Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Sorry Kama nitakuwa nimekuelewa tofauti maybe. Kinachokusumbua sasa hivi Ni Ile trauma uliyoipata after kushuhudia kilichomkuta mkeo Kule guest, na si Dharau zake alizokuwa nazo before. Kwa sababu kama uliweza kuvumilia Dharau zake Miaka yote hiyo, Leo ndo zimekuchosha? Mkeo alikuwa na mapungufu yake but silaha yake kubwa ilikuwa Ni "UAMINIFU" na ndo maana hukuweza kuamua cha before. Kwa yeye kubakwa, naelewa unavyojisikia coz Ni Kama amelala na mwanaume mwingine, kitu ambacho wanaume wengi hamuwezi kuvumilia.

If u were seeking for revenge, I guess this is not the right time yet. Na inawezekana mkeo akabadilika after this incidence. Angeweza kubakwa hata Kama angekuwa msikivu kwako. Leo limemfika yeye, Kesho wewe hujui litakalokupata au Huyo atakayekuja Kuwa mkeo atapatwa na janga gani. Ila viatu Ni vya kwako, so wewe ndo unayejua vinavyokukaa
 
Kuna ndoa zaidi ya tendo? Unless unambie kuwa wanaume these days ni materialists...
Umesoma alichoandika...???ni wangapi humu mnaweza sema wake zenu kwa bedi ni perfect?????

Jamaa kamsifu mkewe kabisa kwa huduma anayopata usiku afu useme hakuna ndoa...
Hivi unajua maana ya ndoa...unajua mila nyingi za kiafrika huwezi RITHI ukweni

Kwa hiyo wewe kwako ndoa ni ngono tu basi, kama mkeo akiwa anatoa tunda la roho bila hiyana hata awe hakuheshimu, anakutukana, anakudharau,nk hakuna tatizo?

Sasa huyo mke atakua tofauti gani na changu wa mtaani.

Definition yako ya ndoa imenimaliza nguvu.
 
Thats how a real man acts😊😀😀

Halafu kingine ni kwamba,, kasema mke kabakwa na hajihusishi na hio kesi,,
Hapo ndugu lazma waone kama huyu jamaa aliandaa hao wabakaji, ili kumkomesha wife...

Dunia ina mambo?!

Wivu tu. Haiwezekani kosa moja tu usahau wema wa mkeo to that extent eti unaenda kunywa bia unalala.

BTW hata Mimi LA kuwa accessory to the rape nimeliwaza.

Just saying.
 
Kwa hiyo wewe kwako ndoa ni ngono tu basi, kama mkeo akiwa anatoa tunda la roho bila hiyana hata awe hakuheshimu, anakutukana, anakudharau,nk hakuna tatizo?

Sasa huyo mke atakua tofauti gani na changu wa mtaani.

Definition yako ya ndoa imenimaliza nguvu.

Mtu hawezi acha kukuheshimu akakupa tunda wewe...unless awe amekugeuza dildo...na ndio kama kwenye mechi mpo compatible ndoa haiwezi kamwe ku shake...hayo mengine ni mbwembwe tu


Tatizo vijana siku hizi mnavizia kuoa watoto wa vigogo mkitegemea kukwamua maisha (ntoke vipi)..
Ndo maana kuna wazee hawataki wakwe class ya chini kuhofia watoto zao kugeuzwa mtaji
 
Wivu tu. Haiwezekani kosa moja tu usahau wema wa mkeo to that extent eti unaenda kunywa bia unalala.

BTW hata Mimi LA kuwa accessory to the rape nimeliwaza.

Just saying.

I agree .. ningekuwa ndugu Wa huyo Kaka au Mke kusema kweli ningempiga kibao kwa unyama anaoufanya.. yaani kweli unapata ubavu Wa kwenda kunywa bia bila kutaka kujua hali ya mkeo kweli ni haki... wakaka mnaelekea wapi? Mangapi sisi tunayabeba kwa sababu yenu.? ..
 
Mi nahisi wewe ndiye umetafuta hao watu wamshikishe adabu na upate sababu ya kumuacha.Maana alikukera kupitiliza.

