Wana JF tumwambie Rais Magufuli kwa kauli moja, amfukuze kazi Waitara

Waangalie mawaziri kama lugola, mpina, kigwangala na ata waziri Mpya wa viwanda. Utagundua wana Sifa moja kubwa. Uwezo wa akili unafanana sna.
 
Mkuu alisema wale wanaongea sana bungeni siwateui ng'o, wanatakiwa mazombi kuteuliwa hawezi kuteua wanaojielewa.
 
"Msaliti hawezi kuachwa hivi hivi akisavaivu" (Magu, 2017). Kesho yake kilichotokea pale Dodoma "Area D" wote ni mashahidi. Huyu ndiye wakumshitaki kwa mahakama na kwa Mungu. Waitara cha mtoto. Hana hata asiyejulikana mmoja wa kumlinda.
 
hii post mbona Kama ya yule mwandishi wa gazeti la jamvi la habari
 
Labda wangekufukuza wewe kwanza huko ulipo then tutafikiria upya..jambo lisilokuwa na ushahidi wa kimahakama unalitamkaje hapa..we vip bana. Acha wivu wa kitoto wacha achape kazi...najua issue ni uwaziri wake...bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
Wewe kweli ni "Babeli" Tuambie ni Babeli ile ya kale au ni huyu Mama wa Makahaba!!!?
Hoja Ni kuwa Waitara Ni kiongozi, tena Waziri ambaye ofisi yake iko chini ya Ikulu. Tunahitaji ushahidi gani wakati hajakanusha kuwa siyo yeye anayetoa povu kwenye clip inayozunguka. Hakuna Cha wivu, hatuwezi kuacha kuwakemea viongozi walevi na kuwaacha watekeleze nia zao ovu dhidi ya Watanzania.
Unapaswa kujua kuwa kule Ujerumani Hitler hakuwa peke yake. Walikuwepo akina Goering waliotenda ukatili hata kuliko Hitler mwenyewe. Hivyo basi tuungane kusema kwa sauti: Waitara must Go!!!
 
"Give them enough rope to hang themselves " Tuwaambie ili wajue kuwa wapo watu ambao hawakubaliani na hiyo kauli. Tumwambie mkuu Waitara must go.
Definitely, Ni wazimu kuwa na kiongozi anayetangaza hadharani tena akiwa mbele za watu kwamba serikali ikikosolewa basi imekwamishwa!!! Haya kama si mawazo ya enzi za ujima nini hasa.
Mhe. Rais, wewe ni Rais wa nchi yetu, umeapa kuwalinda Watanzania wote bila kujali ni wazima, wagonjwa, vilema au hata vichaa. Kwa Katiba na sheria zetu ni Mahakama tu plus saini yako ndivyo vinaweza "kumtanguliza" mtu aliyefanya makosa hata ya uhaini.Sasa Waitara Ni nani hata atamke kutanguliza watu. Hivyo Mhe Rais timiza wajibu wako, mfukuze Waitara serikalini. Waitara must Go!!!
 
HAHAHAAAAAAAAAAAAAA......MANENO MAZITO SANA HAYA PASKALI KHAAAAA!!!
 
Yeye huwa hapangiwi...
Hapangiwi!!!? Labda na Mabeberu, lakini sisi Wananchi lazima tumpangie. Moja la muhimu la kumpangia ni kumwondoa Waitara ofisini kwake Tena kwa kumfukuza kazi. Haiwezekani Waziri tunayemlipa sisi ale njama ya kutaka "kumtanguliza" Mtanzania mwenzetu kinyume Cha Katiba na Sheria zetu, halafu kiongozi wetu mkuu aliyemteua mtu huyo adai "hapangiwi!!!" Kwa hili atambue kuwa Waitara must Go!!!
 
Iwapo Rais alisema maneno uliyonukuu basi alikosea. Sasa tusimruhusu kutoa matamshi ya aina hiyo, na njia muafaka ni kumwambia wazi kuwa kila . Mtanzania ana haki ya kuishi Hadi mahakama itoe hukumu ya kifo na Rais aidhinishe kwa saini. Si kinyume chake. Rais kwa kujua hatari ya matamshi ya aina hiyo amchukulie Waitara hatua. Amfukuze kazi maana Hakuna namna: Waitara must Go!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…