Wana CHADEMA msitukane mamba kabla hamjavuka mto

kwani ndugu kuna mtu kataja kuwa yeye ni cdm au kwa woga wako unaona ucdm?ndo ivo kama unaogopa gizani ata ukiona mti unaanza kujiuliza kuwa ama umeona shetani,au muujiza au jini refu,ni uoga tu...hata usemeje,hautaweza kutarnish image ya cdm kwa kutuhusisha sisi na cdm,hata cdm ikifa leo bado tutazidi kupinga udhalimu...watoto wa wakulima tumepata elimu kwa tabu na hatutaacha

Hueleweki ndugu, unakwenda kwa mwendo na mbwembwe za tractor aina ya power tiler. Kelele kubwa lakini kasi hakuna. Unachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja. Naomba upumzishe akili, tuonane kesho.
 
Kuna mzee mmoja aliniambia kwamba miaka ya 60 Samweli Sitta na wenzake wakiwa wanafunzi wa UDSM waliandamana wakiwa na mabango kuelekea ikulu kupinga mpango wa serikali kuwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia mafunzo ya JKT.Walikuwa hoja nyingi za msingi likiwemo hilo lakini katikati yao akachomekwa mtu wa usalama aliebeba bango linalokashfu serikali...na hiyo ikawapa serikali sababu ya kuwaaachia waingie ikulu na Mwalimu Nyerere akawalamba viboko.

Nachosisitiza hapa ni kuwa ni vizuri pia kusikiliza upande mwingine wa shilingi hata kama hoja hukubaliani nayo...lakini kinachonishtua ni namna watu wanaotoa maoni ya kukisaidia CDM wanavyoshambuliwa kwa maneno ya kejeli na dharau kana kwamba hiki ni chama cha watu wasiofanya makosa.....Na hili linanishawishi kuamini kuwa miongoni mwa watu wanaokisapoti kuna mamluki,ambao hutoa maneno ya kejeli kuonyesha wanakipenda chama kumbe wanakipaka sifa mbaya ya kukionyesha ni chama kisichokubali kukosolewa.

Haiwezekani iletwe hoja hapa halafu wanaokiunga mkono karibia wote watoe maneno ya kuponda tu bila kujadili hoja.Mtatuharibia chama na kikaonekana ni cha watu wasio kuwa na busara na wanaokurupuka.Hata miongoni mwa viongozi wa CDM wanatofautiana kwa mawazo na hoja lakini hatuwasikii wakipigana vijembe. Tafadhali viongozi muwe mnapita humu kusafisha hali ya hewa.

Kama kuna mtu atakupinga huyo akapimwe akili yake mkuu mana umemaliza.
 
Sishangai kwa vile chadema ni siyo chama Bali ni henge la kishabiki.
 
Back
Top Bottom