Wamiliki wa maduka ya uwakala wa mabenki na chuma ulete

Joasi

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
768
667
Ndugu habarini,

Hapa ni nyumbani naomba tupeane uzoefu.

Binafsi nipo na ofisi ya Uwakala wa mitandao ya simu na Banks kama wakala wao.

Tatizo nalokutana nalo ni chuma ulete au sijui ni kiini macho.

Tarehe 23.3.2022 alikuja mteja kwa bashasha sana na aliweka 50,000 asubuhi kama saa 2 hivi.

Saa 8 mchana akarudi na sh 20,000 nimwekee Aitel na nikaandika kwa usahihi kabisa.

Cha kushangaza baada ya dk45 nahisi tu kama yule mteja nimemzidishia kiwango.

Kucheck nakuta nimetuma 200,000.

Aisee siku ilikuwa ngumu sana kwangu ngumu mno mno.

Na niliwahi poteza 1,900,000 kwa namna nisiyoijua kabisa.

Na nikaiweka ni chuma ulete.

Kuhusu kufunga hesabu aisee sijawahi Acha kufunga hesabu kwa kweli.

Baada ya hapo ilinibidi nihame na kutokana na uchache wa wateja.

Huku nilipoami nimerekebisha vizuri ofisi sasa HOFU yangu ni Chuma ulete naona inaweza kuniletea shida tena sijiamini kabisa

Naomba wajuvi wa kuzuia hili jini yaani mnisaidie kutatua .

Mawakala wa kutoa huduma za kifedha naomba mine experience yenu also wajuvi wa namna ya kutatua hii hali .

Nitakuja na mrejesho wa kufanikiwa kuizuia kama nitapata suluu hapa jamvini.
 
Nakumbuka mwaka 2017 kuna siku nilienda kutoa pesa kwa wakala wa tigo pesa kusudi langu ilikuwa kutoa elfu 50 kumbe nimetoa laki 5. Baada ya muda yule dada kanipigia kuniambi kuwa kumbe nimemtumia laki 500 badala ya elfu 50 na akaniahidi atanirudishia pesa yangu.
Nilisubiria na kweli baada ya wiki moja yule dada kanitumia ile pesa yangu laki 450 na nilikuwa simujui na yeye alikuwa hanijui. Sijui yuko wapi ila popote alipo God bless her.
 
Mwanzo nilikua nagombana na wife kwenye ofisi yetu ya uwakala, yeye alikua anachukua matumizi hapo hapo akitegemea ikitoka commission afidie cha ajabu kila ikifika mwisho wa mwezi anakuta mtaji una drop, yeye alikua ana force kila siku twende kwa waganga tukatafute dawa ya kuizuia chuma ulete la sivyo Biashara tutaifunga, mimi nikawa namwambia chuma ulete ni wewe mwenyewe kwenye hii Biashara, nikamuacha mpaka mtaji uka drop kabisa mpaka akawa anaona aibu kukaa ofisini maana kila mteja akija kutoa hela au kutuma anamwambia sina flot au sina keshi, nikapambana kwenye shughuli zangu za kilimo nikamtafutia mtaji mzuri, nikamboreshea ofisi, nikawa namtengea hela ya kutumia pembeni na nikamwambia kila ikiisha uniambie, ikawa kila jioni nikamuelekeza kufunga Hesabu, sasa hivi yeye ndio balozi wa kuwaambia wanawake wenzake kwamba hakuna chuma ulete kwenye Biashara, chuma ulete katika Biashara ni wewe mwenyewe
 
Kuna watu huwa hawapo makini sana na tarakimu,anaweza akaja mtu anataka kudeposit 3000tsh yeye akaweka 30000tsh au 5000tsh yeye akaweka 50,000tsh au 17500tsh yeye akaweka 175000tsh,umakini unahitajika sana kwenye hii biashara kinyume na hapo utalia chuma ulete kumbe chuma ulete ni wewe mwenyewe
 
Ndugu habarini,

Hapa ni nyumbani naomba tupeane uzoefu.

Binafsi nipo na ofisi ya Uwakala wa mitandao ya simu na Banks kama wakala wao.

Tatizo nalokutana nalo ni chuma ulete au sijui ni kiini macho.

Tarehe 23.3.2022 alikuja mteja kwa bashasha sana na aliweka 50,000 asubuhi kama saa 2 hivi.

Saa 8 mchana akarudi na sh 20,000 nimwekee Aitel na nikaandika kwa usahihi kabisa.

Cha kushangaza baada ya dk45 nahisi tu kama yule mteja nimemzidishia kiwango.

Kucheck nakuta nimetuma 200,000.

Aisee siku ilikuwa ngumu sana kwangu ngumu mno mno.

Na niliwahi poteza 1,900,000 kwa namna nisiyoijua kabisa.

Na nikaiweka ni chuma ulete.

Kuhusu kufunga hesabu aisee sijawahi Acha kufunga hesabu kwa kweli.

Baada ya hapo ilinibidi nihame na kutokana na uchache wa wateja.

Huku nilipoami nimerekebisha vizuri ofisi sasa HOFU yangu ni Chuma ulete naona inaweza kuniletea shida tena sijiamini kabisa

Naomba wajuvi wa kuzuia hili jini yaani mnisaidie kutatua .

Mawakala wa kutoa huduma za kifedha naomba mine experience yenu also wajuvi wa namna ya kutatua hii hali .

Nitakuja na mrejesho wa kufanikiwa kuizuia kama nitapata suluu hapa jamvini.
Tafuta tiba Hao mbuz wapo

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Kuwa Makini Kama unashindwa tafuta MTU muwe wawili.
 
Sehemu nilipoweka, mwenzangu amefunga sababu ya chuma ulete...

Basi namimi nawavimbia mie ndo mchawi karba mwenyewe wananishindwa wananiogopa 🤣🤣🤣🤣🤣 maana ukiwaambia hakuna chuma ulete mtabishana.

Ukweli ni huu umakini na kupiga mahesabu.
Pesa bila daftari huisha bila habari.
 
Hii biashara haina uchawi wala chuma ulete. Umakini ndiyo kila kitu. Ukikosa tu umakini, basi chuma ulete naye hatacheza mbali.

Mfano amekuja mteja kuweka 20,000/=, sasa wewe na mawazo yako ukamuwekea 40,000/=!! Hapo lazima chuma ulete asingiziwe.
 
Back
Top Bottom