Wana filamu kuandamana, kisa Kanumba ka-comediwa!

Wakuu Heshima Mbele,
Kuna kitu kimoja naona hakijawekwa bayana hapa kuhusu huyu Kanumba. Watu wengi wanashindwa tofautisha au changanua hii kitu. Kuna swala la LUGHA na swala la UMBUMBUMBU wa mtu mwenyewe. Umbumbumbu nikimaanisha lack of appropriate knowledge of things, exposure etc. Sasa jinsi nionavyo mimi mtu ambaye si MBUMBUMBU yaani mwenye uelewa wa mambo mbalimbali na ambaye yuko exposed vizuri hata kama hajui lugha vizuri, atabaki kuwa mtu mwenye mchango makini na wa kuonekana ktk jamii. Sasa kwenye issue ya Kanumba si LUGHA, ni uMBUMBUMBU and lack of exposure.

Mfano ni watu wangapi umekutana nao hawajui kiingereza (ie. wanaongea kwa kusua sua) lakini points wanazomwaga au the way wanavyo angalia vitu mwenyewe una-appreciate? Wapo wengi sana.

Vile vile kuna watu ambao wanakimombo kimetulia ajabu, wanaflow mpaka waweza sinzia lakini ukiangalia substance ya anachoongea waweza tapika. Uelewea wa mambo na mazingira fulani ni muhimu pia.

Nilichokiona kwa kanumba ni kwamba hayuko that exposed, hata kama lugha ina sua sua lakini kuna mambo ya msingi hayajui. Hata ukiangalia ile biography yake, hata angeiweka kwa kiswahili still ilikuwa na mapungufu mengi sana.

Sisemi kwamba lugha haichangii, la hasha, inachangia lakini kwa case ya Kanumba it is more of what he knows than the language itself.
 
Badala ya kuandamana kudai haki za kazi zao wanazo zulimiwa na wadosi wao wana andamana kwa swala UJINGA nendeni mkasome nyie maneno mengiii mpaka haki zenu zinapotea hivi hivi.
 
Badala ya kuandamana kudai haki za kazi zao wanazo zulimiwa na wadosi wao wana andamana kwa swala UJINGA nendeni mkasome nyie maneno mengiii mpaka haki zenu zinapotea hivi hivi.

Mkuu well said hapo.
 
This is for Kanumba n Company

British Council- Tanzania (Dar es Salaam)

Office Hours
Monday to Friday0730 - 1530Saturday, Sunday and public holidays ClosedLearning Centre HoursMonday to Friday 0800 - 1800Teaching Centre hoursMonday to Saturday 0800 - 2000

spacer.gif
Address
spacer.gif
spacer.gif
Samora Avenue / Ohio Street
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
PO Box 9100
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
spacer.gif
Dar es Salaam, Tanzania
spacer.gif
spacer.gif
Map
spacer.gif
spacer.gif
Where to find us in Tanzania
spacer.gif
spacer.gif
Telephone
spacer.gif
spacer.gif
+255 (0) 22 2165300
spacer.gif
spacer.gif
Fax
spacer.gif
spacer.gif
+255 (0) 22 2112669 / 2116577
spacer.gif
spacer.gif
E-mail
spacer.gif
spacer.gif
info@britishcouncil.or.tz
spacer.gif
 
Nafikiri hili suala hamjaliangalia katika mapama yake...mimi sijaribu kumtetea Kanambu ila naona hili suala lilichukua sura nyingine.Yaani watu kujaribu kumdhalilisha Kanumba kwa kuwa tu hakuweza kuji-express kithungu kweli hii tuona sawa?

Kiingereza ndo nini?Je kwa kuzungumza kiingereza kizuri sana ndo inaonekana mtu ameelimika.Haya ni mawazo finyu kabisa na mtazamo kuwa kwa sababu Kanumba ameharibu mambo kwa kuwa hakuongea kiingereza kizuri ni potufu na ambao unapaswa kukemewa kabisa katika jamii yetu.

