Mtu yeyote, akili timamu, mwenye kazi nzuri Ulaya au Marekani, hata siku moja siwezi kukushauri kurudi hapa Tanzania. Utaishiwa kufanyiwa majungu na kurudi zako na aibu. Lakini ukiwa muosha wazee na choo, njoo, piga majungu ya nguvu kish autafanikiwa.
Serikalini na hata ndani ya vyama vya kisiasa, hawa madiaspora VICHWA hawawezi kukubalika kwa sababu mitazamo yao ni tofauti. Mtu aliyefanya kazi ya maana marekani kwa miaka mingi, hawezi kurudi hapa na kukubalisha kupindisha work ethics kwa manufaa yake binafsi. Hizi ni kazi ambayo wasomi uchwara kama Nape , Nchimbi, Mahanga wanaziwezea.
Kwa kifupi ni kwamba mazngira ya Diaspora ni magumu sana humu nchini, unless wanajiajiri. Hata akikuijia JK mwenyewe, usikubali kuja. JK msanii babu kubwa mwenye longolongo kibao. Utaiishia kuuwawa au kufanyiwa majungu na frustration za ajabu. Wanajifanyaga kutafuta wataalamu, lakini wapi. Kwa wanawake lazime uvue chupi. Mwanamme Rushwa, na hata ukipata kazi, unapewa kazi kulinda maslahi ya watu. Wasomi wangapi walotukuka wapo huko Ulaya, unadhani wanahitajika serikalini?
Kama hawapati 30% hakuna kitu. Diaspora kaeni huko mfanye kazi zenu, hadi pale Dr. Slaa atakapoingia madarakani