Usijitoe Kwenye Usalama Wako

Usijitoe Kwenye Usalama Wako

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,204
Reaction score
1,694
Yn 10:28-29 SUV
[28] Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. [29] Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.

Ukisikia mtu yupo mikono salama bila shaka unapata picha ya uhakika mtu huyo analindwa na yupo kwenye ulinzi wa uhakika, na hakuna kitakachomdhuru katika maisha yake.

Mtu akikuambia mtoto wako yupo mikono salama, kama ulikuwa na wasiwasi juu ya jambo fulani unapata utulivu wa ndani na kukaa vizuri.

Walio ndani ya Yesu wapo salama, adui hawezi kuwafanya chochote, haya sio maneno matupu au ya hewani, huu ni ukweli ulio wazi kabisa.

Unaweza kujiuliza inakuwaje mtu anasema ameokoka au yupo ndani ya Yesu na anasumbuliwa na Shetani?

Huyu mtu anaweza akawa hana neno la Mungu, anakuwa amejaa hofu, wasiwasi au mashaka mengi, anateswa hayo na hayo. Na wakati mwingine Mungu huruhusu amtese kwa mapenzi yake mwenyewe.

Wengine wanasema wapo ndani ya Yesu, au wanasema wameokoka, au wanafanya na huduma kabisa, ila kwa upande mwingine wanafanya mambo yanayomchukiza Mungu, na kumfurahisha Shetani.

Roho Mtakatifu hakai kwenye mchanganyo alionao mwamini, anapokaa pembeni Shetani anapata nafasi ya kutosha kumtumikisha huyo mtu anavyotaka.

Adui Shetani amekuja mara nyingi kwenye maisha ya wana wa Mungu, ila hakuweza kuwadhuru kutokana na ulinzi walionao kutoka kwa Baba yao wa mbinguni.

Nkuhakikishie unao usalama wa kutosha ndani ya Yesu Kristo, unaweza kupinga kutokana mafundisho uliyonayo ila ukweli hutobadilishwa na mtazamo ulionao juu ya Yesu.

Usijitoe kwenye mikono salama ya Yesu, upo salama, na unayo ahadi ya uzima wa milele baada ya maisha haya hapa duniani.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom