Wana Diaspora: Je mliorudi kufanya biashara au Kazi zinaendeleaje? Mmejifunza nini mpaka sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana Diaspora: Je mliorudi kufanya biashara au Kazi zinaendeleaje? Mmejifunza nini mpaka sasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, Jul 11, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,111
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Kuna wana Diaspora wengi walirudi nyumbani miaka ya karibuni kufungua kampuni zao na wengine kufanya kazi. Je wanaendeleaje. Kama wewe ni mwana Diaspora uliyerudi tupe ukweli hapa tuelewe. Kama una rafiki au ndugu aliyerudi na unaelewa maendeleo kuanzia arudi tupe apa ili watu tuweze kujifunza. Kuna tatizo moja la Culture kwasababu wewe ni Mtanzania ni vigumu watu kuelewa kama Culture yako imebadilika kidogo ukienda Tanzania lakini baada ya kukaa sehemu miaka 10, 15 au 20 Culture yako haiwezi kuwa ileile. Je mnakabiliana vipi na hili swala.
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Tanzania bila kujichanganya na wakubwa na pia kujiunga na chama tawala hauwezi kufanikiwa
  [​IMG]
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Naona Le Mutuz anakimbiza sana hapo mjini siku hizi. Soon tutamsikia akirushwa na FM Academia etc.....

  'Pedejeee Le Mutuz'......kimbiza haooooooooo
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mtu yeyote, akili timamu, mwenye kazi nzuri Ulaya au Marekani, hata siku moja siwezi kukushauri kurudi hapa Tanzania. Utaishiwa kufanyiwa majungu na kurudi zako na aibu. Lakini ukiwa muosha wazee na choo, njoo, piga majungu ya nguvu kish autafanikiwa.

  Serikalini na hata ndani ya vyama vya kisiasa, hawa madiaspora VICHWA hawawezi kukubalika kwa sababu mitazamo yao ni tofauti. Mtu aliyefanya kazi ya maana marekani kwa miaka mingi, hawezi kurudi hapa na kukubalisha kupindisha work ethics kwa manufaa yake binafsi. Hizi ni kazi ambayo wasomi uchwara kama Nape , Nchimbi, Mahanga wanaziwezea.

  Kwa kifupi ni kwamba mazngira ya Diaspora ni magumu sana humu nchini, unless wanajiajiri. Hata akikuijia JK mwenyewe, usikubali kuja. JK msanii babu kubwa mwenye longolongo kibao. Utaiishia kuuwawa au kufanyiwa majungu na frustration za ajabu. Wanajifanyaga kutafuta wataalamu, lakini wapi. Kwa wanawake lazime uvue chupi. Mwanamme Rushwa, na hata ukipata kazi, unapewa kazi kulinda maslahi ya watu. Wasomi wangapi walotukuka wapo huko Ulaya, unadhani wanahitajika serikalini?

  Kama hawapati 30% hakuna kitu. Diaspora kaeni huko mfanye kazi zenu, hadi pale Dr. Slaa atakapoingia madarakani
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tanzania pazuri tu hamna shida sema ukija huku usifikiri kwakuwa unaongea kizungu puani ndio utapewa kipaumbele iwe ajira , business etc watu wameamka sana.

  Pia uwe tayari kuishi Tanzania kama mtanzania sio kama mgeni au mtu uliyekaa nje miaka mingi.

  Ukifika Roma ishi kama Mromani.
   
 6. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  sie wengine wacha tubaki hapa hapa ....
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,779
  Likes Received: 83,124
  Trophy Points: 280
  Kuna vigodi faza na vigodi maza mpaka uvilambe lambe na wakutoe upepo kisha uwaambie kama nawe ni mwanachama hai wa magamba ndio mambo yako yakunyokee. Mfano halisi ni Dr Ferdinand Masau mzalendo aliyeamua kurudi nyumbani kuwasaidia Watanzania wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo. Katumia pesa zake chungu nzima leo hii anaadhirika kwa nia yake nzuri ya kutaka kuisadia Tanzania na Watanzania.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Swali zuri sana; jibu lake lina sura mbili:

  Sura ya Kwanza: Mwulize Dr Masau alieacha kazi nzuri huko Texas akaenda kuanzisha huduma ya tiba ya moyo Tanzania; ni takribani miaka saba sasa tangu afanye hivyo mwulize amefanikiwa vipi.

