Future Bishop
Member
- Dec 4, 2009
- 75
- 15
Golder , jua kwamba hakuna kanuni katika jambo hili na wala hakuna kitu kinachoitwa ratiba inayoweza kuwa sawa kwa wote. Hili ni suala la mme na mke kukubaliana lakini pia linategemea hamu ya kila mmoja. Hata kula chakula cha kawaida, japo tunajipangia kula angalau mara tatu kwa siku asubuhi, mchana na jioni naamini kuwa ukijisikia hamu ya kula muda wowote na uwezo upo unakula. Na wakati mwingine ni kuwa mchana au jioni pamoja na kuwa ni ratiba ya kula chakula, unaweza usile chakula kwa kuwa husikii hamu ya kula. Ndivyo ilivyo kwenye ndoa kwamba itategema hamu ya mmojawapo au wote kwa pamoja; mkijisikia kufurahishana kila siku hakuna atakayewaingilia ilimradi mmepatana na kila mmoja anamfurahia mwenzake. Kinachotakiwa kwenye ndoa ni kuchukuliana na kusindikizana, usimlazimishe mwenzako kama hajafikia hatua ya kujisikia na ni wajibu wako wewe unayejisikia kutengeneza mazingira ya mwenzako kujisikia ili furaha iwe kwa wote.