Wamiliki wa Magari Adimu (brand tofauti na TOYOTA, Magari yenye changamoto ya upatikanaji wa Spare Parts) Tukutane Hapa

Dreamlinerz

Member
Jun 17, 2019
62
77
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Sisi wamiliki wa magari ambayo ni brand tofauti na TOYOTA tunapata changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea wengine kushindwa kuyahudumia magari yao na mwisho kuachana nayo au kuyatelekeza kwenye magereji au kuyauza kwa bei ya HASARA kitu kinachopelekea magari haya kuonekana hayafai na watu wengi kusita na kuogopa kuyanunua.

Sasa basi Uzi huu ukawe msaada wa kupeana habari,taarifa,na huduma ambazo zitapelekea kusaidia kupunguza adha ya kuhudumia magari yetu kuanzia kwenye upatikanaji wa spare parts kwa bei reasonable na mafundi wenye ujuzi wa kuzielewa hizi gari.

Mimi binafsi nimeshakutana na changamoto nyingi kwa kumiliki ka gari kangu kadogo aina ya VW POLO, nimevumilia matatizo mengi ya mafundi na bei kubwa za spare tangu nimeanza kukamiliki lakini kilichonitokea juzi juzi hapa ndicho kilichopelekea mimi kuleta huu mjadala humu jukwaani ili tuweze kusaidiana na mwishowe magari haya yaonekane ya kawaida na isiwe adhabu kuyamiliki.

Gari yangu ilikuwa na tatizo la fuel pump la muda mrefu kidogo baada ya kuwekewa mafuta machafu,kwahiyo ilikuwa na tatizo la kuchangaya, ilikuwa naweza kusimama kwenye mataa taa zikiruhusu gari inakosa nguvu ya kwenda kabisa kiasi kwamba magari ya nyuma yangu yananipigia honi, fundi akaniambia hiyo itakuwa tatizo ni fuel pump, ikabidi niingie mtandaoni nikakutana na jamaa anauza spare za magari mbalimbali sitamtaja humu basi fuel pump bila housing yake ilinitoka 250,000/=

Pamoja na kubembeleza nipunguziwe bei haikusaidia ilinibidi ninunue tu kwasababu gari ndio ninayoitumia kwa mizunguko yangu mjini lakini iliniuma sana kwasababu najua online aliexpress fuel pump hiyo isingezidi 70,000 mpaka kuipata lakini ingenibidi nisubiri wiki tatu au zaidi na hiyo ndio ilikuwa changamoto

Na hiyo sio mara ya kwanza kununua spare kwa bei mbaya kuizidi hii, changamoto ni nyingi sana kwahiyo wale wamiliki wenzangu wa magari haya adimu, mafundi, wauzaji spare tukutane hapa tuelezee changamoto tunazokutana nazo ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kusaidiana.

Nawasilisha.
 
Usimiliki gari kama hauna uwezo baki na miguu yako
ujumbe wako wapo unaowahusu,lakini ukisoma vizuri nilichoandika sio kwamba siwezi kumiliki ila tatizo naweza kuwa na pesa ila spea hupati au unauziwa spea kwa bei za kukomoa.

Kwahiyo hapa tunatafuta solution kwa kupeana taarifa labda wapi mtu atapata spea kwa bei reasonable iwe ni kwa kuagiza nje au mtu anakuja bongo mnamuagiza spea kwa pamoja mnamchangiabaadhi ya gharama na vitu kwama hivyo, ndio lengo la hii mada.
 
Polo naionaga kama Vitz ya VW vile ila mkuu jitahidi uwe na urafiki na dealers wanaofanya kazi kwenye garage au kubwa zibazotengeneza hayo magari i.e sina uhakika kama ni CFAO au DT
Dobie
Hapo labda nikiupgrade nipate VW POLO ya 2013 ambapo sifikirii kwa sasa kutokana na shida ya upatikanaji wa spare na mafundi wa haya magari,kama mafundi na wauza spare wa mtaani wanaturingia namna hii vipi hao wa dealers itakuwaje?
 
Hapo labda nikiupgrade nipate VW POLO ya 2013 ambapo sifikirii kwa sasa kutokana na shida ya upatikanaji wa spare na mafundi wa haya magari,kama mafundi na wauza spare wa mtaani wanaturingia namna hii vipi hao wa dealers itakuwaje?
Unajua hao dealers possibility ya kua wana garage za mtaani ni kubwa sana huwezi jua unaweza ukawa unapata hata spea kwa bei ya punguzo fulani
 
Huyu jamaa nimemkubali sana, nilikuwa natafuta spare ya nissan bluebird hapa dar naambiwa 360,000 ila nilipomcheki yeye kaniagizia nje nadhani nairobi kwa 140,000 ndani ya siku mbili mzigo nikaupata na sasa nadunda mtaani.
 
Asante kwa taarifa,naona wahusika wamenisaidia.
Mkuu ulikuwa sahihi ukiona mtu anajibu pumba kwahuu uzi uliouleta ujuwe huyo anamiliki baiskel achana naye mimi nimemiliki mazda imenitesa kwenye spea najuta kwenye Toyota kifaa cha 125000 mazda utapata kwa 400,000 wakati huo spea nishida kuzipata, kwa ushauli mfuko ukituna gari yakununua ni Toyota
 
Back
Top Bottom