propaganda tena za kisasa. Tujipange na kisha tuwakabili kwa propaganda murua na za kisomi bila kuvunja katiba ya nchi wala sheria za nchi.
Katika kipindi hiki ambacho mfumo wa chama unafanya kazi usiku na mchana kuwakabili maadui zetu wa NDANI na nje, ndicho kipindi mwafaka kwetu kukabiliana na propaganda za kitoto za vijana ngumbalo wa ccm waliojazana humu mitandaoni wakijaribu kuganga njaa kwakueneza uongo na uzushi dhidi ya CHADEMA.
Ninawahakikishia kuwa Chadema imezishinda hila zote za CCM za kuifarakanisha na umma, na sasa wanaweweseka tu,
Madiwani wasaliti tuliwapiga chini bila kuangalia sura zao, Masali Tumewapiga chini bila kuangalia sura zao, na sasa VIdeo yao ya Lwakatare imewafia mikononi sasa wanahaha pakutokea hawajui hata sababu yakumshitaki huyo Lwakatare,
Wakati ccm wao wapo bize na Video, Wanachadema tulieni tujikite kwenye ishu zinazowahusu wananchi moja kwa moja, fichueni ubadhirifu, rushwa, na matattizo ya kila sekta nchini,
Chadema iandae vijana wasomi wazuri kisha iwapeleke kwenye wizara zote nchini, wanaweza kupeleka kila wizara vijana 5 tu, hao kazi yao kuu iwe kufichua maovu na matatizo yaliyokwenye wizara hizo, vilevile waweze kupendekeza nini chakufanya ili kuondoa matatizo hayo.
MFAN0: Timu ya vijana hao iyafichue matatizo yaliyo kwenye Elimu, Uchumi, Afya, Ulinzi, Maji,Chakula, Nishati, Miundombinu na kisha viongozi wa Kitaifa waende katika majukwaa ya kiisiasa na waatangazie wananchi hali ya sekta hizo nchini na hatua za haraka za kuchukua. Tukifanya hayo ninaamini ndani ya siku 60 tu CCM itaangushwa na umma wa Watanzania.
PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZZZZZ!!!!! ...................................!!!!
mkombozi wa kuteka na kupanga ugaidi kama al shabab
Mmeshawakabidhi kwa polisi wale wanaong'oa wenzao kucha na macho pasipo kutumia ganzi? Na wale wanaorushia wenzao vitu vyenye ncha kali? Ama kweli safari hii mmeamua kuruka sarakasi na TAULO sebuleni.
Yeriko, napendekeza m4C ianze kampeni mkoani Kagera KWAMBA LWAKATARE ASIPOACHIWA HURU NDANI YA SIKU 7 MKOA WA KAGERA UTAJITENGA NA KUJITANGAZA JAMHURI HURU.
Na hivyo hivyo kwa mkoa wa mtwara - kama serikali inafanya ushenzi huu basi wananchi wajitangazie jamhuri huru.
sisiem hawajui siku zao za kukaa magogoni mwisho ni 2015
Mkuu, hilo siyo swali.Very funny !!!
Mtu afanye ugaidi halafu muandamane eti aachiwe au mlikuwa nae?
Tatizo la chadema siku zote ni kuendesha siasa za kitoto na hamko strategic kabisa..Sasa hao vijana wa kwenda kila wizara mnawatuma kama waajiriwa au kwenda kuiba siri za serikali ili ziletwe chamani na kutoa siri hizo kwa umma kupitia viongozi wenu..Kama mchezo wenyewe ndo huu mnawafundisha nini wapinzani wenu wa kiasiasa mkichukua nao waende kila ofisi ili kuiba nyaraka za serikali ili iweje na kwa manufaa ya nani..Mwisho nakumbuka ile mada yako kuwa Katika siasa za kenya nyie chadema mko na Odinga na ukalazimisha Kenyatta ni kama CCM,,,HEBU TUPE MATOKEO Yercko Nyerere ni nani alishinda kati ya Odinga wa CDM na Kenyatta wa CCM..kuwenu makini sana na aina ya siasa mnazozifanya.
Tatizo la chadema siku zote ni kuendesha siasa za kitoto na hamko strategic kabisa..Sasa hao vijana wa kwenda kila wizara mnawatuma kama waajiriwa au kwenda kuiba siri za serikali ili ziletwe chamani na kutoa siri hizo kwa umma kupitia viongozi wenu..Kama mchezo wenyewe ndo huu mnawafundisha nini wapinzani wenu wa kiasiasa mkichukua nao waende kila ofisi ili kuiba nyaraka za serikali ili iweje na kwa manufaa ya nani..Mwisho nakumbuka ile mada yako kuwa Katika siasa za kenya nyie chadema mko na Odinga na ukalazimisha Kenyatta ni kama CCM,,,HEBU TUPE MATOKEO Yercko Nyerere ni nani alishinda kati ya Odinga wa CDM na Kenyatta wa CCM..kuwenu makini sana na aina ya siasa mnazozifanya.
Very funny !!!
Mtu afanye ugaidi halafu muandamane eti aachiwe au mlikuwa nae?