Wana CHADEMA msitukane mamba kabla hamjavuka mto

Mimi nijuavyo mtu umri ukienda sana anakuwa mzee,na nguvu za kufanya kazi ngumu zinapungua kwa kiasi kikubwa,hivyo basi usisherekee babu yako kufanya birthday maana siku zake ndio zinaishiria hivyo,BYE BYE BABU CCM.

Kwahiyo ccm wanasheherekea kulikaribia kaburi siyo? Hiyo nayo habari njema kwangu na kwa waTz walio wengi kama ni hivyo
 
kwani ndugu juma au ndugu kichaa kama ulivojiita kwenye thread hii unalinganisha cdm na ccm?unataka kusema kuwa kuishi kwingi ndo ujiniasi au?basi babu yangu kwa sasa angekuwa injia wa roketi-maana ni mzee wa miaka85...pia juma kwani kwenu kinyesi mnajipakaga?maana ni maneno ya aibu unaleta...kajipande...nasema kuwa umetumwa kama ulivotangulia kusema...

Tatizo lenu hamjui hata kusoma. Hiyo hapo chini misemo ya mifano. Sasa wewe kwa akili yako mifano umegeuza na kuwa kitu halisi. Lakini haishangazi kwa sababu akili yako hapo ndo imefikia ukomo wake wa kufikiri. Kuelewa inahitaji mtu makini anayejua vyema lugha. Si mbumbumbu kama ulivyo wewe.
 
Yaan the way wanavyo reply us thread inaonesha wazi gonjwa ulilolisema kweli limeshawaadhiri hata ARV hazina uwezo wa kurefusha fahamu zao!

naona ARV ya kukuza bongo za hawa jamaa itakuwa ngumu sana kupatikana. Wakati mwingine bora uachane nao na gonjwa lao lisilo tiba.
 
Huwa sipendi hili neno: UMETUMWA. Hii ni kudhalilisha JF. Yaani Great Thinkers siyo kwamba wanafikiri bali wanafikirishwa na kutumwa!
 
Kuna mzee mmoja aliniambia kwamba miaka ya 60 Samweli Sitta na wenzake wakiwa wanafunzi wa UDSM waliandamana wakiwa na mabango kuelekea ikulu kupinga mpango wa serikali kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia mafunzo ya JKT.Walikuwa hoja nyingi za msingi likiwemo hilo lakini katikati yao akachomekwa mtu wa usalama aliebeba bango linalokashfu serikali...na hiyo ikawapa serikali sababu ya kuwaaachia waingie ikulu na Mwalimu Nyerere akawalamba viboko.

Nachosisitiza hapa ni kuwa ni vizuri pia kusikiliza upande mwingine wa shilingi hata kama hoja hukubaliani nayo...lakini kinachonishtua ni namna watu wanaotoa maoni ya kukisaidia CDM wanavyoshambuliwa kwa maneno ya kejeli na dharau kana kwamba hiki ni chama cha watu wasiofanya makosa.....Na hili linanishawishi kuamini kuwa miongoni mwa watu wanaokisapoti kuna mamluki,ambao hutoa maneno ya kejeli kuonyesha wanakipenda chama kumbe wanakipaka sifa mbaya ya kukionyesha ni chama kisichokubali kukosolewa.

Haiwezekani iletwe hoja hapa halafu wanaokiunga mkono karibia wote watoe maneno ya kuponda tu bila kujadili hoja.Mtatuharibia chama na kikaonekana ni cha watu wasio kuwa na busara na wanaokurupuka.Hata miongoni mwa viongozi wa CDM wanatofautiana kwa mawazo na hoja lakini hatuwasikii wakipigana vijembe. Tafadhali viongozi muwe mnapita humu kusafisha hali ya hewa.
 
Sijatumwa na mtu kusema haya. Nimejituma mwenyewe. Hapo natoa jibu la post ya kwanza kutoka kwa mashabiki wa CDM. Wala sijapokea bahasha kama kauli mbiu yenu humu isemavyo.

