Wana CCM Kiwira wakamatwa kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM Kiwira wakamatwa kwa rushwa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mmwaminifu, Mar 31, 2012.

 1. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kundi la akina mama wamekutwa katika jengo la saccos Kiwira ambalo bado halijaisha wakiwa na makada (wanaume) watatu wa CCM. Wanachadema wamezunguka eneo hilo na tayari polisi wamewasili. Ikumbukwe eneo hilo linatarajia kuwa na uchaguzi wa diwani kesho.
  Source: Wapo radio
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Rushwa na CCM ni kama binadamu na roho yake. No rushwa no CCM anymore.
   
 3. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  piga haoooo
   
 4. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Lazima wapigwe maana makamanda wamepazingira tayari. Hakuna mtu kutoka hadi kieleweke!
   
 5. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hadi ninapopost habari hii, makada kadhaa wa CCM wamefungiwa ndani ya jengo moja katika mji mdogo wa Kiwira mkoani Mbeya. Hii ni kutokana na kugundulika kwamba walikuwa wanagawa hela kwa ajili ya kurubuni wapiga kura ktk uchaguzi wa udiwani utakaofanyika kesho ktk kata hii.

  Kuvuja kwa mpango huu kumetokana na kutoridhika kwa baadhi ya watu waliopata mgao wa pesa hiyo. Baada ya uhuni huu kuvuja, mara moja wafuasi wa CHADEMA walikusanyika na kuzingira jengo walimokuwa hawa makada wa CCM. Baada ya hapo walitoa taarifa polisi ambapo muda mfupi baadaye polisi kadhaa kutoka Tukuyu walifika ktk eneo la tukio.

  Lakini pamoja na hivyo, ilishindikana kuwatoa hawa watu kutokana na hasira walizonazo wafuasi wa CHADEMA. Hali hii ilipelekea OCD naye kufika ktk eneo la tukio ambaye naye pia ilionekana kama kushindwa kuwatoa nje. Hadi hivi ninavyopost hii habari, TAKUKURU wameishafika hapa. Kwa sasa anasubiriwa RPC kuja kuamua hatima ya hawa jamaa.

  Kiukweli hali kwa sasa sio shwari kwani polisi wameishaanza kulipua mabomu ya machozi. Biashara nyingi zimeanza kufungwa.

  Ila mtaniwia radhi endapo nitakuwa kimya baadaye,cos mimi mwenyewe nipo njiani napita tu. Ila naamini jf ipo kila mahali, wadau wengine watazidi kutujulisha.

  Nawasilisha.....
   
 6. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu mimi nipo ktk eneo la tukio, na polisi wameishaanza kutawanya watu kwa mabomu ya machozi.
   
 7. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mvua zinanza kunyesha sasa, huenda hali ikatulia baadaye.
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasilichome hilo Jumba moto, au lenyewe haliko Jirani na soko?
   
 9. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Du! Kama kawaida yao. Hao watuhumiwa si ndo wanatengenezewa njia nyeupe ya kusepa?
   
 10. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Hali ni mbaya sana hapa Kiwira, pamoja na mvua nyingi kuendelea kunyesha polisi wa Magamba wanaendelea kurusha mabomu ya mchozi kuharalisha Magamba wa kike kugawana rushwa. Cha kusikitisha polisi wa tz wamesomea kuwalinda kwa nguvu zote wagawa rushu, Kesho utamskia RPC akikanusha vikali kwamba wanawake wa magamba walikuwa wagawna rushwa. We subiri utasikia vijana wa CHADEMA walikuwa wakifanya vurugu tumewadhibiti.
   
 11. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kama TAKUKURU na Polisi wataendela kushindwa kuwafikisha Mahakamani hao wana CCM, siku chache zijazo watu wataanza kuchukua sheria mkononi kama wanavyowafanyia wezi sugu halafu Polisi waanze kulalamika.
   
 12. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ktk harakati za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho.ILIKUWA HIVI,viongozi wa chama cha Mapinduzi,walikaa kwenye nyumba fulani hapa kiwira,wafuasi wa Cdm wakaizingira nyumba hiyo,na kuenda kuita polisi na Takukuru.polisi walipofika wakaanza kupiga mabomu,na wafuasi wa Ccm kukimbia.
   
 13. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tupatie full story mkuu usiwe kama unafukuzwa. Kwani viongozi wa ccm kukaa kwenye nyumba fulani ndilo tatizo? Au tatizo hasa ni lipi hadi cdm wawazingire????
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Yaani mkuu polisi walifika tu na kuanza kutwanga mabomu bila hata vurugu?
   
 15. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  watu wengine wanaleta thread hapa haraka haraka bila details sijui wanawahi kuwa wa kwanza? kitu haina contents unaweka ya nini??
   
 16. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wafuasi wa Cdm walihisi hiyo nyumba,wanapeana rushwa,maana walikusanywa kinamama wapatao 70,ndani ya nyumba hiyo.Chadema walitaka polisi na Takukuru waingie ndani ya nyumba na kuchukua maelezo,cha ajabu polisi walipofika,wakaanza kupiga mabomu,ndipo wakinamama waliokuwemo ndani na viongozi wao kukimbia.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  kwani hao polisi wana akili timamu mkuu, wanaweza kukipiga mabom hata kichaka alimradi waambiwe kinataka kuandamana kwa maelekezo ya cdm.
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Story haijajitosheleza
   
 19. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kitendo hicho cha kuwataarifu polisi ndiyo kosa kubwa!! kwani ccm wanatoa taarifa polisi kuja kuwalinda dhidi ya cdm. Next time, hao wanamama, wawekeni chini muwape somo wataelewa tu. Akina mama ndiyo mtaji wa ccm saizi! Ila 2015 siyo mbali kwani kila kichwa kitakuwa kimejiandikisha na kama liwalo na liwe basi ni 2015.
   
 20. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kimbunga, wale wakinamama wenu wa Magamba walikusanyika katika nyumba hapa Kiwira wakigawana rushwa, hata hivyo gawio lilikuwa la kupunjana, mmoja wao akajifanya Yuda Isakariote! Akachomoka kuwatonya viongozi wa CHADEMA waloamua kuizingira nyumba hiyo na kuwapigia simu polisi wa Magamba. Chakusikitisha hapa Tz. CCP polisi wetu wamefundisha kuwatetea Mgamba kwa nguvu zao zote hata kama ni kumwaga damu wa watetea haki, palisi walichokifanya hapa kiwira ni kuanza kurusha mabomu ya machozi hovyo hovyo ili kuwaruhusu akinamama hao kusepa kusikojulikana!. Kesho we subiri RPC wa Mbeya kukanusha habari hii vikali.
   
Loading...