Hata mie niliwaza ivo, anaweza itwa aisaidie mahakama katika upelelezi, na jee watoto watamuonaje yeye kama baba, amejisafisha nafsi yake ana hakika watoto watapenda hukumu aliyoitoa?
 
Mkuu, kwanza nikupe pole!

Pili, kwa kadiri ya maelezo yako wewe ndie chanzo cha mkeo kujenga dharau juu yako!

Tatu, natamani ningesikia na upande wa pili (mkeo) pia maana ni ngumu kutegemea one side story kuweza kupata ukweli halisi.

Nne, mali za urithi alizoachiwa mko hazikuhusu hivyo sioni tatizo kama hajakushirikisha kakt hilo, cha muhimu wewe unajua kuwa mkeo ana ukwasi wa mali za urithi.

Tano, nashangaa kama kweli ni wanandoa ila mnachukuliana kama wapangaji ktk nyumba moja. Inawezekanaje mkeo anakuaga anaenda kuangalia shamba B'moyo, kitu ambacho hajakushirikisha na wala hujishughulishi kumuhoji kutaka kujua kulikoni! Matokeo yake ndio kaishia kwenye mikono ya wabakaji. Kifupi umeshindwa kutimiza wajibu wako wa kumlinda mkeo!

Sita, baya zaidi mkeo kapatwa na tatizo ambalo wewe ulitakiwa kuwa mstari wa mbele ktk kumsaidia kinyume chake umesimama mbali na kuwa mtazamaji..., eti kisa huko nyuma ulishamkanya lakini hasikii! Wahenga walisema mtoto akinyea mkono hupaswi kuukata bali unausafisha na maisha yanaendelea!

Saba, inakuwaje mkeo anaenda aendako akirudi ndio anakupa taarifa kuwa alikwenda kitchen party n.k..? Inaonekana wewe ni mwanaume mwenye gubu, usiyempa mkeo hata uhuru wa kuhudhuria matukio kama kitchen party n.k.

Ushauri: Punguza jazba/hasira kwa sababu hazitatui tatizo. Simama na mkeo ktk wakati huu mgumu alionao na pia fikiria mstakabali wako wa familia yako.., wanao n.k.

Kila kheri
 
Wakuu salaam,

Mimi ni mwenyeji humu ndani ila tu kutokana uzito wa habari hii niliona nije under cover kwa miaka 4 niliyokaa Jf kuna ambao tunajuana personally na ni wengi tu.

Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.

Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.

Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."

Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.

Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.

Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.

Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.

Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.

Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.

Tulikotoka na mwanamke huyu:-

Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)

Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.

Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.

Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaño yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.

Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.

Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.

Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.

Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.

Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.

Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.
kwa kuwa ulishapanga kumuacha we muache tu sababu akuna namna nyingine.
 
Ingawa stori nyingi za humu ndani ni chai....


Umeongra meeeeeengi lakini ukiangalia ulichokiandika ni hasira ya pesa/ madili /mafanikio ya mkeo ndio yanayokutesa

Na umetumia kubakwa kwake kama sababu


Nikirudi kwa wanawake...mnachochagua waume chagueni wanaume sio tu wanaowapenda kwa dhati kiasi cha kuwa tayari kusupport ndoto zenu. ..watakawaelewa..... na kujitoa kwenu kwa hali na mali.....mwisho mhakikishe Nyumba yenu iwe na mawasiliano

Kaka yupo sahihi kabisa kumuacha huyu mwanamke.nikisoma between lines ni kwamba huyu mwanaume alishamchoka huyu mkewe kwa tanbia zake chafu ila alikuwa anatafuta sababu tu ya kumuacha.huyu mama ana fikra za kimasikini sana.kwamba mali alizorithi kutoka kwa baba yake hataki mumewe azijue wala azifaidi hata chembe.well kama alitaka hivyo basi angewaachia ndugu zake/kaka zake wachukue zote then yeye abaki kwa mumewe kwa roho safi.lakini kama amezipokea hakuna namna ambayo familia ya mumewe itaacha kufaidi nazo kwa namna moja au nyingine.na ukiangalia maelezo ya huyu jamaa wala hana mpango na hizo mali ila sasa zinamfanya mkewe anakuwa too busy na issues ambazo hazijengi zaidi ya kubomoa familia.hapo hakuna familia tena kila mmoja achukue hamsini zake kwa sababu ya ubinafsi wa mama.
 