Nakubali kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao walikusanyika hawakujenga hoja za msingi zaidi ya kulalama tu ila pia nawapongeza baadhi yao ambao walionesha kuwa tukio zima liligubikwa na hali ya udhalilishaji.

Kwa mfano ukiangalia Radio clouds walikuwa na jingle kadhaa za kumponda Kanumba....sasa kweli a radio station ambayo inategemewa kufanya mambo ya maana zaidi inatoa jingles ili kumponda mtu aliyekosea kuzungumza kiingereza halafu zaidi huyu anajulikana kabisa kuwa kiingereza si lugha yake ya kwanza.

Wasanii waliuliza........ni mara ngapi radio na vyombo vyetu vya habari wame-comment kuhusu kiingereza kibovu mno cha MARCIO MAXIMO,kocha wetu wa timu ya taifa?Tuseme hiki hatukioni kwa kuwa yeye ni mtu kutoka Brazil?Kwa hiyo unapoangalia unaona ilikuwa hali ya ukandamizaji na kupotosha hali halisi.

Nafikiri tuna nafasi ya kukosoa na kuponda lakini tufanye hivyo tukiwa na mtazamo wa kurekebisha na kujaribu kusaidia mtu ai-improve otherwise kukosoa kwetu na kuponda itakuwa kama ni jitihada za kudidimizana and this where a problem is.
 
Hebu tuanzeni kuandika Kiingereza sisi humu kwenye hii topic....

Yap, simtetei najua kakosea na hataki kushauriwa ila tumjadili Kanumba kwa kiingereza hapa tuone kama wachangiaji hawajapungua!!
 
Hebu tuanzeni kuandika Kiingereza sisi humu kwenye hii topic....

Yap, simtetei najua kakosea na hataki kushauriwa ila tumjadili Kanumba kwa kiingereza hapa tuone kama wachangiaji hawajapungua!!

Why don't you lead the way and put your comments in English?
 
Nafikiri hili suala hamjaliangalia katika mapama yake...mimi sijaribu kumtetea Kanambu ila naona hili suala lilichukua sura nyingine.Yaani watu kujaribu kumdhalilisha Kanumba kwa kuwa tu hakuweza kuji-express kithungu kweli hii tuona sawa?

Kiingereza ndo nini?Je kwa kuzungumza kiingereza kizuri sana ndo inaonekana mtu ameelimika.Haya ni mawazo finyu kabisa na mtazamo kuwa kwa sababu Kanumba ameharibu mambo kwa kuwa hakuongea kiingereza kizuri ni potufu na ambao unapaswa kukemewa kabisa katika jamii yetu.

Nakubali kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao walikusanyika hawakujenga hoja za msingi zaidi ya kulalama tu ila pia nawapongeza baadhi yao ambao walionesha kuwa tukio zima liligubikwa na hali ya udhalilishaji.

Kwa mfano ukiangalia Radio clouds walikuwa na jingle kadhaa za kumponda Kanumba....sasa kweli a radio station ambayo inategemewa kufanya mambo ya maana zaidi inatoa jingles ili kumponda mtu aliyekosea kuzungumza kiingereza halafu zaidi huyu anajulikana kabisa kuwa kiingereza si lugha yake ya kwanza.

Wasanii waliuliza........ni mara ngapi radio na vyombo vyetu vya habari wame-comment kuhusu kiingereza kibovu mno cha MARCIO MAXIMO,kocha wetu wa timu ya taifa?Tuseme hiki hatukioni kwa kuwa yeye ni mtu kutoka Brazil?Kwa hiyo unapoangalia unaona ilikuwa hali ya ukandamizaji na kupotosha hali halisi.

Nafikiri tuna nafasi ya kukosoa na kuponda lakini tufanye hivyo tukiwa na mtazamo wa kurekebisha na kujaribu kusaidia mtu ai-improve otherwise kukosoa kwetu na kuponda itakuwa kama ni jitihada za kudidimizana and this where a problem is.

