Wamkataa Mtemvu mbele ya Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamkataa Mtemvu mbele ya Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ortega, Feb 2, 2011.

 1. Ortega

  Ortega Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  *Wamshangaa ameteuliwa na nani

  Na Benjamin Masese,Temeke

  MBUNGE wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu jana alijikuta na wakati mugumu kwa kuzomewa na wananchi wake wakidai sio chaguo lao bali ni la Serikali kitendo kilichosababisha kuamusha mori za kisiasa za uchaguzi wa mwaka jana.

  Mtemvu alikumbana na mkasa huo alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi wake katika ziara ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ya kutembela miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara zinazojengwa ili kupunguza msongamano wa magari Dar es Salaam.

  Hata hivyo wakati zomeazomea hiyo ikirindima mkutanoni, Mtemvu alijitetea kwa sauti ya chini kwa kuhoji alichaguliwa na nani kama sio chaguo lao ambapo wananchi walisema wazi kuwa ni uchakachuaji wa kura hali iliyomlazimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Galawa kuingilia kati na kuwatuliza.

  Wananchi hao walidai kuwa tangu mbunge huyo ashike nafasi hiyo miaka kadhaa hakuna alichokifanya hasa upande wa barabara tofauti na mambo yake binafsi.

  Hata hivyo Magufuli alipokaribishwa na Mkuu wa Mkoa kuzungumzia na wananchi alianza kumtetea Mtemvu kwa kuwaambia kwamba watake wasitake ndio mbunge wao.

  Aliwataka wananchi kusahau mambo ya kisiasa kwa kuwa muda wa uchaguzi umeisha na kinachohitajika ni kuleta maendeleo bila kujali itikadi za vyama.

  Anasema kuwa kama serikali ingekuwa inaangalia itikadi za vyama isingekuwa inatoa huduma kwa wananchi huku akisisitiza kwamba ujenzi wa barabara zinazojengwa ni wananchi wote na hata misaada inayotolewa haiangalii vyama.

  Mbali na Magufuli kutoa ufafanuzi huo bado wananchi waliendelea kutoa maneno ya kutomtambua wala kumpa ushirikiano.

  Hata hivyo baada ya mkutano huo kumalizika kuliibuka makundi mbalimbali ya wananchi kutoka vyama mbalimbali vya siasa kurushiana maneno huku kila mmoja akidai ujumbe umewafika.

  Upande mwingine ulidai kuwa ujumbe umeifikia serikali kwmaba wananchi hawamtaki mbunge huyo na wengine wakidai kuwa serikali inamtambua.
   
 2. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Si vibaya watu kueleza hisia zao. Ila nashangaa wanafanya sasa wakati wangechukua hatua Oktoba kwenye sanduku la kura kisha nguvu ya uma Novemba nafikiri ingekuwa tamu zaidi....anyhow it is not too late to make it right.

  Ortega, tafadhali source ya habari yako hii ni gazeti au nini?
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Khaaaaa!!!!! Leo hii wapiga kura wake wanamgeuka any way its too late waliishampa jembe na nyundo
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Tisheti kofia soda na pilau ziliwalewesha
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hata mimi nawashangaa kwa nini hawakufanya hivyo october 2011 anyway wanaweza kutumia njia nyingi lah! wasubiri 2015
   
 6. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huenda walifanya lakini kura zikachakachuliwa
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Wamesema ni uchakachuaji, unataka waeleze nini zaidi??????
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  thread isiyokuwa na soource = crap
   
 9. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Wailfanya lakini tume ya uchaguzi ikafanya adjust!
   
 10. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  na hayo ndio madhara ndio maana akazomewa :msela:
   
 11. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu msiwe wasahaulifu, Temeke huyu jamaa hakushinda, matokeo yao hayakutangazwa kwa haki na wote tunajua, sema watu wa temeke sio sawa na kawe ama ubungo!
   
 12. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  na ngoma za kiduku na mchiriku:peace:
   
Loading...