Wana-MMU NAOMBA MNIPOKEEE TAFADHALI...MIE NI MGENI

Wana-MMU NAOMBA MNIPOKEEE TAFADHALI...MIE NI MGENI

Kisaka80

Senior Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
151
Reaction score
94
Wapendwa wana MMU,

Kwanza poleni na Majukumu yenu mazito ya kila siku, na pia Hongereni kwa kudumisha upendo hapa jukwaani. Mungu azidi kuwapa nguvu na kuzidi kupendana zaidi katika shida na raha pia.

Back to the topic,

Wapendwa wangu..mimi ni mtanzania lakini siifahamu vizuri Tz zaidi tu ya kusoma baadhi maeneo katika ramani na kuangalia katika TV. Sasa nimeona ni vema nizunguke katika baadhi ya maeneo ili angalau niwe na idea ya kuifahamu vizuri nchi yangu. Nataka nianzie safari yangu DSM hadi Moshi..nikae wiki moja, niende Hai..siku 3, Niingie A-town, Manyara (Babati)...nitokee Singida...kisha nitue tena DSM.

Maeneo hayo yote sijawahi fika hata siku moja. Hivyo nawaomba Ndugu zangu wana MMU mlioko huko MNIPOKEE...TAFADHALI..!

Mnipokee katika maana ya kunitajia....Lodge/Guest House ambazo ni standard, zimetulia na pia ni affordable kwa maisha ya mtanzania wa kawaida. Ukiweza kutupia na bei per one night sleep itakuwa ni nzuri zaidi na itanisaidia kujipanga vema.

WANA - MMU WA MAENEO HAYA:
1.Moshi...mjini
2.Hai.../Boma ng'ombe...
3.Arusha..mjini
4.Babati...
5.Singida mjini...

NB:-Unaponishauri hiyo lodge/Guest House pia zingatia na usalama...wa kutosha.

Mwisho natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wapendwa wote.

Wana-MMU wa maeneo tajwa hapo juu NAOMBA MNIPOKEEEE.....MIMI NI MGENI...!
 
Ngoja wazoefu waje ila jiandae pia kupokelewa na bebiz za kichaga huko moshi lol kila lakheri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom