Wana filamu kuandamana, kisa Kanumba ka-comediwa!

Mambo Ya Kanumba
Steven Charles Kanumba is my name, i was born in a Christian family of 2 girls and i happen to be the last born and the only boy to Mr. & Mrs. Charles Meshark Kanumba.

Mi naona kizunguzungu hapa....!!! Steven Charles Kanumba Ali-close vipi?? au aliogopa kuuliza menu akaamua kusingizia closing? Halafu siku ile pale ilikuwa usiku saa moja ya CAT, (saa 2 ha huku EAT), sasa yeye alikuwa na mpango wa ku-open muda gani?? (Usiku wa manane)??

Jamani, lazima tukubali kuwa mtu anapokataa kukosolewa basi ana mtindio wa ubongo au amefilisika kimawazo!! Nobody is perfect, cha kufanya ni kukubali mabadiliko
 
Nafikiri hili suala hamjaliangalia katika mapama yake...mimi sijaribu kumtetea Kanambu ila naona hili suala lilichukua sura nyingine.Yaani watu kujaribu kumdhalilisha Kanumba kwa kuwa tu hakuweza kuji-express kithungu kweli hii tuona sawa?

Kiingereza ndo nini?Je kwa kuzungumza kiingereza kizuri sana ndo inaonekana mtu ameelimika.Haya ni mawazo finyu kabisa na mtazamo kuwa kwa sababu Kanumba ameharibu mambo kwa kuwa hakuongea kiingereza kizuri ni potufu na ambao unapaswa kukemewa kabisa katika jamii yetu.

Nakubali kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao walikusanyika hawakujenga hoja za msingi zaidi ya kulalama tu ila pia nawapongeza baadhi yao ambao walionesha kuwa tukio zima liligubikwa na hali ya udhalilishaji.

Kwa mfano ukiangalia Radio clouds walikuwa na jingle kadhaa za kumponda Kanumba....sasa kweli a radio station ambayo inategemewa kufanya mambo ya maana zaidi inatoa jingles ili kumponda mtu aliyekosea kuzungumza kiingereza halafu zaidi huyu anajulikana kabisa kuwa kiingereza si lugha yake ya kwanza.

Wasanii waliuliza........ni mara ngapi radio na vyombo vyetu vya habari wame-comment kuhusu kiingereza kibovu mno cha MARCIO MAXIMO,kocha wetu wa timu ya taifa?Tuseme hiki hatukioni kwa kuwa yeye ni mtu kutoka Brazil?Kwa hiyo unapoangalia unaona ilikuwa hali ya ukandamizaji na kupotosha hali halisi.

Nafikiri tuna nafasi ya kukosoa na kuponda lakini tufanye hivyo tukiwa na mtazamo wa kurekebisha na kujaribu kusaidia mtu ai-improve otherwise kukosoa kwetu na kuponda itakuwa kama ni jitihada za kudidimizana and this where a problem is.

Tatizo la wasanii wetu si lugha kama wengi walivyofafanua. Maximo yes lugha inamsumbua lakini unaelewa logic yake.
wanatakiwa wajue maana ya sanaa, kama wanatengeneza movie, inapaswa ionekane kama movie. picha zao nyingi nimeziona, lakini si sanaa ile tunayoijua ni kama wanaelezea matukio ya kawaida na kwa kawaida mno bila kuonyesha ubunifu wowote utakaomfanya mtu anayetizama kuumiza kichwa kidogo kufikiri (ambapo ndiyo kwenye utamu wenyewe wa picha). Tatizo lao kubwa ni umbumbumbu. wanatakiwa wafanye kazi kubwa sana kujiendeleza ki sanaa. si wabunifu; si watunzi wazuri; hawajui ku act au wanachukua nafasi wasizostahili; wanajiinua mno kuwa kwenye level wasiyostahili; nk nk.
ushauri
1. Watafute wataalamu wa kutunga stories, UDSM, au Bagamoyo nk.
2. Watafute waongozaji wazuri (profesionals), wasiongoze wao
3. Washauriwe waigize wakiwa kwenye natural form
4. Wasilazimishe nafasi kwenye movie
5...........
6.............
 
Kanumba's awards from Kanumba's blog


YEAR 2005 I was nominated for BEST ACTOR in Tanzania (Risasi Awards)


YEAR 2006 A winner of the IJUMAA Sexiest male bachelor of the year (Global Publishers tz)

YEAR 2006 Best Actor of the Year(Baab Kubwa Magazine)


YEAR 2007 Awarded AN INTERNATIONAL AWARD as THE BEST ACTOR in Tanzania (Hollywood John Wayne International Awards)


YEAR 2008 Awarded a Honorary Award (Tanzania Film Vinara Awards)


YEAR 2008 Best Artist of the Year 2007/2008 (Federation of Artist in Tanzania, SHIWATA)

Aaaaaaaaaaaaaggggggggggghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!
 
kweli sasa mambo ni hovyohovyo Tanzania, zile enzi ulikuwa uwezi kusikia miziki ya kipuuzi maredioni na wale jamaa wa TFL (Tanzania Film) walikuwa wapo makini mno katika ukaguzi wa filamu zote, sasa hizi za kina Kanumba hata kwenye maigizo hazipo,
Kama Kanumba anataka kuwa international Cerebrity hana budi kujifunza lugha ya mawasiliano duniani (Kiingereza), Van Dame ni Mbelgiji lakini alipigana kujifunza kiingereza ili aingie Hollywood, kwa nini Kanumba asiige mfano huo au kama ni shida bac apate ushauri kutoka kwa TK (Teddy Kalonga) ambaye anakula bata pale Hollywood

Kituko niko pamoja na wewe...hata gavana wa California Arnold Schwarzenegger...naye hivyo hivyo kama Van Dame...
 
kwa ufahamu wangu ni vigumu sana kutengeneza movie nzuri kwa kutumia vifaa vibovu.

hiki kinaharibu sana movie za kitanzania.

unakuta movie imerekodiwa na sony PD170 au Sony PD190,hizi ni amateur level cameras maalum kwa weddings and birthday parties,tena western wedding ambazo usually zina wageni 50-100.kwa maana kuwa hata hizi wedding za kitanzania zinazojaza kanisa la watu 1000 hizi camera hazifai.

ukija hizo studio zao ndio kabisa,full of pentinum 4 processor's computers with movies edited with the likes of adobe software etc,this is sad.

Elimu ya watu waliopo kwenye movie industry tanzania ni kiduchu,sasa kama sound editing inafanywa na DJ unategemea kusiwe na makelele?

hapa wakuwalaumu ni wasomi wetu ambao wakishapata vi-degree kuna baadhi ya kazi wanazipiga mstari-hawazitaki tena,sio saizi yao,mie huu naona ufinyu wa akili.

Pindi watanzania watakapoanza kwenda university kusoma vitu kama sound engineering na video editing as well as convesion etc ndipo mtakapoanza kuona movie zenye quality nzuri.

actors wetu wanajitahidi ila ukosefu wa exposure na muongozo vinawaangusha.wale wenzao wa hollywood sio ma-genius kiasi hicho sema they have the right people running their brands.PR Managers should ring a bell here..,

kuhusu lugha ni vizuri wakatumia kiswahili,ili wawe huru zaidi na wawe natural zaidi,movie nzuri hata usipoongea maneno ya kiingereza hata oscar itashinda.art has a way of talking to people.si mnakubuka "memoirs of geisha" and many other movies that won the best foreign movie award?!

hii tabia yao ya kukopi movie za ki-nigeria inakera sana watu-especially the educated segment of tanzanians..,which is growing rapidly.Lakini kwa asilimia kubwa ya watanzania ambao nao kingereza ni mtego,hizi movie zina wapenzi wengi tu wakutosha,so i guess this is marketing forces speaking here.so sa,it kills creativity.
But we should expect this from form 4 leavers right?
 
Kineno kipya cha mtaani ni UKANUMBA,ukikosea lugha hapo ujue umekanumba na utaambiwa acha ukanumba!
 
Wadau!! Waacheni hii mijamaa iyandamane ili jamii na watazania wote wajue huo upuuzi, ujinga na umbumbu wao.
 
Samahani mie nitapingana kidogo na wachangiaji hapo juu, Hvi ni Watanzania wangapi wanaweza kuongea sentensi 5 kwa kiingereza bila kuboronga?? Ni wachache ambao wamepata bahati ya kusoma shule za English Medium na wengine wengi ambao wazazi wao walikuwa na uwezo wa kuwapeleka ulaya wakasome. Sisi wengine tuliosoma shule zetu za kina Kanumba hatuwezi. Na hata ukienda kujiendeleza kusoma kiingereza kuflow inakuwa ni ngumu sana. Mie nafikiri badala ya kumcheka na kum-critisize labda tungetafuta namna ya kumshauri.

Kama mnaangalia Big Brother kuna Mshiriki wa kiume kutoka Msumbiji anaitwa Lionel hajui kabisa Kiingereza na anachapia ile mbaya, Tujiulize kitu kimoja kwani Kiingereza ni lugha yetu??? Watu mmeifanya issue sana, Na wala sio suala la shule kwani ni wangapi wamesoma mpaka Chuo Kikuu na Degree zao lakini hawawezi ku-flow kiingereza? Sio tu wasanii wenzake hata sisi tupo wengine wengi ambao hatukupendezewa na namna watu walivyoli-handle suala la Kanumba akiwa BBA