Najua kuwa, Viongozi wa CDM hasa Mnyika, ni watu makini sana. Wanajua nini wanafanya katika vita ya kumkomboa Mtanzania. Nawaunga mkono mia kwa mia. Sasa kimbembe ni kwa mashabiki wa chama, sina hakika kama wote wanaopiga kelele ni wanachama hai au la.

Lakini wanahitaji semina na ushauri nasaha, wapate mfundo wa kuacha hasira, jazba, chuki, hamaki, ukali na kejeli wanapoambiawa ukweli. Lazima watambue kuwa vyama navyo vina kifo, na vifo vingine hutokea ghafla kama kile cha CUF. Kwani walikuwaje wale jamaa? Sasa hivi wako wapi? Msibweteke na mafanikio ya chama kwa sasa!

Kumbukeni kuwa ndio kwanza bado kinatambaa. Wenzenu wanasherekea miaka 35, umri wa mtu mwenye mjukuu. Nyie je? Mingapi! Msitukane wakunga wakati uzazi bado ungalipo.

Kubalini ushauri, na kukosolewa pia. Mtu akikucheka, usimtukane. Jitazame kwani unaweza kuwa umejipakaza kinyesi. Na siku zote kichaa akikwambia "nyoka huyoo" usipuuze! Anaweza kuwa nyoka kweli kwani kichaa naye ana macho japo akili zake zimekaa upande...

Point unayo, jaribu kuiweka wazi kidogo wanajamvi wakuelewe.
 
Kuna mzee mmoja aliniambia kwamba miaka ya 60 Samweli Sitta na wenzake wakiwa wanafunzi wa UDSM waliandamana wakiwa na mabango kuelekea ikulu kupinga mpango wa serikali kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia mafunzo ya JKT.Walikuwa hoja nyingi za msingi likiwemo hilo lakini katikati yao akachomekwa mtu wa usalama aliebeba bango linalokashfu serikali...na hiyo ikawapa serikali sababu ya kuwaaachia waingie ikulu na Mwalimu Nyerere akawalamba viboko.

Nachosisitiza hapa ni kuwa ni vizuri pia kusikiliza upande mwingine wa shilingi hata kama hoja hukubaliani nayo...lakini kinachonishtua ni namna watu wanaotoa maoni ya kukisaidia CDM wanavyoshambuliwa kwa maneno ya kejeli na dharau kana kwamba hiki ni chama cha watu wasiofanya makosa.....Na hili linanishawishi kuamini kuwa miongoni mwa watu wanaokisapoti kuna mamluki,ambao hutoa maneno ya kejeli kuonyesha wanakipenda chama kumbe wanakipaka sifa mbaya ya kukionyesha ni chama kisichokubali kukosolewa.

Haiwezekani iletwe hoja hapa halafu wanaokiunga mkono karibia wote watoe maneno ya kuponda tu bila kujadili hoja.Mtatuharibia chama na kikaonekana ni cha watu wasio kuwa na busara na wanaokurupuka.Hata miongoni mwa viongozi wa CDM wanatofautiana kwa mawazo na hoja lakini hatuwasikii wakipigana vijembe. Tafadhali viongozi muwe mnapita humu kusafisha hali ya hewa.
Mkuu mzee 6 aliwahi kulambwa bakora! Ndio maana ana uchungu.
Mkuu umenena kweli, wapenzi wa CDM wana mahaba kiasi kwamba penye chongo wao wanaona ni kengeza tu!
 
Aisee umenifumbua macho mkuu. Kwa post yako sasa naamini kuwa kumbe mashabiki wa CDM wenye akili na busara zao wametulia tu. Ila wale watukanaji wanaojifanya ndiyo wenye uchungu ni pandikizi wa CCM ndani ya CDM. Ni sampuli ya huyo afisa usalama aliyewachomekea kina Sitta. Hawa ni watu hatari kwa CDM.
 
Mkuu mzee 6 aliwahi kulambwa bakora! Ndio maana ana uchungu.
Mkuu umenena kweli, wapenzi wa CDM wana mahaba kiasi kwamba penye chongo wao wanaona ni kengeza tu!

Kuanzia leo watoa kashfa wote, wale ambao wanajibu upuuzi badala ya hoja. Wataitwa PANDIKIZI wa CCM ndani ya CDM.
 
