Wana-CCM vileeni vyama vya upinzani visife

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,296
2,000
Kuna watu bila kujali itikadi yao ya kisiasa ambao kazi yao ni siasa. Watu wa aina hii lazima wafanye siasa maana maisha yao yote yanategemea siasa.

Kuna tofauti kubwa kati ya chama cha siasa na mwanasiasa. Mwanasiasa anaweza kufukuzwa na wenzake kutoka ndani ya chama au anaweza kukihama chama baada kukerwa na namna mambo yanavyo au yalivyoendeshwa ndani ya chama chake.

Katika nchi changa kama yetu ambayo kuunda chama cha siasa ni kazi ngumu sana na mgombea binafsi haruhusiwi bila shaka mwanasiasa aliyefukuzwa au kuhama chama atahitaji kujiunga na chama kingine harakaharaka ili maisha yake ya kisiasa yaendelee.

Hivyo Vyama vya Upinzani ni lazima viwepo na ni muhimu kwa wanasiasa wote bila kujali wewe ni nani wapi.

Ni ajabu kuona wanasiasa wa CCM wakifanya kila kitu wajuacho na wawezacho ili vyama vya siasa vife. Vyama ambavyo watavihitaji mara tu watakapofurushwa au kukerwa ndani ya chama chao.

Hii ni kuonyesha kuwa elimu zetu tulizopewa hazitoshi kabisa. Ni elimu za kutupatia nafuu ya leoleo tu isiyojali kesho kutakuwaje. Ni elimu zinazotufanya tuendeshwe na matukio ya kila siku.

Ni afya kwa mwanasiasa kuviona vyama vyote vya siasa vinakuwepo na vinakuwa ili viwe kimbilio pale wenzako watakapo kufurusha chamani.
 
Top Bottom