Unatoka tangu asubuhi bila kumtaarifu mumeo na watu ambao mumeo hawajui tena wanaume wawili. Wanaamua kwenda kunywa huko walikoenda hadi hao wahuni kumtilia madawa, ana simu kwenye begi lake lakini hakuona umuhimu wa kumtaarifu mumewe yuko wapi na akina nani au hata kumtaarifu mama yake yuko wapi na akina nani. Kamsababisha mumewe mpaka aingie mochwari kuangalia miili isiyomhusu zoezi ambalo si rahisi hata kidogo. Nakubaliana nawe kabisa amevuna alichopanda huyu, mume hapa hastahili kubebeshwa lawama zozote.

Huu ndo tunaouta kujenga hoja siyo kutumia hisia.

Mwanamke awajibike kwa uovu wake. Usipofunzwa na mamayo, utafunzwa na ulimwengu. Bahati mbaya ni kwamba dunia haikuchukulii kama mtoto bali kama dunia
 
Kaka yupo sahihi kabisa kumuacha huyu mwanamke.nikisoma between lines ni kwamba huyu mwanaume alishamchoka huyu mkewe kwa tanbia zake chafu ila alikuwa anatafuta sababu tu ya kumuacha.huyu mama ana fikra za kimasikini sana.kwamba mali alizorithi kutoka kwa baba yake hataki mumewe azijue wala azifaidi hata chembe.well kama alitaka hivyo basi angewaachia ndugu zake/kaka zake wachukue zote then yeye abaki kwa mumewe kwa roho safi.lakini kama amezipokea hakuna namna ambayo familia ya mumewe itaacha kufaidi nazo kwa namna moja au nyingine.na ukiangalia maelezo ya huyu jamaa wala hana mpango na hizo mali ila sasa zinamfanya mkewe anakuwa too busy na issues ambazo hazijengi zaidi ya kubomoa familia.hapo hakuna familia tena kila mmoja achukue hamsini zake kwa sababu ya ubinafsi wa mama.

Tania zake chafu ni kama IPI?
 
Huwa najiuliza maswali mengi sana. Kwa nini watu tunathamini sana vile vinavyoweza kupatikana na kila mtu kuliko yale ambayo unaweza ukaishi maisha yako yote na usiyapate. Wangapi wana mapesa mengi ya ajabu na hawana hata mtu wa kuwaambia habari? Watu wenye mali na pesa zao wanafanya makosa na kujipata kwenye shida nyingi kwa sababu hawakupata wa kuwaambia na kuwakanya hapo unakosea. Kila mtu anaweza akapata pesa lakini wachache sana watapata wenzi wanaowapenda na kuwasupport mpaka vile ambavyo havifai kussuport. Hebu tujifunze kuwa na priorities.

Kuna haja gani ya kufanya kazi 24/7 kama wale ninaowapenda hawatafurahia jasho langu. Huyu dada pole zake anafanya kazi hata Jumapili. Kama kulikwa na ulazima wa hilo dili kufanyika siku hiyo mi ningebeba wote isipofanikiwa siku inakuwa haijaenda bure. Sioni sababu ya kuficha ficha as wanaotakiwa kufaidika ni familia yangu. Huu kwangu ni ubinafsi mbaya kabisa. Hana muda na nyumbani na kile anachotafuta hakionekani anatafuta kwa ajili ya nani?

Hakuna binadamu perfect mapungufu ya kibinadamu ni mengi mno, we need all kind of support kuliko chochote kile, no matter the situation hakuna binadamu anastahili kubakwa iwe funzo la makosa yake. Sasa ndio wakati anahitaji support ya wanaomzunguka nevile pablo after all yeye ni mama wa watoto wako. Mpe support ya kutosha hope ata recover ndio mambo mengine yaendelee.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kila mtu anajua kwa nini yuko ndoan. Anyway, your life, your rules.
 
Egocentirc....

