Wamjua Mtu huyu? Ndiye "MO" original

Wamjua Mtu huyu? Ndiye "MO" original

MpigfilimbiwaHamelin

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2014
Posts
652
Reaction score
169

Kwa taarifa Mohamed Amin 'MO' ndiye mwandishi pekee wa habari aliyetoa ukweli kuhusu njaa ilivyokuwa inawaua watu Ethiopia. Katika miaka ya 1980s kulikuwa na njaa kubwa iliyowaua waethiopia zaidi ya 50,000. Rais wao wakati ule Dikteta Mengistu alizuia kabisa waandishi kuingia Ethiopia ili kuficha maovu/aibu hio. 'MO' mwndishi mpiga picha Mkenya alifanya ujasiri wa kujipeleka Ethiopia kupata habari. ALIMLAGHAI Mengistu hadi kumlanisha na kuingia Ethiopia akapiga picha nyingi ikiwemo ile maarufu ambayo Tai (vulture) alikuwa anamsogelea mtoto asiyejiweza kwa njaa ili amnyofoe nyama. Picha hiyo iliwaliza watu dunia nzima.
Ndipo MJ - Michael Jackson, Lionel Richie na wanamziki wengine wakaimba ule wimbo maarufu wa USA FOR AFRICA - WE ARE THE WORLD!!. nakupata fedha nyingi zilizosaidia kuoka maisha ya watu.

"MO" alianza kazi ya upigaji picha hapa Dar mwaka 1963, badaye alihamia Nairobi. Alikufa ktk ajali ya ndege akitoka Ethiopia mwaka 1996, baada ya ndege kutekwa na kuanguka karibu na visiwa vya Commoro.
Picha ya ajali ya ndege aliyopanda "MO" pia ni moja ya picha pekee iliyochukuliwa live kwa bahati tu na mtalii aliyekuwa akiogelea na mkewe beach huko Comoro

Tazama hapa
www.youtube.com/watch?v=Ob8nE4f2ZWc
 
Back
Top Bottom