Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu ni kuhusu watangazaji wa michezo hasa katika suala la soka. Inanikera pale unaposikia watangazaji wakijikita kujadili timu/ligi moja (EPL) na kuacha kutuhabarisha mechi/michuano mingine. Hivi sasa pana michuano ya FIFA U20 fainali inafanyika Korea Kusini lakini, mfano jana,Clouds ,FM katika kipindi chao cha michezo usiku walijikita EPL na kuacha kujikita katika uchambuzi wa michuano hii. Nawaomba wamiliki wa vyombo vya habari wasiwape uhuru uliopindikia wawapo kazini japo wawe wakifuatilia hali ya mambo katika vipindi hivo.