wana JF nakufa na kipaji changu tafadhali nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wana JF nakufa na kipaji changu tafadhali nisaidieni

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by KAMBOTA, May 31, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe mkoani morogoro niko mwaka wa kwanza nachukua shahada ya production and operation management niliwahi kusoma seminari ya Mtakatifu Maria Visiga kwa O-level na baadaye Ilboru special school kwa A-level , sasa marehemu mama yangu alikuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi za watoto na mimi nikazaliwa na kipaji cha uandishi , nikageuka mtunzi wa vitabu, mashairi n.k , mpaka gazeti la Dira wakanikubali na kwasasa naandikia kwenye gazeti hilo kama mchambuzi upande wa makala za kisiasa na kihistoria. Sasa kinachonichanganya akili ni kuwa licha ya watu kukiri kuwa nina uwezo wa kuandika na kutunga ila bado hawako tayari kunisaidia, huku wakijua gharama za uchapaji ni kubwa mno sitoweza ku-afford, katika purukushani zangu nimefanikiwa kusajili kampuni yangu iitwayo Vijana Intellectual Company mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa tano ila sina pesa za kuchapa vitabu , wengi wa watu wanaojifanya wanasaidia ni wagumu mno na ni matapeli wa mjini, kwasasa nina umri wa miaka 21 ni kijana wa kiume na ni mtanzania pure kabisa . Huwa nafikiria kusubiri labda baadae nitakapokuwa na fedha za kutosha kuchapa lakini hofu yangu ni kuwa kwasasa ndiyo kijana mbichi na nguvu na akili yangu inachemka sana hivyo ni heri nikachakarika kutunga sasa kabla uzee haujaninyemelea, hivyo lengo hasa la kuja hapa jamvini ni kuwa natafuta mtu aliyetayari kunifadhili au kusimamia kazi zangu ili zichapwe na kusambazwa awe mtu mwenye uzoefu na aliyetayari kukuza vipaji vya vijana, awe na maono na mtazamo wa kimaendeleo mimi niko tayari hata kuingia mkataba naye ila cha msingi awe serious na kazi sitaki longolongo au blah blah, kifupi sipendi porojo za kupotezeana muda,naweza kuandika kwa lugha mbili yaani kiingereza na kiswahili kwa ufasaha kabisa bila matatizo yoyote, hivyo tafadhali aliyetayari tuwasiliane tuanze kazi haraka, sipendi kufa na kipaji changu nataka kuacha urithi kwa taifa letu na ulimwengu mzima...ASANTENI SANA
  Contacts zangu ni 0717-709618 au novakambota@gmail.com
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Jaribu kujua gharama za uchapishaji za makampuni ya lndia, wengi wanakimbilia huko kutokana na unafuu wanaoupata
   
 3. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I wish ningekusaidia, ila sina ujuzi wowote na mambo ua uchapishaji wa vitabu, ninachojua ni kusoma tu.
  Hope utapata wafadhili, all the best.
   
 4. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hebu jaribu kufanya mawasiliano na mbunge wa Tarime. Unaweza kupata mawasiliano yake kwenye website ya bunge.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni nikuombee tu mafanikio kwani sina mchango katika hili!
   
 6. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  msaidie pesa za kazi hiyo
   
 7. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  kila la kheri kaka
   
 8. g

  gooner Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iliboru special school ndo ipi hiyo?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  usife na kipaji chako... encourage other kids has wa sekondari kupenda kusoma na kuandika hadithi, soon utakuta umezaa kambota wengine wengi
   
 10. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  dah hongera kaka ila nakushauri km una program madhubuti nenda benki kapate mkopo, au jiunge kwanza na vikundi vya ujasiriamali kuna mikopo ya riba nafuu huko.
   
 11. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ndo wakina ngungi wa thiongo wajao...kaka mi nakushauri umalize chuo kwanza alafu mengine baadaye.unaweza ukazeeka mwili ila siyo akili.kila la kheri
   
 12. PlanckScale

  PlanckScale JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Dogo, kwanza badilisha fikra za kimasikini!

  Kama unakipaji cha utunzi basi kiendeleze...andika story zaidi; fungua blog uandike story za kuvutia; omba kazi kwenye magazeti mengine kwani kazi yako kama ni nzuri wenye magazeti watakulilia...USINGOJE KUSAIDIWA KAMA KIPAJI UNACHO!!

  Kama wengine walivyo sema hapa, tengeneza business plan na cost analysis ya hicho unacho taka kufanya, kisha utakuwa na plan yakukufikisha utakako kufika. Endelea kujielimisha kuongeza kipaji cha pale utakapo kwenda, alafu umaarufu wako utauza kazi zako automatically.

  Kuomba omba msaada unakuwa kama taifa letu; lina natural resources kibao, lakini bado tunaomba misaada:confused2:
   
 13. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Unasema hutaki blah blah, basi investor ndio kabisa hawataki maneno matupu. Huwezi kusema nimeandika vitabu ikatosha, vitabu gani na vinapatikana vipi, hata kama hujachapisha toa maelezo ni vipi utaziwakilisha hizo kazi kwa wale wenye interest. Pia kwa vile hujawa na jina kwenye uandishi usitegmee investor atapoteza muda kwenda Dira kuzisaka kazi zako.

  Wawekezaji mbali na kureview kazi wao wenyewe, wanazipeleka kwa 'wataalamu' - waandishi waliobobea, publishers and printing companies. Hapa hajasaini mkataba wala hajatoa pesa, sana sana analipia gharama za reviews. Vile vile ukumbuke area za investment ziko nyingi na watafutaki kama wewe ni wengi.

  Kwa upande wangu napenda kusoma vitabu na si kuwekeza hivyo nakutakia kila la heri.
   
 14. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa nyambari nyangwine nimepata sana habari zake kutoka kwa walimu maarufu, jamaa ni bonge la mnyonyaji yeye anachokifanya ni kutafuta walimu na kuandika kazi sasa tatizo ni pale kwenye maslahi anakuwa mnyama na pia huwa anawadhulumu kbs hata senti ya jasho lako hupati zaidi ya kuambiwa nimepata hasara kitabu hakiuziki au nilichapa nakala chache wakati ukienda madukani vitabu vyako kibao vipo na vinauzika, halfu huwa anatumia majina yake kwenye hivyo vitabu na si jina lako mtunzi
   
Loading...