Wana Simba SC wenzangu acheni Kununua Magazeti ya Mwanaspoti, Tanzania Daima na Nipashe kwani yana Upendeleo kwa Yanga SC

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Haya Magazeti siku Yanga ikifungwa hayaandiki kwa Ukubwa wake na tena unaweza hata Habari ya Yanga SC Kufungwa usiikute au ukaikuta katika Kurasa za ndani ila Siku tu Simba SC ikifungwa utaona wanaipa Habari hiyo Umuhimu mkubwa katika Kurasa za mbele huku wakiikoleza kabisa.

Tumechoka na aina hiii ya Unafiki na leo hii nawaombeni wana Simba SC wenzangu wote kuwa hakuna Kununua tena Magazeti ya Kiunazi ( yanayoipendelea Yanga SC ) ya Mwanaspoti, Tanzania Daima na Nipashe hadi pale yatakapojirekebisha na iwe Fundisho kwa Magazeti mengine na Waandishi wa Habari wengine.

Jana Yanga SC imefungwa tena huku Goli lingine Mwamuzi Saanya akiliweka Kwapani mwake halafu leo Vichwa vya haya Magazeti wamendiika nanukuu..." Yanga SC ndiyo kama mlivyosikia " huku lingine likiweka tu Picha ya Goli 1 la Ruvu na 0 la Yanga na lingine halijaiweka kabisa mbele hiyo Habari huku wakiwa wameipa Kipaumbe kidogo sana.

Sasa subiria Magazeti haya kama Simba SC leo nayo itafungwa uone watakavyoandika Vichwa vyao vya Habari vibaya na vya Kuikandamiza Simba SC Kesho. Na walivyo Wanafiki hata pale tu Simba SC ikitoka Sare bali Vichwa vyao vya Habari vinakuwa ni vya Kuidhihaki Simba SC kwa gharama ya Kuipendelea Yanga SC.

Tumewachokeni sasa na sasa nasi wana Simba SC tutawakomoeni kwa namna hii ya Kiuchumi kama siyo Kimapato ili mkome.
 
Mengine hayo sijawahi nunua ila mwanaspot ni wanazi wakubwa wa Yanga na huwa sinunui siku hizi. Mwanaspot nawapa volume 1 kwa uzi huu. Bora ununue gazeti la Jangwani kuliko mwanaspot kama unataka habari za Simba. Na bora freebasics wameondolewa.
 
na kuongezea wakiiandika kwa ubaya yanga imefungwa magazeti hayanunuliwi, lakini simba ikifungwa magazeti yananunuliwa mno na wananchi
 
Kama ulikuwa hujui sasa sikia hii: Magazeti ni business. ni suala la biashara....Yanga ndio wanunuzi wakubwa wa magazeti...Ikifungwa Yanga magazeti hudoda...ukiiandika vibaya Yanga magazeti hayanunuliki
 
Hii Reseach yako ya Kipumbavu kama ulivyo Mpumbavu juu ya huu Upumbavu wako uliouwasilisha hapa uliufanyia wapi na lini?

Huwa unaangalia kipindi cha Kurasa za mwisho cha Azam tv siku za Jumamosi ambapo huwaalika wahariri mbalimbali wa mgazeti ya michezo kufanya uchambuzi?

Hao wahariri ndiyo wanaosema ya kwamba mashabiki wanaonunua magazeti kwa wingi ni wale wa Yanga! huku wenzangu wa Simba wakiishia tu kusoma vichwa vya habari. Nimeona nikujibu kwa niaba ya huyo mdau uliyemtolea mapovu.
 
Mleta mada, hivi ulikuwa hujui kuwa Yanga ni timu ta magazetini? Hata hivyo hatununui magazeti kwa ajili ya Yanga.

Vv
 
Yanga ni timu ya wananchi, inapendwa na wazalendo, watanzania wengi wanapenda habari zake ziwe nzuri na za kuvutia, tofauti na simba ambayo habari zake hazina mvuto kwa jamii na wananchi kwa ujumla
Sio simba ni Simba alafu mbona mimi sizipendi hizo habari za litimu lako ina maana mimi sio mwananchi?
 
Cleverbright, magazeti yapo kibiashara zaidi licha ya kuhabarisha,,hivyo ukiona habari za watani zetu zikiandikwa kwa mapambio zaidi maana yake mashabiki wao ndio wanunuzi zaidi kuliko sisi wanamsimbazi.

Hii pia nilishaisikia kwenye kipindi cha wahariri wa magazeti ya michezo kikirushwa na Azam Tv siku za weekend, wanasema Yanga akifungwa magazeti hayauzi lakini siku akishinda biashara huwa nono.
Habari ya Yanga kuwa bingwa tpl itauza zaidi magazetini kuliko ya Simba kuwa bingwa CAF-CL
 
Kama simba itakuwa inashinda vizuri mechi zake, wakiipendelea yanga watakuwa wamepunguza nini.?
 
Mengine hayo sijawahi nunua ila mwanaspot ni wanazi wakubwa wa Yanga na huwa sinunui siku hizi. Mwanaspot nawapa volume 1 kwa uzi huu. Bora ununue gazeti la Jangwani kuliko mwanaspot kama unataka habari za Simba. Na bora freebasics wameondolewa.
halaf hilo gazeti hivi ni lazma ukurasa wa kwanza uwe na habari ya simba na yanga?
 
Brother sisi simba sio watu wa magazeti hilo liko wazi kabisa.. yanga wananunua sana magazeti sanasana timu yao ikifanya vizuri..washabiki wa simba wengi akili zao ni advanced huwa wanasoma habari zaidi kupitia internet na sio magazetini na ndo maana tuna Simba app ambayo yanga hawana. ndala huwa wananunua sana gazeti simba ikifungwa au gongo wazi ikishinda lakini washabiki wa simba wengi wameidharau yanga na wala hawafuatilii habari zake kama yanga wanavyofuatilia za simba.. hata hivyo mikaratasi ya nini brother?? tembelea simba app upate habari motomoto
 
Back
Top Bottom