Ushauri. Hujaelewa nini sasa! Inamaana wewe hata mtu akikushauri huelewi?

Unachokilenga sijakielewa mkuu.mm napenda pale chama kinapokosea kikosolewe ili kirekebishike.lakini pia unapotoa lawama toa na mfano halisi ningekuunga mkono kama ningeona mfano hata 1 wakile chadema walichokosea wakaambiwa alafu mashabiki wakaleta matusi.kinyume na hayo ni haki ukiambiwa umetumwa
 
Kuanzia leo watoa kashfa wote, wale ambao wanajibu upuuzi badala ya hoja. Wataitwa PANDIKIZI wa CCM ndani ya CDM.

I see!Inawezekana ikawa kweli tunasoma michango ya MAPANDIKIZI maana mfuasi wa kweli hawezi kupingana na ukweli wenye lengo la kumtaka ajisahihishe.
 
Upo sawa kabisa mkuu, m2 mwenye busara hua tayari kukosolewa. Kama walivyo viongozi we2 wa CHADEMA.
 
juma kidogo,narudia umetumwa,haiwezekani ukaleta mada ya kimbumbumbu kama ulivoniita...tangu niwepo jf hujawahi kuleta constructive idea kwa chama pinzani...ivi ni kwa lipi tuendelee kuwa na ccm kama point of reference wakati imejaa mafisadi na matapeli waliolipeleka taifa kubaya... wewe pamoja na wenzako hamna moral authority kuweza kuwa kwenye frontline kutolewa mfano...ndugu unatoaje mifano bila substance?acha kuogopa kivuli chako...
 
Unachokilenga sijakielewa mkuu.mm napenda pale chama kinapokosea kikosolewe ili kirekebishike.lakini pia unapotoa lawama toa na mfano halisi ningekuunga mkono kama ningeona mfano hata 1 wakile chadema walichokosea wakaambiwa alafu mashabiki wakaleta matusi.kinyume na hayo ni haki ukiambiwa umetumwa

Hapa hakuna hata haja ya mfano. Wote siyo wageni hapa JF. Kwa mfano mnachokosea ni pamoja na kujibu post utumbo badala ya hoja zenye mashiko.
 
[QUOTE=chatumkali... ndugu ivi ukisoma mada ya jumakidogo,wewe unaona ni wapi amekosoa CDM tofauti na kurusha kejeli kuwa cdm kuna washabiki nk nk kwani ushabiki yeye unamkeraje ingali mada zake zote za nyuma ni kejeli?hatutashindwa kumjibu kwa kuogopa kuitwa MAPANDIKIZI...Mara ngapi akina FF wamekuwa wakileta ushauri mufilisi kwa cdm wakati daily wanapinga classical thoughts!? haiwezekani!
 
juma kidogo,narudia umetumwa,haiwezekani ukaleta mada ya kimbumbumbu kama ulivoniita...tangu niwepo jf hujawahi kuleta constructive idea kwa chama pinzani...ivi ni kwa lipi tuendelee kuwa na ccm kama point of reference wakati imejaa mafisadi na matapeli waliolipeleka taifa kubaya... wewe pamoja na wenzako hamna moral authority kuweza kuwa kwenye frontline kutolewa mfano...ndugu unatoaje mifano bila substance?acha kuogopa kivuli chako...

Ni kweli nimetumwa! Lakini nimetumwa na akili yangu. Huchukuwa muda mwingi sana kumfanya mbumbumbu kama wewe ambumbuke na kuwa mbumbuka. Unajua kuna mbumbumbu, na mbumbuka. Mbumbuka ni yule aliyevuka hatua ya umbumbumbu na kuelimika kidogo. Hujaielewa thread inayotoa ushauri kwa mashabiki wa CDM. Unataka kunihamisha kwenye mada na kunipeleka katika mwavuli wa ufisadi, ufisadi unaoaminishwa wewe kwa kufuata mkumbo kwa sababu ya umbumbumbu wako. Rudi kwenye mantiki ya thread husika tusonge na mada mkuu.
 
Back
Top Bottom