Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,608
- 860,789
Ni pambazuko la siku nyingine tena... Wengi mko vitandani mwenyu mkimalizia usingizi mnono na ndoto anuwai... Wengine tuko zamu...
Neno SALAMA si geni masikioni mwetu ni neno la kawaida na lililozoeleka mno... Nakumbuka pia nikiwa shule ya msingi nilisoma na binti mmoja mshihiri aliitwa SALAMA... Alikuwa mzuri, mtulivu, mpole na mwenye haiba ya kuvutia mno.....
SALAMA ni neno la kheri linaloakisi ulinzi, amani na usalama.... Wakristo kuna wimbo huwa wanaimba unaitwa NI SALAMA ROHONI MWANGU... Taasisi za kifedha kwenye mabenki hutujamasisha kuweka pesa zetu benki kwakuwa ni sehemu SALAMA...! Mifano ni mingi kiimani na kidunia pia... Hata kwenye ushirikina huwa tunawatengenezea watu kinga ili wawe SALAMA...!!!
Kwenye usalama kuna kinga... Ndio maana hata mtoto mdogo hukimbilia kwa mzazi wake anapohisi hatari kwakuwa akiwa kwa mzazi wake hujihisi SALAMA.. Kwamba yuko mahali SALAMA kwenye mikono SALAMA
Kwahiyo ili usalama uwepo popote ni lazima kuwepo na vitendea kazi, vifaa kinga na nguvu kazi yenye taaluma na ujuzi wa USALAMA...
Watu wenye ujuzi na hii kaliba ya USALAMA hujulikana kama WANA USALAMA.
Mwana usalama halisi hana alama, hana mavazi rasmi, hajioneshi wala kujitangaza... hawa pekee ndio huweza kukuchukua kwenye mikono SALAMA na kukupeleka sehemu SALAMA.... Sehemu salama ni sehemu yenye kinga zote muhimu.. Hivyo basi ni sehemu isiyojulikana na wasiohusika...
Si mara chache tumesoma na kusikia ama kutangaziwa kuwa watu wasiwe na wasiwasi kwakuwa fulani yuko kwenye mikono SALAMA, sehemu SALAMA... Hii ni assurance kubwa ya kuwatoa watu hofu....
Katika maisha yangu ya kuzunguka hapa na pale duniani mpaka nchi ya wagagagigikoko nimeshuhudia mara nyingi tu watu waliochukuliwa na mikono SALAMA na kupelekwa sehemu SALAMA
Kuna ambao hawakurudi na hawajawahi kuonekana tena...!
Kuna ambao walirudi lakini wakiwa hoi nyang'anyang'a
Kuna ambao waliokotwa wakiwa mahututi kwa kibano na vitasa vya uhakika
Kuna ambao walikutwa wametupwa mahali wakiwa kwenye kilevi cha dozi kali isiyojulikana
Kuna ambao walipatikana wakiwa tayari ni marehemu
Nimetafakari kwa kina nikiwa hapa chumba cha wafu dhima ya Mwana usalama, mikono SALAMA na sehemu SALAMA... Sijawahi kuona mtu kaenda huko na kurudi kakenua meno kwa furaha.
Sijawahi kuona aliyebahatika kurudi halafu akasimulia kwa hakika nini alikutana nacho.
Bali nilichoshuhudia ni majeraha na macho yaliyojaa kihoro na jinamizi la kutisha..... Baada ya kutafakari haya nimejikuta.
Nawaogopa wana usalama
Naiogopa mikono salama
Napaogopa mahali salama....!!!
LAKINI SIPINGANI NAO WALA KUPINGA UWEPO WAO... kwakuwa napenda pia USALAMA na kuwa SALAMA... Salimini
Good morning, Africa....!!!