  Sura ya Pili: waulize wale wote waliorudi na kuanzisha business au kufanya kazi wakiwa affiliated na chama tawala kwa namna moja au nyingine.
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  If you have something to offer utafanikiwa, be it skills, goods or service.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Bora nipige box huku huku niwe nauza simu bongo na kukodisha vyombo vya harusi. Hayo mengine yapo complicated.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Dr.Massau huyu huyu ambae hajawahi kuwa na leseni ya kufanya kazi Texas au Dr.Masau mwengine?
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hizi ni propaganda tu za kuhalalisha yaliyofanywa na serikali yetu. Angekuwa siyo daktri aliyefuzu na wa kuaminika katika fani yake, daktari maarufu kama Dr Cooley asingemkubali; wazungu huwa hawakopeshi. Dr. Cooley huyo alijitolea hata kumsaidia Dr. Masau kupata vifaa na hadi kukubali kuwa anamtembelea Tanzania kumsaidia katika operations ambazo ni more complex.
   
 13. d

  dachy12 Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  i think inategemea na kiwango cha ujuzi/elimu na uzoefu ulio nao katika maswala mbalimbali ,pia Tanzania ya sasa imenuka na rushwa and corrupted government at large so unakuta professionalism inaachwa na wana associate mafanikio na siasa ndo mana inakuwa ngumu ukirudi kupata breakthrough kwenye maeneo mbalimbali coz of bribes katika system..
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mbona kwa maneno yake mwenyewe Dk.Masau alisema kuwa hajawahi kuwa na leseni ya kufanya kazi Texas? Au kajisingizia?

  *Kusaidiwa na Mzungu haimaanishi kuwa alikuwa na kibali cha kufanya kazi Texas, au aliwahi kufanya kazi huko.
   
 15. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Key to all can be broadly summarized as "Tanzania bila kujichanganya na wakubwa na pia kujiunga na chama tawala hauwezi kufanikiwa".
   
 16. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nyie MADIASPORA hamna haja ya kujua yanayowafika wenzenu zaidi ya kuona mambo yaliyomfika mtaalam wa upasuaji wa moyo DR. MASAU!!! Alimyima hisa kwenye hospitali yake waziri mmoja basi huyo waziri wa chama cha magamba akatumia influence yake na kwa vile ni memba wa cc ya magamba ; wakamfanyia fitina huyo daktari bingwa mpaka hospitali yake imefungwa na vifaa vyote kupigwa mnada!! Hiyo ndio bongo ikiongozwa na serikali ya mkweree anaekuja kutalii huko huko Amerika na uingereza na kuwadanganya kuwa mrudi nyumbani!! Huku hakuna kitu ni kuzinguana tu.
   
 17. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nakushauri ndugu kama huko ughaibuni resident permit/work visa yako iko OK, wewe endelea kubana huko huko na ufanye kurudi Bongo kusalimia tu. Na haswa kama wewe ni msomi, ukirudi Bongo there is a big chance you will get frustrated just after a few months. Kwani ujanja ujanja wa Bongo utakuwa umeusahau na hauwezi, hivyo kila jambo utakalo panga kufanya litapiga mwamba. Ushauri, baki huko huko mwana Diaspora

   
 18. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimerudi toka mwezi wa kumi mwaka jana.. miezi mitatu ya mwanzo ilikuwa tight sana. Nikajipanga na nikaamua kufanya shughuli zangu mwenyewe(SIO KUAJIRIWA). ilikuwa ngumu mwanzo. Ila kwa sasa hivi ninaona ninafanya vizuri na ninaona mwanga mkubwa mbele kuliko miaka niliyokaa USA.. Ukweli ni kwamba kuna CHANGAMOTO zake tofauti na changamoto za ulaya na marekani..
   
 19. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,111
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Hivyo kuna dada mmoja ambaye ni ndugu kamaliza shule kwa shidashida baada ya miaka mingi. Kapata kazi kwenye kampuni ya mafuta na anatengeneza kama $50,000 kwa mwaka na anakaa Texas ambako gharama za maisha ni za wastani. Vilevile ana green card lakini kuna watu wana mwambia he rafiri zako wanafanya vizuri zaidi bongo!. Mimi nimemshauri asubiri mpaka kampuni za mafuta na gas zianze kufanya production ambayo ni kama miaka mitatu au minne. Vilevile nimemwambia asisikilize sana watu.
   
Loading...