Hapa siungani na wewe hata kidogo mkuu,Kanumba alichemka,period.Kama lugha yakiingereza haipandi ni bora tu angezungumza kwa lugha ya Kiswahili ama Kisukuma badala ya kumwaga PUMBA zile ambazo alijua kabisa kuna mamilioni ya watu duniani yanamuangalia live..Na hao waandaaji waliompeleka hawakuliangalia hili???,kwa nini wampeleke mtu ambaye ni maimuna kwenye TV show kubwa kama BBA.

Halafu unakosea sana unapomlinganisha Kanumba(Kayumba???) na Marcio Maximo aisee,Maximo hajui Kiswahili,yeye lugha anayoijua kiufasaha ni Kireno tu na hata kwao Kiingereza chafundishwa kwa nadra sana tofauti na sisi Tanzania ambako mwanafunzi huanza somo la Kiingereza(enzi zetu) tangu darasa la 3 na akifika Sekondari Kiingereza hutumika kama ndiyo medium of Instruction,Kanumba yeye kasoma mpaka form 6 that means katumia kiingereza akiwa shule na kuujua uwezo wake ukoje katika lugha hiyo ya watu,lakini pamoja na akwamba anajua uwezo wake wa kuzungumza na kuandika kiingereza ni mdogo bado anadiriki kusimama mbele ya jamii na kuanzakuongea madudu kama yale aiyoongea katika BBA ama yale aliyoandika kwenye ile Biography yake,kwa nini asingemuajiri mtu kumtayarishia hiyo biography yake??,na je kwa nini hao Multichoice Tanzania wasingemtafuta msanii/mtu ambaye wanajua kabisa aweza kuongea kiingereza kwa ufasaha kwa ajili ya kutuwakilisha waTanzania

Tubadilike jamani,tusiutetee ujinga/upuuzi huu,kama vp tuyatumie makosa haya ya Kanumba kuitangaza lugha yetu adhimu ya Kiswahili badala ya kukikumbatia kiingereza ambacho kwa baadhi ya watu ni kigumu kuongea bila ya kukariri maneno(nakumbuka enzi za DEBATE shuleni)…Pa1
 
Last edited:
Hivi Kanumba kaongea nini Kule BBA 4? Kuna mjomba yeyote aweza kutusaidia clips tafadhali?

Nani alimchagua Kanumba kwenda mle ndani kukaribisha mastaa wa BBA4 mwaka huu? je ulifanyika usaili wa kutosha kwa lugha ya BBA 4?

Hivi kwenye pambabo la ngumi wampeleka mcheza ngoma? aaah nimeuliza tu!! Kosa lilianzia hapo, kwani sote twajua tukiangalia BBA, lugha inayotumika ni Kimombo. Sasa kama kanumba hajui Kimombo, kwanini alipelekwa mle???

Swali jingine tunapaswa kujiuliza, hata kama si tatizo lake la kutojua Kimombo, hivi kanumba anaweza akashusha mada tukazielewa na kuzitafakari hata kwa Lugha ya Kiswahili?

Aitwe siku moja kwenye Q&A session ya radio au TV yeyote afu tumuone akimwaga sera kwa Lugha ya Kiswahili! Hivi anaweza kabisa huyu??????

Then, baada ya hapo, ruhsa wasanii wa maigizo kuandamana!
 
Pamoja na kwamba KANUMBA ni maamuma lakini kuna kitu wakuu tusisahau.... UTU.

Kuna sheria za defamation ambazo badala ya kuandamana nadhani KANUMBA na mabogus wenzake wangezitumia kuwaangika msalabani ze comedy. Kwani vitendo vyao ni uchizi kuliko ubogas wa KANUMBA na vidampa wake.

Muvi za BONGO ni chariot chasser kwa masupa staa na siyo even amateur yaani hata mwanzo bado.

Tudumishe UTU watanzania
 
Aisee,sanaaa ya bongo inaelekea wapi?
Mbona ugonvvi mwingine kati ya wasanii hauna maan?

