mimimkuu
Member
- Oct 12, 2010
- 38
- 9
Sijatumwa na mtu kusema haya. Nimejituma mwenyewe. Hapo natoa jibu la post ya kwanza kutoka kwa mashabiki wa CDM. Wala sijapokea bahasha kama kauli mbiu yenu humu isemavyo.
Najua kuwa, Viongozi wa CDM hasa Mnyika, ni watu makini sana. Wanajua nini wanafanya katika vita ya kumkomboa Mtanzania. Nawaunga mkono mia kwa mia. Sasa kimbembe ni kwa mashabiki wa chama, sina hakika kama wote wanaopiga kelele ni wanachama hai au la.
Lakini wanahitaji semina na ushauri nasaha, wapate mfundo wa kuacha hasira, jazba, chuki, hamaki, ukali na kejeli wanapoambiawa ukweli. Lazima watambue kuwa vyama navyo vina kifo, na vifo vingine hutokea ghafla kama kile cha CUF. Kwani walikuwaje wale jamaa? Sasa hivi wako wapi? Msibweteke na mafanikio ya chama kwa sasa!
Kumbukeni kuwa ndio kwanza bado kinatambaa. Wenzenu wanasherekea miaka 35, umri wa mtu mwenye mjukuu. Nyie je? Mingapi! Msitukane wakunga wakati uzazi bado ungalipo.
Kubalini ushauri, na kukosolewa pia. Mtu akikucheka, usimtukane. Jitazame kwani unaweza kuwa umejipakaza kinyesi. Na siku zote kichaa akikwambia "nyoka huyoo" usipuuze! Anaweza kuwa nyoka kweli kwani kichaa naye ana macho japo akili zake zimekaa upande...
Mbona mwenyewe unaonekana unajazba....punguza kwanza ndo ukemee wengine