Wana CHADEMA msitukane mamba kabla hamjavuka mto

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Sijatumwa na mtu kusema haya. Nimejituma mwenyewe. Hapo natoa jibu la post ya kwanza kutoka kwa mashabiki wa CDM. Wala sijapokea bahasha kama kauli mbiu yenu humu isemavyo.

Najua kuwa, Viongozi wa CDM hasa Mnyika, ni watu makini sana. Wanajua nini wanafanya katika vita ya kumkomboa Mtanzania. Nawaunga mkono mia kwa mia. Sasa kimbembe ni kwa mashabiki wa chama, sina hakika kama wote wanaopiga kelele ni wanachama hai au la.

Lakini wanahitaji semina na ushauri nasaha, wapate mfundo wa kuacha hasira, jazba, chuki, hamaki, ukali na kejeli wanapoambiawa ukweli. Lazima watambue kuwa vyama navyo vina kifo, na vifo vingine hutokea ghafla kama kile cha CUF. Kwani walikuwaje wale jamaa? Sasa hivi wako wapi? Msibweteke na mafanikio ya chama kwa sasa!

Kumbukeni kuwa ndio kwanza bado kinatambaa. Wenzenu wanasherekea miaka 35, umri wa mtu mwenye mjukuu. Nyie je? Mingapi! Msitukane wakunga wakati uzazi bado ungalipo.

Kubalini ushauri, na kukosolewa pia. Mtu akikucheka, usimtukane. Jitazame kwani unaweza kuwa umejipakaza kinyesi. Na siku zote kichaa akikwambia "nyoka huyoo" usipuuze! Anaweza kuwa nyoka kweli kwani kichaa naye ana macho japo akili zake zimekaa upande...
 
tangu lini mtu mwenye akiri akatoka cdm? Huko ni waganga matumbo tu kwa style ya kukosoa ili waendelee kula umaskin mbaya sana
 
Tangu lini mtu mwenye akili akatoka ccm chama cha ubwabwa na makhilikhili!haaahaaaaaa
 
Mike Tyson alikuwa bingwa wa dunia katika uzito wa juu kwenye ngumi, akiwa na miaka 18.
 
Sijatumwa na mtu kusema haya. Nimejituma mwenyewe. Hapo natoa jibu la post ya kwanza kutoka kwa mashabiki wa CDM. Wala sijapokea bahasha kama kauli mbiu yenu humu isemavyo.

Najua kuwa, Viongozi wa CDM hasa Mnyika, ni watu makini sana. Wanajua nini wanafanya katika vita ya kumkomboa Mtanzania. Nawaunga mkono mia kwa mia. Sasa kimbembe ni kwa mashabiki wa chama, sina hakika kama wote wanaopiga kelele ni wanachama hai au la.

Lakini wanahitaji semina na ushauri nasaha, wapate mfundo wa kuacha hasira, jazba, chuki, hamaki, ukali na kejeli wanapoambiawa ukweli. Lazima watambue kuwa vyama navyo vina kifo, na vifo vingine hutokea ghafla kama kile cha CUF. Kwani walikuwaje wale jamaa? Sasa hivi wako wapi? Msibweteke na mafanikio ya chama kwa sasa!

Kumbukeni kuwa ndio kwanza bado kinatambaa. Wenzenu wanasherekea miaka 35, umri wa mtu mwenye mjukuu. Nyie je? Mingapi! Msitukane wakunga wakati uzazi bado ungalipo.

Kubalini ushauri, na kukosolewa pia. Mtu akikucheka, usimtukane. Jitazame kwani unaweza kuwa umejipakaza kinyesi. Na siku zote kichaa akikwambia "nyoka huyoo" usipuuze! Anaweza kuwa nyoka kweli kwani kichaa naye ana macho japo akili zake zimekaa upande...

kina pinda + kiroboto a. k.a anna malinda na njaa yenu ya posho,mtaujua jk na bado mtageukana sana
 
Yaan the way wanavyo reply us thread inaonesha wazi gonjwa ulilolisema kweli limeshawaadhiri hata ARV hazina uwezo wa kurefusha fahamu zao!
 
Mchangiaji wa kwanza katika bandiko ana nafasi kubwa sana ya ku-influence michango mingine mingi (siyo yote) itakayofuatia.

(Source: Mimi mwenyewe katika utafiti unaoendelea.)
 
Mimi nijuavyo mtu umri ukienda sana anakuwa mzee,na nguvu za kufanya kazi ngumu zinapungua kwa kiasi kikubwa,hivyo basi usisherekee babu yako kufanya birthday maana siku zake ndio zinaishiria hivyo,BYE BYE BABU CCM.
 
Kwani kuna Boxer alidumu? na hata kama hakudumu, ila ni boxer number 2 aliyeitikisia dunia huku Moh Ali akishika namba 1.

Cha muhimu duniani ni kuacha kumbukumbu. Tyson ameiacha na hadi kesho ataendelea kukumbukwa.

Kwa Tanzania, CCM itasahaulika. Wana bahati tu kuwa walianzia kwenye TANU ambacho kitakumbukwa milele.

Chukua Chako Mapema.
Lakini hakudumu. Akaishia kumpiga jino mtu sikio.
 
kwani ndugu juma au ndugu kichaa kama ulivojiita kwenye thread hii unalinganisha cdm na ccm?unataka kusema kuwa kuishi kwingi ndo ujiniasi au?basi babu yangu kwa sasa angekuwa injia wa roketi-maana ni mzee wa miaka85...pia juma kwani kwenu kinyesi mnajipakaga?maana ni maneno ya aibu unaleta...kajipande...nasema kuwa umetumwa kama ulivotangulia kusema...
 
Back
Top Bottom