Kama kawaida ya original comedy,wiki iliyopita walimuigiza kanumba akishindwa kuongea kimombo pale mjengoni south..yaani BBA revolution. Jana tukashuhudia wasanii kibao wa filamu nchini wakitaka kuandamana na wakijadili jinsi ya kuwaangamiza original comedy.... Hii ilikuwa kenye kipindi chabongo movies EATV jana usiku.

Hivi kweli hii ni sahihi wasanii kujadili jinsi ya kuwaangamiza wasanii wenzao?

Mtindo wa kuwaaigiza watu,original comedy hawajauanza leo wala jana.....wamewaigiza mawazili,wabunge,watu maarufu,mpaka Rais...

Kumuigiza kanumba ndo imekuwa nongwa?

Tunaliangalije hili bandugu....tuelekea pabaya.

hujajua mkuu. Hiyo ni muvi laiv si rekoded ambayo unapaswa kutulia na kutazama na wala si kuhofu. Enjoy the trailer
 
Kanumba's awards from Kanumba's blog

YEAR 2005 I was nominated for BEST ACTOR in Tanzania (Risasi Awards)

YEAR 2006 A winner of the IJUMAA Sexiest male bachelor of the year (Global Publishers tz)

YEAR 2006 Best Actor of the Year(Baab Kubwa Magazine)

YEAR 2007 Awarded AN INTERNATIONAL AWARD as THE BEST ACTOR in Tanzania (Hollywood John Wayne International Awards)

YEAR 2008 Awarded a Honorary Award (Tanzania Film Vinara Awards)

YEAR 2008 Best Artist of the Year 2007/2008 (Federation of Artist in Tanzania, SHIWATA)
 
kweli sasa mambo ni hovyohovyo Tanzania, zile enzi ulikuwa uwezi kusikia miziki ya kipuuzi maredioni na wale jamaa wa TFL (Tanzania Film) walikuwa wapo makini mno katika ukaguzi wa filamu zote, sasa hizi za kina Kanumba hata kwenye maigizo hazipo,
Kama Kanumba anataka kuwa international Cerebrity hana budi kujifunza lugha ya mawasiliano duniani (Kiingereza), Van Dame ni Mbelgiji lakini alipigana kujifunza kiingereza ili aingie Hollywood, kwa nini Kanumba asiige mfano huo au kama ni shida bac apate ushauri kutoka kwa TK (Teddy Kalonga) ambaye anakula bata pale Hollywood
 
Tatizo la wasanii na wanamichezo wetu wanacheza sana na majukwaa. Wakisikia wanapigiwa makofi tu wanavimba vichwa ,wanakuwa wakaidi wasiotaka hata ushauri. Sasa kama watu waliomuona KANUMBA kachemsha kwa nini wasimseme?????????. Nadhani anatakiwa awe MJINGA aliyetayari kukosolewa na kurekebishwa kuliko kuwa MPUMBAVU asiyetaka kukosolewa na aendelee kutuletea madudu yake. KANUMBA kukosea sio kosa ila kosa ni kurudia kukosea.
 
Kanumba's awards from Kanumba's blog

YEAR 2005 I was nominated for BEST ACTOR in Tanzania (Risasi Awards)

YEAR 2006 A winner of the IJUMAA Sexiest male bachelor of the year (Global Publishers tz)

YEAR 2006 Best Actor of the Year(Baab Kubwa Magazine)

YEAR 2007 Awarded AN INTERNATIONAL AWARD as THE BEST ACTOR in Tanzania (Hollywood John Wayne International Awards)

YEAR 2008 Awarded a Honorary Award (Tanzania Film Vinara Awards)

YEAR 2008 Best Artist of the Year 2007/2008 (Federation of Artist in Tanzania, SHIWATA)
Angalia hata hizo Tuzo zenyewe,ni UPUPU mtupu yaani...Eti best Actor wa Tanzania anayetambuliwa na John Wayne International ya Hollywwood...Lol..,halafu kichekesho et Dogo huwa ajiita Denzel Washington wa Tanzania
 
Back
Top Bottom