WanaCCM 8 waliopitishwa kugombea Ubunge wa EALA

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimewapitisha wanachama nane kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA) utakaofanyika Septemba 22, mwaka huu.

Akitangaza majina ya makada wa CCM waliopitishwa na Kamati ya Wabunge wa CCM leo, Msimamizi wa Uchaguzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amewataja waliochaguliwa kuwa ni Nadra Juma Mohamed, Dk.Abdulla Hasnuu Makame, Machano Ali Machono.

Wengine ni Angela Kizigha, Dk.Shogo Mlozi, James Ole Millya, Dk.Ng’waru Maghembe na Anar Kachambwa. Amesema wanachama 179 walijitokeza kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo ambapo Kamati Kuu ya CCM baada ya kufanyika mchujo ilitoa majina 26 ambayo yamepigiwa kura wa wabunge ili kupata wanachama nane.

“Kwenye mchujo kuna mambo mengi kuna taarifa za upekuzi za kawaida, kwa maana ya sifa watu walikuwa na sifa tunatikisana sana kutoka 179 tukaja na watu 26 ambao leo wamejitokeza kujieleza, Tanzania kwa upande wetu kwenye chama tuna nafasi nane na moja ni kwa ajili ya upinzani,”amesema.

Uchaguzi wa wajumbe tisa watakoiwakilisha Tanzania EALA utafanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake utakaoanza Septemba 13, mwaka huu.
 
Back
Top Bottom