Tuache Kasumba ya kikoloni lugha yetu ni kiswahili na ndio 'Communication Language yetu Watanzania.
unachokisema kuhusu Kiiingereza uko sawa, lakini acha kumtetea kanumba kwasababu ki ukweli kaboronga , na kumbuka kanumba hakwenda pale kama mshiriki kaenda kama celebrity tena kwa kujigamba msanii anayetaka kwenda kimataifa, sasa jiulize swali moja wangapi wameenda Hollywood ambapo hawajui Kiingereza?
swala la msingi yeye kanumba anajua kabisa kwamba BBA lugha inayotumika kuwasiliana ni Kiingereza na si nyingine yeyote , alikubali vipi kwenda kuliwakilisha taifa wakati hata msingi wa kiingereza hana? na si hilo tu nadhani utakubaliana na mimi jinsi upeo wake wa akili wa kujibu maswali ulivyokuwa mdogo ,
na tafadhali acha kusingizia shule za serikali ndo kisa cha kanumba kutojua kingereza , kwasababu majority tumesoma kwenye shule hizohizo lakini tumefanya juhudi binafsi kujaribu kujifunza hicho kiinegereza, yuko kwenye uigizaji kwa miaka mingapi amejishindwa kujifunza hata kiingereza cha kuombea maji? wakati alipokuwa anapanga kuigiza movie na wanigeria si ndo ilikuwa changamoto kubwa ya kwenda kozi ya kiingereza?
mbona mnaacha kuongea ukweli na kutetea vitu visivyo na msingi, Je unataka kuniambia kisa tumesoma shule za serikali na sio English Medium basi tusijiendeleze tukapata kazi kwenye mashirika ya kimataifa kisa nadumisha kiswahili changu? weee bwana acha hizoooo,
hawa wasaniiii ukweli wanalewa na sifa huko mitaani tunaonana nao kila siku maringo ulevi na uzinzi ndo wao wanaona ndo maisha wameyapatia lakini ukweli mie ningekuwa wao ndo kwanza maisha yanakuwa yanaanza kwa kujipanga na kujiendeleza zaidi, afadhali hata hawa wasaniii wa muziki naona siku hizi wamezinduka wanaingia shule na kujiendelza.
wasaniii wanatakiwa wasome waongeze upeo wao wa uelewa na ufanisi, na waache blah blah blah za akina kanumba na rey
 
Swala hapa sio kuongea kiingereza...swala ni wasanii wanataka kuandamani kisa kukomediwa....sasa kama unasoma between lines utaona point!

Kukomediwa ni muhimu watake wasitake maana kazi ya sanaa ni nini? kukosolewa pia ni kazi ya sanaa,sasa kama hawataki kukosolewa wahamie sayari nyingine ambayo hawatakutana na mambo ya kukosolewa.

kama mtu hataki kukosolewa lazima atakuwa na matatizo ya kumtosha,kwanza ukiona unakosolewa jua hiyo ni changamoto kwako na pia itakuweka mahali pazuri pa kurekebisha yale ambayo hayajakaa sawa.
 
Tatizo la percent kubwa sana ya wasanii wa bongo ni elimu ndogo na exposure hakuna!!!!hawapendi kujifunza!!!!!..it is my view kuwa they do not bother reading books, articles...browsing the internet to learn whats happening outside our borders etc....kazi yao kubwa ni kufuatilia upuuzi, kujidai once they think they have become famous, kuendekeza ngono zembe, pombe u name it!!!!! What the movie industry in Tz needs is people with brains who are ready to learn, be creative and come up with good movies.....not the "copy and paste" that is going on now.....kwa wale wote wanaoplan kuandamana eti kumtetea Kanumba i have a message for you.....GET A LIFE U MORONS!!!!!!

a free advuce kanumba , ur still young why dont u go to school now?
 
Sio Kanumba tuuu!!!!! wako wengi lakini wamejificha!!!siku yao ipo!!!!!hasa hao wanajiita masuper star!!!!
 
Bwana Gwiji wewe unamwambie mwenzio aende shule wakati wewe hata spelling za english zinakushinda advice inaandikwa hivi sio (advuce) taratibu wabongo andika kiswahili lugha yako!!!!!!!!
 
Bwana Gwiji wewe unamwambie mwenzio aende shule wakati wewe hata spelling za english zinakushinda advice inaandikwa hivi sio (advuce) taratibu wabongo andika kiswahili lugha yako!!!!!!!!

mh! sasa nani anayejua lugha? huyu naye kiswahili kimemshinda? au ni taiping era tu? kw ujumla wetu wabongo wachache sana wenye kuongea kiingereza fasaha! na hasa ni wachache zaidi wenye kuongea kiingereza cha ukweli....kwa kuangalia matamshi na matumizi ya misamiati mballimbali katika mazingira tofauti. Kutojua kiingereza siyo ishu sana kama mtu ni msanii asilia mwenye kujituma...tunaona wahindi na wachina wanajipenyeza mpaka hollywood kwa kiingereza cha kuungaunga. Nikirudi kwenye mada yetu, Kanumba anajifunza kiingereza jamani, kujua lugha kwa urahisi zaidi ni kuitumia, unakosea watu wanacheka unajirekebisha, siyo kwenda twisheni halafu unatoka bila lolote. Tufanyeni kazi kwa bidii jamani, wengine wanaongea kiingereza kizuri tu mtaani lakin wamefulia sana tu, na wengine hawajui kiingereza vizuri lakini wanafanya biashara za mamilioni ya dola na waingereza.

karagabaho
 
Back
Top Bottom