Priorities haziji tu, ni vitu vinajengwa katika makuzi. I wish tungeiona dunia kwa jicho unaloona wewe.

Huwa najiuliza maswali mengi sana. Kwa nini watu tunathamini sana vile vinavyoweza kupatikana na kila mtu kuliko yale ambayo unaweza ukaishi maisha yako yote na usiyapate. Wangapi wana mapesa mengi ya ajabu na hawana hata mtu wa kuwaambia habari? Watu wenye mali na pesa zao wanafanya makosa na kujipata kwenye shida nyingi kwa sababu hawakupata wa kuwaambia na kuwakanya hapo unakosea. Kila mtu anaweza akapata pesa lakini wachache sana watapata wenzi wanaowapenda na kuwasupport mpaka vile ambavyo havifai kussuport. Hebu tujifunze kuwa na priorities.

Kuna haja gani ya kufanya kazi 24/7 kama wale ninaowapenda hawatafurahia jasho langu. Huyu dada pole zake anafanya kazi hata Jumapili. Kama kulikwa na ulazima wa hilo dili kufanyika siku hiyo mi ningebeba wote isipofanikiwa siku inakuwa haijaenda bure. Sioni sababu ya kuficha ficha as wanaotakiwa kufaidika ni familia yangu. Huu kwangu ni ubinafsi mbaya kabisa. Hana muda na nyumbani na kile anachotafuta hakionekani anatafuta kwa ajili ya nani?

Hakuna binadamu perfect mapungufu ya kibinadamu ni mengi mno, we need all kind of support kuliko chochote kile, no matter the situation hakuna binadamu anastahili kubakwa iwe funzo la makosa yake. Sasa ndio wakati anahitaji support ya wanaomzunguka nevile pablo after all yeye ni mama wa watoto wako. Mpe support ya kutosha hope ata recover ndio mambo mengine yaendelee.
 
Thats how a real man acts[emoji4][emoji3][emoji3]

Halafu kingine ni kwamba,, kasema mke kabakwa na hajihusishi na hio kesi,,
Hapo ndugu lazma waone kama huyu jamaa aliandaa hao wabakaji, ili kumkomesha wife...

Dunia ina mambo?!

Real men never do such silly acts...
Ushajiuliza upande wa pili kimetokea nini hadi jamaa wakambaka mke wake?...
Labda tuseme jamaa ameamua kwa pupa na hasira na inaelekea alikuwa anasubiri wakati muafaka wa kurevenge...
Jamaa atumie busara awatafute hao majamaa akae aongee nao asikie upande wa pili....
Kubaka sio kazi rahisi kama tunavyodhani na mbaya zaidi ni mke wa mtu...
Kuna sehemu huyu mdada alikosea kikubwa ndo maana wabaya wake wameamua kufanya unyama wa aina hii...
Unaweza kujidai kuingilia hii kesi kwa pupa na kujidai kuwazika wabaya wako kumbe mkeo alikosea sehemu kubwa sana na mbaya zaidi wewe unaweza kujikuta jela baada ya kufanya ujinga kama huo...
Hapa busara zinahitajika kwa kiasi kikubwa, jamaa awashirikishe watu wazima wa karibu kumsaidia kwenye maamuzi au wampe busara ya nini cha kufanya...
Jamaa angeingiwa na utu na ubinadamu wa kumpa faraja mke wake hadi mambo yatakapokuwa shwari then asikilize nini sababu ya yeye kubwakwa then afanye maamuzi muafaka ambayo anaona yatamfaa...
Kwa sasa kumuacha italeta picha mbaya sana na inawezekana hata hao polisi wakamuweka kwenye kesi kuwa alisuka huo mpango...
Wakati mwingine wanawake wanatuvumilia sana kwenye kila hali ila tunashindwa kuwavumilia pale wanapokosea...
Mke wake anaweza kugeuka malaika baada ya madhoruba haya kumtokea...
 
Da! Hiki nacho kisa! Mie naona hao jamaa wala hawakuwa na tamaa za kimwili zaidi ya kumkomoa.nahisi kwenye dili zake kuna fedha aliwarusha wakaona wajilipe kwa uroda.pole sana jamaa.
 
Back
Top Bottom